settings icon
share icon
Swali

Je! Mungu hupeana maono kwa watu hii leo? Wakristo wanastahili kutarajia maono kuwa sehemu ya uzoefu wao wa Ukirsto?

Jibu


Mungu anaweza kupeana maono kwa watu hii leo? Naam! Mungu hupeana maono kwa watu hii leo? Pengine. Tunastahili kutarajia maono kuwa kama tukio la kawaida? La. Vile imeandikwa kwa Bibilia, Mungu alinena na watu wakati mwingi kwa njia ya maono. Kwa mfano Yusufu, mwana wa Yakobo; Yusufu, mume wa Mariamu; Suleimani; Isaya; Danieli; Petero; na Paulo. Nabii Yoeli alitabiri umwagikaji wa maono, na hii ilitibitishwa na mtume Petero katika Matendo ya Mitume mlango wa 2. Ni muimu kujua kwamba tofauti kati ya maono na ndoto ni kuwa maono hupeanwa wakati mtu ako macho bali ndoto hupeana wakati mtu amelala.

Katika sehemu nyingi za dunia, Mungu anaonekana akitumia maono na ndoto sana. Katika sehemu ambazo kuna uchache au hamna ujumbe wa injili karibu, na mahali ambapo watu hawana Bibilia, Mungu anachukua ujumbe wake kwa watu moja kwa moja kupitia kwa ndoto na maono. Hii yote inakubalina na mfano wa Kibibilia wa maono kutumika kila wakati na Mungu kufunua ukweli wake kwa watu katika siku za mwanzo mwanzo wa Ukristo. Ikiwa Mungu anakusdia kuwasiliana ujumbe wake kwa mtu, Anaweza njia yo yote ile anapata zinastahili kuptaina maono yake katika sehemu zile ujumbe wa injili tayari unapatikana. Hakuna kizuizi kwa kile Mungu anataka kukitenda.

Kwa wakati huo huo, lazima tuwe macho sana wakati inafikia maono na kufasiri maono. Lazime tuweke katika akili kuwa Bibilia imekamilika, na inatuambia kila kitu tunastahili kujua. Ukweli kuu ni kuwa ikiwa Mungu alikuwa anapeana maono, yatakubaliana kabisa na chenye kimekwisha funuliwa katika neno lake. Maono kamwe yasiwai pewa mamlaka sawa au mamlaka zaidi kuliko neno la Mungu. Neno la Mungu ndio mizani yetu kwa Imani ya Kikristo na matendo. Kama unaamini kuwa umepokea maono na unahisi kuwa ni Mungu alikupa, kwa kusali chunguza chenye neno la Mungu na akikisha maono yamekubalina na maandiko. Kwa kusali kichukulie kile Mungu anakutaka ufanya kwa uzito kuambatana na maono (Yakobo 1:5). Mungu hawezi mpa mtu maono na aifiche maana ya maono. Katika maandiko, popote mtu alimuuliza Mungu maana ya maono, Mungu aliakikisha ilielezeka kwa huyo mtu ( Danieli 8:15-17).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mungu hupeana maono kwa watu hii leo? Wakristo wanastahili kutarajia maono kuwa sehemu ya uzoefu wao wa Ukirsto?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries