settings icon
share icon
Swali

Je! Mapepo yapo?

Jibu


Biblia inazungumzia kuhusu mapepo kuwa viumbe halisi. Hata hivyo, maelezo ya Maandiko kuhusu mapepo ni tofauti sana na dhana inayojulikana na wengi kuwahusu. Biblia inaelezea mapepo kuwa wenye nguvu lakini kwa kiwango na mwishowe ni viumbe watashindwa. Hao ni malaika waliomfuata Shetani katika kuasi Mungu “Ufunuo 12:3-4). Biblia haitoi maelezo mengi kuhusu mapepo, lakini yale imepeana yanatosha kuonda hekaya za kawaida.

Mapepo yanarejelewa kwa majina kadhaa mbadala, ikiwa ni pamoja na “pepo wachafu” na “pepo wabaya.” Baadhi ya miungu ya uwongo iliyopokea dhabihu za wanadamu inaelezewa kuwa pepo halisi (2 Mambo ya Nyakati 11:15; Kumbukumbu la Torati 32:17). Kwa kuwa mapepo na malaika walioanguka, wanamiliki kiwango sawia cha nguvu na ushawishi kama malaika wa kweli. Hata hivyo, Maandiko yanaonekana kuonyesha kwamba Mungu amewekea mipaka uwezo wao (2 Wathesalonike 2:6-7). Biblia inaonyesha kwamba sio mateso yote yanatokana na ushawishi wa mapepo (Mathayo 10:1; Luka 8:2). Sehemu kubwa ya ushawishi wa mapepo ni ya kiroho, sio kimwili.

Tamaduni maarufu mara nyingi huonyesha mapepo katika umbo la kutisha. Hii ni pamoja na jino la mnyama, makucha makali, mbawa za ngozi, na kadhalika. Au wanaonyeshwa kama kivuli au vizuka. Kati ya haya, hakuna yenye msingi wowote wa kibilbia. Kwa kweli, Biblia hailezei jinsi malaika walionguka wanavyoonekana. Kama ilivyo kwa malaika wa kweli, mapepo ni viumbe vya kiroho ambavyo vina ushawishi wa kiroho, kwa hivyo kuna uwezekano kuwa hawana mwili wa kawaida. Ikiwa wataamua kuchukua mwonekano wa mwili, kwa hakika inaleta maana zaidi kwao kuchagua umbo ka kuvutia badala ya lile ya kutisha (2 Wakorintho 11:14).

Kwa hivyo, mapepo ni viumbe halisi. Mapepo yaliyoelezewa katika Biblia yapo. Hata hivyo, aina ya pepo katika filamu za kutisha na mtindo wa Halloween hayapo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mapepo yapo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries