settings icon
share icon
Swali

Mkristo anapaswa kuhusianaje na marafiki wasio Wakristo?

Jibu


Mkristo anapaswa kuhusiana na marafiki wasio Wakristo jinsi na namana Yesu alivyohusiana na wale ambao hakukumfuata. Tunaweza kuangalia njia chache ambazo Yesu alihusiana na watu na kumwigi tunapohusiana na marafiki zetu wasio Wakristo:

1. Yesu alikuwa mwema, hata wakati watu hawakumwelewa. Watu walichanganyikiwa daima kuhusu Yesu alikuwa nani na kwa nini alikuwa katikati yao. Lakini Marko 6:34 inaandika kwamba, “Yesu alipofika kando ya bahari, aliona makutano makubwa ya watu, akawahurumia kwa maana walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Kwa hiyo akaanza kuwafundisha mambo mengi.” Wajehuri walimpinga; lakini Aliwajibu kwa upole (Luka 8:43-48). Askari wa Kirumi na wakereketwa wa dini walimuua; Alijibu kwa upole (Luka 23:34).

Yesu alikuwa tayari kueleweka vibaya, hivyo angeweza kuwa na subira na fadhili na wasio Wakristo alipokuwa akieleza jinsi ya kuwa na uhusiano na Mungu. Tunahitaji kukumbuka kwamba kama wafuasi Wake sisi, pia, tutaeleweka vibaya. Yesu alituonya, “Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba ulinichukia mimi kabla yenu” (Yohana 15:18). Hata tunapochukwa au kutoeleweka, tunapaswa kujibu kwa fadhili siku zote.

2. Yesu alisema ukweli kila wakati. Hata maisha Yake yalipokuwa hatarini, Yesu alizungumza ukweli kila mara (Mathayo 26:63-65). Tunapozungukwa na wasio Wakristo ambao hawamwabudu Mungu au kushikilia maadili yetu, inatushawishi kunyamaza au kuafikiana na Maandiko ili tusiudhike. Wakati fulani tunaona haya yakitokea kwa Wakristo maarufu wanapoulizwa kuhusu ushoga au uavyaji mimba. Badala ya kusimama imara juu ya kweli ya Neno la Mungu, wengine hushindhwa na msukumo wa marika.

Mvuto wa kuelekea kuwafurahisha wale walio karibu nasi ni tatizo la wanadamu wote. Lakini, kama Wakristo, tunapaswa kuwa “chumvi na nuru” katika uliwengu huu wa giza, usio na ladha (Mathayo 5:13-16). Hatupaswi kuwashinda watu kiakili kwa maoni yetu (ona nambari ya 1, hapo juu), lakini pia hatupaswi kuachilia ukweli. Yesu alizungumza kile kilichohitajika wakati huo bila kujali gharama ya kibinafsi. Alizungumza kile ambacho watu walihitaji kusikia. Lazima tufanye hivyo, pia.

3. Yesu kamwe hakupoteza utambulisho Wake. Ingawa alizungukwa na wasio Wakristo kila siku, Yesu hakuruhusu utamaduni au maoni yake kubadili utambulisho Wake. Hata Shetani hangeweza kumtikisa (Mathayo 4:1-10). Yesu alijua Yeye ni nani na kwa nini alikuwa hapa. Kama Wakristo, ni lazima tuwe salama katika utambulisho wetu katika Kristo ili hata mpinzani mwenye sauti kubwa asiweze kututikisa. Yesu alikula, kunywa, na kusafiri na wasio Wakristo kila siku, lakini Hakuweka kando utambulisho Wake kama Mwana wa Mungu na angeweza, kwa hiyo, kusema kweli, “Yeye aliyenituma yu pamoja nami, hajaniacha, kwa kuwa siku zote nafanya mapenzi yake”

4. Yesu alijua kusudi lake (Marko 1:38). Tishio kubwa kwa nafsi zetu katika kufanya urafiki na wasio Wakristo ni kwamba tunaweza kupoteza kwa urahisi lengo letu. Ulimwengu haushiriki maadili yetu ya kibilbia na una shauku ya kutuvuta kutoka katika kujitolea kwa Kristo. Ingawa tunaweza kufurahia urafiki na wasio Wakristo, ni lazima tufanya hivyo kwa kufahamu kwamba sisi ni raia wa ufalme mwingine. Tuko hapa kama mabalozi wa Mfalme (Waefeso 2:19; Wafilipi 3:20; 2 Wakorintho 5:20). Tunaweza kushiriki katika shughuli na mahusiano na wasioamini, lakini kwa uhakika tu. Ni lazima tuwe tayari kusema kwa heshima, “La, asante,” tunapoombwa tutoke nje ya kusudi letu. Huenda isiwe dhambi ya moja kwa moja tunayohimizwa kufuata, lakini mambo mengine mengi yanaweza kutuvuta kutoka kwenye ibada safi kwa Kristo (2 Wakorintho 11:13). Kupenda mali, tathimini za kilimwengu, maadili ya muda, tafrija, burudani: yote yanaweza kutishia au kuangusha kusudi la Mkristo. Tunapoweka macho yetu kwenye tuzo—kama Yesu alivyofanya—mahusiano yetu na wasio Wakristo yanaweza kufurahisha na kuzaa matunda kwao na sisi (Waebrania 12:1-2).

5. Yesu alichagua wendani wake wa karibu zaidi. Licha ya ukweli kwamba Yesu alitangamana kila mara na wasioamini, Alihifadhi uhusiano Wake wa karibu zaidi na wanfunzi Wake waliowachagua kwa mkono. Hata miongoni mwa wanafunzi, Alichafua watatu—Petro, Yakbo, na Yohana—kushiriki nyakati za faragha zaidi maishani Mwake. Ni wale watatu pekee walioshuhudia kugeuka kwake suar (Mathayo 17:1-9). Ilikuwa ni wale watatu walioandamana Naye hadi kwenye Bustani ya Gethsemane usiku wa kukamatwa Kwake (Marko 14:33-34). Mfano ambao Yesu alitupa ni ule wa urafiki wa kuchagua katika mahusiano. Ingawa tunapaswa kuwa wenye fadhili kwa kila mtu, tukitumikia kwa njia yoyote tuwezayo, tunapaswa kuwa waangalifu kuhusu wale tanaowaruhusu wawe karibu nasi. Marafiki wetu wa karibu hubeba ushawishi mkubwa na wanaweza kuelekeza mioyo yetu mbali na mpangao wa Mungu kwa maisha yetu.

Ikiwa Yesu alipaswa kuwa mwangalifu kuhusu wale aliowaruhusu kumkaribia, lazima tuwe waangalifu pia. Tunahitaji kutafuta wale wanoshiriki imani yetu na upendo wetu kwa Bwana, tukikumbuka kwamba “sisi ni hekalu la Mungu aliye hai” (ona 2 Wakorintho 6:14-16). Tunaweza kuwapenda na kuwatumikia marafiki zetu wasio Wakristo kama njia ya kumheshimu Mungu na kuonyesha jinsi Mungu pia anawapenda.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mkristo anapaswa kuhusianaje na marafiki wasio Wakristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries