Swali
Je, Mkristo anafaa kucheza michezo ya video?
Jibu
Karibu miaka 2000 kamilifu iliyopita, Neno la Mungu halifunzi wazi iwapo au la Mkristo anafaa kucheza michezo ya video. Lakini kanuni za Biblia bado utumika siku hizi kulingana na utumizi mzuri wa wakati wetu. Wakati Mungu anatuonyesha kuwa tendo fulani linadhibiti maisha yetu,tunafaa kutengana nalo bila kusitisha. Huu "mfungo" unaweza kuwa wa kutokana na vyakula, filamu, runinga, muziki, michezo ya video, chochote kivutiacho imani yetu ya kumjua na kumpenda Mungu na kuwahudumia watu wake. Bali baadhi ya vitu hivi vyaweza kuwa sio vibaya kwa vyao vyenyewe, vinakuwa visanamu iwapo vitatuvutia kutoka kwa upendo wetu wa mwanzo (Wakolosai 3: 5; Ufunuo 2: 4). Zifuatazo ni baadhi ya kanuni za kuzingatia, iwapo swali ni kuhusu michezo ya video,televisheni,filamu, au ukimbizaji wowote wa ulimwenguni.
1. Je michezo ya video yaweza kunijenga ama tu itaniburudisha mimi? Kujenga kuna maana ya kukuza . Je kucheza michezo ya video kunaweza kuza upendo wako kwa Mungu,ujuzi ju yake, na huduma kwa wengine? "'Kila kitu kinaruhusika'-lakini si kila kitu kina manufaa. 'Kila kitu kinaruhusika'-lakini si kila kitu kimetungika "(1 Wakorintho 10: 23-24; Warumi 14:19). Wakati Mungu ametupa wakati wa kupumzika , tunapaswa kupata vitendo vya kutuinua tufurahie.Je tunachagua vitendo vinavyoruhusika zaidi ya vinavyosifika?Tuwapo na uamuzi kati bora,nzuri na nzuri zaidi ,tunafaa kuchagua nzuri zaidi(Wagalatia 5: 13-17).
2. Je kucheza michezo ya video kutatii matakwa ya kibinafsi au mapenzi ya Mungu? Mapenzi ya Mungu kwa watoto wake yanaweza kujumulishwa kwa amri yake kuu: "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa nguvu zako zote na kwa akili yako yote ; na, mpende jirani yako kama nafsi yako '"(Luka 10:27). Mapenzi yetu yamechafuliwa na dhambi. Kwa sababu tumeokolewa kutoka kwa matakwa yetu ya kiuchoyo,tunafaa kusalimisha mapenzi yetu (Wafilipi 3: 7-9).Mapenzi ya Mungu yanageuza mapenzi yetu (Zaburi 143: 10). Hatua kwa hatua, matakwa yake kwetu yanakuwa matakwa yetu ya ndani vile vile.
Watu wengi wanaamini mapenzi ya Mungu yanachosha na kuaibisha. Wao wanamtazama mtawa wa kiume aliye pee kwenye nyumba kubwa ya utawa au bawabu wa kanisa mwenye chuki .Kwa upande mwingine, watu ambao hufuata mapenzi ya Mungu kwa maisha yao ndio wenye furaha zaidi,watu wenye kuthubutu daima.Kusoma wasifu wa historia ya mashujaa kama Hudson Taylor, Amy Carmichael, Corrie Ten Boom, na George Mueller kutathibitisha hilo. Hakika, watumwa hawa walikumbwa na ugumu kutoka kwa ulimwengu,nyama za mwili wao wenyewe,na ibilisi. Wanaweza kuwa hawakumiliki uridhi mwingi wa duniani,lakini Mungu alikamilisha kazi nyingi kupitia kwao. kwanza, mapenzi yake yanaonekana yasiyowezekana na matakatifu zaidi kuwa kama mchezo wowote,lakini Mungu atatupa uwezo wa kuyafanya na matakwa ya kupendeza ndani yake. "Kuyafanya mapenzi yako ,Ee Mungu wangu,ndiyo furaha yangu;Naam,sharia yako imo moyoni mwangu" (Zaburi 40: 8a; angalia Waebrania 13:21).
3. Je mchezo wa video unamtukuza Mungu? Baadhi ya michezo ya video hutukuza vurugu,ufisadi,na maamuzi ya kibubu (kwa mfano, "mimi siko kwa shindano ,sasa nitavunja gari langu"). Kama Wakristo, vitendo vyetu vinafaa kuleta utukufu kwa Mungu (1 Wakorintho 10:31) na vitusaidie kukua kwa maarifa na neema ya Kristo.
4. Je kucheza michezo ya video itatoa kazi nzuri? "Kwa maana sisi ni kazi yake, tulioumbwa ndani ya Kristo Yesu kwa kazi nzuri,ambazo Mungu alitayarisha kwa mikono yake,ili tuwe tukitembea ndani yazo" (Waefeso 2:10, tazama pia Tito 2: 11-14 na 1 Petro 2:15). Uvivu na ubinafsi ukiuka kusudi la Mungu kwetu-la kufanya kazi njema kwa wengine (1 Wakorintho 15:58, tazama pia Wagalatia 6: 9-10).
5. Je kucheza michezo ya video kutaonyesha kujidhibiti nafsi ? Watu wengi wamesema kwamba michezo ya video inaweza kuwa mazoea amaisababishe kushikwa na mawazo. Hakuna nafasi katika maisha ya Kikristo kwa vitu kama hizo. Paulo analinganisha maisha ya kikristo na yale ya mkimbiaji anayefanyisha mwili wake mazoezi ili aweze kushinda tuzo. Wakristo wana motisha kubwa kuishi maisha ya kuweka-akiba ya kujizuia_ malipo ya milele mbinguni (1 Wakorintho 9: 25-27).
6. Je kucheza michezo ya video kunaweza komboa wakati? Utaeleza jinzi unavyotumia dakika zako zilizo na kikomo. Kutumia masaa mengi kwa wakati mmoja kucheza mchezo wa video ni vigumu kuitwa utumizi bora wa wakati. "Kuwa mwangalifu sana,alafu, jinsi unavyoishi - sio kama mjinga bali kama mwerefu,ukifanya zaidi ya kila nafasi ya kipekee,kwa sababu siku hizi ni mbaya. Kwa hivyo,usiwe mpumbavu, bali uelewe mapenzi ya Mungu ni nini " (Waefeso 5: 15-17). "kwa wakati uliosalia usiishi kutimiza mahitaji ya kimwili bali kwa mapenzi ya Mungu" (1 Petro 4: 2, tazama pia Wakolosai 4: 5, yakobo 4:14, na 1 Petro 1: 14-22 ).
7. Je,inahitimu jaribio la Wafilipi 4: 8? “Hatimaye ndugu zangu, yo yote yaliyo ya kweli, ya yote yaliyo ya staha, yo yote yaliiyo ya haki, ya yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo" (Wafilipi 4: 8). Wakati wewe unacheza michezo ya video, akili yako inaangazia mambo ya kiungu au ya kidunia?
8. Je! kucheza michezo ya video kunaingiana kusudi la maisha yangu? Paulo aliandika kwamba katika siku za mwisho watu watakuwa "... wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu" (2 Timotheo 3: 4). Utamaduni wa Magharibi unafaa maelezo hayo. Sisi tuna upendo kwa kucheza. Wasio Wakristo hutawaliwa na burudani kama vile sinema, michezo, na muziki kwa sababu hawana madhumuni ya juu kuliko kufurahia maisha kabla ya kifo. Burudani hizi haziwezi kweli kukidhi (Mhubiri 2: 1). Wakati wakristo hutawaliwa na mambo sawa na wasio Wakristo, tunaweza kweli kusema kwamba tunaonyesha maisha mapya "Mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwngu" (Wafilipi 2:15)? Au je, tunathibitisha kwa wengine kwamba sisi kweli ni wa tofauti kuliko wao na kwamba Kristo hajaifanya tofauti kubwa katika maisha yetu?
Paul alichukulia kujua, upendo, na kutii Mungu kuwa kipaumbele kuu chake. "Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu, mbaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo; tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake" (Wafilipi 3: 7-10) . Je, kucheza michezo ya video kutaonyesha upendo wangu kwa Mungu au upendo wangu kwa mambo ya dunia? (1 Yohana 2: 15-17).
9. Je, kucheza michezo ya video kutanipa mtazamo wa maisha ya milele? Wakristo wana matumaini ya tuzo la maisha ya milele mbinguni kama wao ni waaminifu duniani (ona Mathayo 6: 19-21 na 1 Wakorintho 3: 11-16). Kama sisi huzingatia kuishi kwa ajili ya milele badala ya raha zinazopita za dunia, tutakuwa tumesalimisha rasilimali, muda, na mioyo kwa ajili ya huduma (Wakolosai 3: 1-2; 23-24). Kama mali yetu au shughuli huwa sababu yetu kupoteza tuzo zetu za milele, zina thamani gani zinao (Luka 12: 33-37)? Wakristo mara nyingi hujaribu kumtumikia Mungu na tamaa zao wenyewe. Lakini ni wazi Yesu alisema, "Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili" (Mathayo 6:24). Mungu anatupa furaha wakati wa kazi na starehe (Mhubiri 5:19, Mathayo 11: 28-29, Wakolosai 3: 23-24). Ni lazima tutafute uwiano kati ya kazi na burudani. Wakati hatuwezi kutenga muda kwa ajili ya mapumziko kama Yesu alivyofanya (Marko 6:31), tunapaswa kuchagua shughuli za kujijenga imani.
Swali si "Naweza kucheza michezo ya video?" Lakini ni "Je, michezo ya video ni chaguo bora?" Je, hili litanijenga, lionyeshe upendo kwa jirani yangu, na kumtukuza Mungu? Tunapaswa kuendea mambo ya sifa, sio yale tu yameruhusiwa. Hata hivyo Yeye atakuongoza, kwa dhati kumfuata zaidi ya yote. Kujiandaa kwa ajili ya milele. Kila sadaka itaonekana bila kuwa na maana wakati sisi hukutana na Yesu.
English
Je, Mkristo anafaa kucheza michezo ya video?