Swali
Je! Mingurumo saba katika kitabu cha Ufunuo 10:1-7 ina maana?
Jibu
Mingurumo saba inaonekana katika Ufunuo 10:1-7. Katika maono yake tabiri, mtume Yohana aliona malaika mwenye nguvu akitembea juu ya bahari na nchi kavu akiwa na hati ndefu mkono mwake. Yule malaika alitoa mngurumo kama ule wa simba, na hapo sauti za mingurumo saba ikaongea. Yohana alipokuwa tayari kuandika, sauti toka mbinguni ikamwambia “Yatie muhuri hayo yaliyosemwa na hizo radi saba na usiyaandike” (Ufunuo 10:4).
Tukio la zile sauti saba za mingurumo hutokea tena katika baragumu za sita na baragumu za saba. Mingurumo saba sio kelele za kawaida ya mngurumo wa radi, bali ni mngurumo kama ule wa sauti ukiwasilisha ujumbe. Neno la Kigiriki lililotafsiriwa “mgnurumo” limaanisha “kurindima.” Mngurumo mara nying huwa ni ishara ya hukumu katika Maandiko kama vile ilivyo katika 1 Samueli 2:10; 2 Samueli 22:14, na sehemu zingine nyingi katika Ufunuo (Ufunuo 8:5; 11:19; 16:18), kwa hivyo hizi sauti saba za nguvu zinalia kwa ajili ya hukumu ya Mungu juu ya dunia yenye dhambi. Mngurumo unawakilisha sauti ya Mungu. Zaburi 18:13 inasema, “Bwana alinguruma kutoka mbinguni,
sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.”
Ushahidi zaidi wa mingurumo saba kuwa sauti ya Mungu upo katika Ufunuo 4:5: “Kwenye kile kiti cha enzi palikuwa panatoka miali ya umeme wa radi, ngurumo na sauti za radi. Mbele ya kiti cha enzi, taa saba zilikuwa zinawaka. Hizi ndizo roho saba za Mungu.” Tena sauti ya Mungu inaelezewa kuwa kama mngurumo wa mirindimo ambao unaonyesha mamlaka, ukuu wa enzi na utukufu wa Bwana wetu mwenye enzi. Katika aya hii, Yohana aliona utangulizi ghadhabu ya Mungu itakayo miminwa kwa dunia vile imeelezewa katika Ufunuo milango ya 16-19.
Yohana alipokuwa karibu kuyaandika maneno ya mingurumo saba, sauti kutoka mbingu inamwamurisha atie muhuri yale alifunuliwa. Kiti kile kile cha enzi kilichotoa miale ya moto na mingurumo kinatoa amri ya kuiweka siri chenye sauti imefunua. Sababu ya kutiwa muhuri haijatolewa, lakini inaweza kuwa kwamba hukumu ilikuwa ya kutisha kunakiliwa. Maudhui ya ujumbe kamwe hayajafunuliwa katika Maandiko, kwa hivyo hatuwezi kisia katika hilo. Mingurumo saba ndio maneno pekee katika Ufunuo yametiwa muhuri.
English
Je! Mingurumo saba katika kitabu cha Ufunuo 10:1-7 ina maana?