settings icon
share icon
Swali

Je, maserafi ni? Maserafi ni malaika?

Jibu


Maserafi (moto, moto unaochoma) ni viumbe malaika vinavyohusishwa na maono ya nabii Isaya juu ya Mungu wake katika hekalu wakati Mungu alimwita kwa huduma yake ya unabii (Isaya 6:1-7). Isaya 6:2-4 imerekodi, " Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa maawili aliruka. Wakati, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, na BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake. Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi." Maserafi ni malaika wanaomwabudu Mungu daima.

Isaya sura ya 6 ni sehemu pekee katika Biblia hasa inataja maserafi. Kila Serafi alikuwa na mabawa sita. Walitumia mawili kuruka, mawili kufunika miguu yao, na mawili kwa kufunika nyuso zao (Isaya 6:2). Maserafi akaruka juu ya kiti cha enzi ambacho Mungu alikuwa amekaa, kuimba sifa zake na kuutia utukufu wa Mungu na ukuu wake. Viumbe hawa inaonekana pia waliwahi kuwa mawakala wa utakaso kwa ajili ya Isaya wakati yeye alianza huduma yake ya kinabii. Mmoja aliweka makaa ya mawe ya moto juu ya mdomo wa Isaya kwa maneno, "Tazama hili imekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa" (Isaya 6:7). Sawa na aina nyingine ya malaika watakatifu, maserafi ni waatiifu kikamilifu kwa Mungu. Sawa na makerubi, maserafi hasa walijushugulisha katika kumwabudu Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, maserafi ni? Maserafi ni malaika?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries