Swali
Matunda ya Roho Mtakatifu ni gani?
Jibu
Wagalatia 5:22-23Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi juu ya mambo hayo hakuna sharia.” Matunda ya Roho Mtakatifu ni matokeo ya kuwepo kwa Roho Mtakatifu katika maisha ya Mkristo. Biblia inaeleza wazi kwamba kila mtu hupokea Roho Mtakatifu wakati yeye anaamini katika Yesu Kristo (Warumi 8:9, 1 Wakorintho 12:13; Waefeso 1:13-14). Moja ya madhumuni ya msingi ya Roho Mtakatifu huja katika maisha ya Mkristo ni mabadiliko ya maisha. Ni kazi ya Roho Mtakatifu kuambatana na mfano wa Kristo, na kutufanya sisi zaidi kama yeye.
Matunda ya Roho Mtakatifu ni tofauti moja kwa moja na matendo ya mwili katika Wagalatia 5:19-21, "Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndivyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.” Kifungu hiki kinaelezea watu wote, kwa viwango tofauti, wakati hawajui Kristo na kwa hiyo hawako chini ya ushawishi wa Roho Mtakatifu. Mwili wetu wa dhambi unazalisha aina fulani ya matunda yanayoonyesha asili yetu, na Roho Mtakatifu anazalisha aina ya matunda yanayoonyesha asili yake.
Maisha ya Kikristo ni vita vya mwili ulio wa dhambi dhidi ya asili mpya iliotolewa na Kristo (2 Wakorintho 5:17). Kama binadamu viumbe tulioanguka, sisi bado tumenazwa katika mwili wa dhambi na kwamba tunathami mambo ya dhambi (Warumi 7:14-25). Kama Wakristo, tuna Roho Mtakatifu kuzalisha matunda yake ndani yetu na nguvu za Roho Mtakatifu zinapatikana kwa kushinda matendo ya mwili (2 Wakorintho 5:17; Wafilipi 4:13). Mkristo kamwe hawezi kuwa mshindi kabisa katika siku zote kuonyesha matunda ya Roho Mtakatifu. Ni moja ya sababu za maisha ya kikristo, ingawa, kwa kuendelea kuruhusu Roho Mtakatifu kuzalisha zaidi na zaidi ya matunda yake katika maisha yetu- na kumruhusu Roho Mtakatifu kushinda tamaa mbaya zinazopinga. Tunda la Roho ni kile ambacho Mungu anatamani maisha yetu yaonyeshe, na kwa msaada wa Roho Mtakatifu, inawezekana!
English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili
Matunda ya Roho Mtakatifu ni gani?