settings icon
share icon
Swali

Ni nini maana ya maridhiano ya Kikristo? Kwa nini tunahitaji kupatanishwa na Mungu?

Jibu


Fikiria marafiki wawili ambao wana vita au majibizano. Uhusiano wao mzuri mara moja waliufurahia umeharibika kiwango cha kuachana. Wanakatisha mawasiliano kati yao wenyewe mawasiliano yanaonekana kuwa yasiyo ya maana kwao. Marafiki hatua kwa hatua kuwa wageni. Utengano huo unaweza tu kurudishwa kwa maridhiano. Kupatanishwa ni kurejeshwa tena kwa urafiki au maelewano. Wakati marafiki wa zamani husuluhisha tofauti zao na kurejesha uhusiano wao, maridhiano yametokea. Wakorintho wa pili 5:18-19 inasema, "Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao, naye ametia ndani yatu neon la upatanisho."

Biblia inasema kwamba Kristo alitupatanisha sisi na Mungu (Warumi 5:10; 2 Wakorintho 5:18, Wakolosai 1:20-21). Ukweli kwamba sisi tulihitaji maridhiano kwa maana uhusiano wetu na Mungu ulikwisha vunjika. Jinsi Mungu ni mtakatifu, sisi ndio wa kulaumiwa. Dhambi zetu zimetutenga kutoka kwake. Warumi 5:10 inasema kwamba sisi tulikuwa maadui wa Mungu: "Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui wa Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tuataokolewa katika uzima wake!"

Wakati Kristo alikufa juu ya msalaba, Alikamilisha hukumu ya Mungu na alifanya hivyo ili iwezekane kwa maadui wa Mungu, ili sisi, tuwe na amani naye. "Maridhiano" yetu na Mungu, basi, yanahusisha zoezi la neema yake na msamaha wa dhambi zetu. Matokeo ya kafara ya Yesu ni kwamba uhusiano wetu umebadilika kutoka uadui hadi urafiki. "Siwaiti ninyi watumishi ... Badala yake, mimi nimewaita marafiki" (Yohana 15:15). Maridhiano ya Kikristo ni ukweli mtukufu! Tulikuwa adui wa Mungu, lakini sasa ni marafiki zake. Sisi tulikuwa katika hali ya hukumu kwa sababu ya dhambi zetu, lakini sisi sasa tumesamehewa. Tulikuwa vita na Mungu, lakini sasa tuna amani ipitayo fahamu zote (Wafilipi 4:7).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini maana ya maridhiano ya Kikristo? Kwa nini tunahitaji kupatanishwa na Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries