Swali
Je! Agano la Kale linatabiri ujio wa Kristo mara ya pili?
Jibu
Agano la Kale linatabiri kukuja kwa Kristo mara ya pili, ambao pia unaitwa ujio wa pili wa Masiha. Baadhi ya nabii za Agano la Kale uhusu kuja kwa kwanza, wakati Kristo alizaliwa kama mwanadamu. Zingine zinazohusu ujio wa pili, ambao ndio ushindi wa mwisho wa Masiha. Ni muhimu kukumbuka kwamba unabii hauelezei juu ya wakati ujao njia ya kina kama vile historia inavyoelezea yaliyopita. Basi huku nabii za Agano la Kale kwa hivyo zinaelezea ujio wa kwanza na ujio wa pili, tafsiri nyingi za awali za unabii huu ziliziunganisha zote mbili na kuwa tukio moja. Hasa wakati wa miaka iliyoelekea kuzaliwa kwa Ysu, ilidhaniwa kuwa Masiha atakuwa kiongozi wa kisiasa/mfalme wa kijeshi ambaye atakuja na ufalme wa kidunia (Luka 19:11). Kwa mjibu wa huduma ya Yesu, kuna uwezekano kuelewa longo kamili la Kristo na hali kamili ya ufalme Wake.
Kuangalia nabii za Agano la Kale kwa makini kwaonyesha dhana msingi ya dhanio la ujio wa kwanza na wa pili. Mika 5:2 na Isaya 7:14 zinatabiri ujio wa kwanza. Kwa upande wake Isaya 53:8-9 inatabiri Masiha atakaye teseka na kufa, huku akiuawa baada yake kuonekana. Wakati huo huo manabii kama vile Zakaria (Zakaria 12:10) yasungumzia Masiha yule yule “aliyedungwa mkuki” maadui wake watamwona tena. Kwa hiyo dokezo ziko hapa.
Nabii nyingi za Agano la Kale zinatabiri ushindi wa mwisho wa Kristo, ambao utatokea katika ujio wake wa pili. Hii inajumhisha semi kutoka kwa vitabu vya Zekaria (Zekaria 9:14-15; 12:10-14; 13:1 9:14-15) Amosi (Amosi 9:11-15); Yeremia (Yeremia 30:18; 32:44; 33:11,26); na Yoeli (Yoeli 3:1); ambazo zinaelezea ujio wa ushindi wa Masiha kuongoza Israeli katika wokovu. Kumbuka kwamba hili pia katika muktadha wa maandiko kama vile Kumbukumbu la Torari 30:3-5 na hivyo ndivyo ulivyo utabiri wa ushindi wa mwisho wa Masiha.
Vile vile, maandiko yamemnakili Yesu akifanya ulinganisho wa moja kwa moja na nabii za Agano la Kale wakati yeye mwenye anakauli ujio wa pili. Kwa mfano, neno Lake katika Mathayo 24:31 na Marko 13:27 hufanana na maelezo ya Isaya 52:15 na Isaya 59-62.
Katika yote, Biblia ya Kiebrania inaonyesha kwamba mwana wa ahadi ataonekana, ataondolewa na baadaye kutokea kwa ushindi. Ujio wa kwanza ushatokea; ujio wa pili bado uu katika siku za usoni. Agano zote Jipya na Kale zinatabiri ujio wa pili wa Masiha.
English
Je! Agano la Kale linatabiri ujio wa Kristo mara ya pili?