settings icon
share icon
Swali

Je, inamaanisha nini kuomba mkate wetu wa kila siku?

Jibu


Sala ya Bwana, ni sala ambayo Yesu alitumia kuwaelekeza wafuasi wake jinsi ya kuomba, inajulikana sana miongoni mwa Wakristo. Wengi huisoma kwa umoja kama namna ya kawaida ya ibada na sala ya dini (liturujia); wengine hutafakari kila sehemu katika wakati wao wa faragha na Mungu au wanaiona kuwa ni kielelezo cha sehemu za sala. Sala hiyo imeandikwa katika Mathayo 6:9-13 na Luka 11:2-4. Sehemu moja ya maombi inasema, “Utupe loe mkate wetu wa kila siku” (Mathayo 6:11).

Maana ya kwanza na dhahiri ya ombi hili ni kwamba Mungu atatutegemeza kimwili. Pengine Yesu alikuwa anarejelea utoaji wa Mungu wa mana, ambayo ilitolewa kila siku jangwani (kutoka 16:4-12; Kumbukumbu la Torati 8:3; Yohana 6:31). Tunamtambua Mungu kama mtoaji wetu na kumtegemea Yeye kukidhi mahitaji yetu ya kila siku. Hii haimaanishi kuwa tunamtarajia Mungu atupe mana kihalisi bali kwamba tunaelewa kwamba Yeye ndiye anayefanya kazi yetu iwe na matudna, na nyakati nyingine hata kutimiza mahitaji ya kimwili kwa njia za kimuujiza. Muda mfupi baada ya kuwalekeza wafuasi Wake jinsi ya kusali, Yesu alizungumza nao kuhusu mahangaiko. Alisema, “Kwa hiyo nawaambia, msisumbukie maisha yenu kwamba mtakula nini au mtakunywa nini; au msumbukie miili yenu kwamba mtavaa nini. Je, maisha si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?... Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia” (Mathayo 6:25,33). Cha kupendeza, katika Sala ya Bwana, ombi linalotangulia ombi la mkate wa kila siku ni kwamba ufalme wa Mungu uje.

Kuomba mkate wa kila siku sio tu kuhusu utoaji wa kimwili. Inaweza pia kurejelea kumwomba Mungu atuandalie mahitaji yetu yasiyogusika. Katika Mathayo 7:7-11 Yesu alisema, “Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango. “Au ni nani miongoni mwenu ambaye mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe? Au mwanawe akimwomba samaki atampa nyoka? Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?” Wazazi wazuri hutoa sio tu kile watoto wanachohitaji katika haya maisha, bali pia kwa mahitaji ya vitendo, ya kihisia, naya uhusiano. Mungu ni mtoaji wa zawadi nzuri (Yakobo 1:17). “Ikiwa Mungu hakumhurumia Mwanawe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote, atakosaje basi kutupatia vitu vyote kwa ukarimu pamoja naye?” (Warumi 8:32).

Mungu tayari amekidhi hitaji letu kuu la kiroho, lile la msamaha na urejesho, kupitia Kristo (Wakolosai 2:13; 2 Wakorintho 5:17, 21; Yohana 20:31). Lakini haishii hapo. Yesu anajiita “Mkate wa uzima” (Yohana 6:35). “Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu” (Yohana 1:4). Yesu anasema alikuja kutuletea uzima tele (Yohana 10:10). Sio tu kwamba tunaokolewa kwa uzima wa milele, lakini pia tunapitia uhusiano uliorejeshwa na Mungu sasa. Tunamtafuta kila siku, naye hutufanya upya siku baada ya siku (Wakorintho 4:16). Daima tawi linaendelea na kulishwa na Mzabibu (Yohana 15:5).

Naam, Mungu hukidhi mahitaji yetu ya kimwili, na yale mahitaji yasiyogusika katika maisha haya. Zaidi ya hayo, Yeye hutimiza mahitaji yetu ya kiroho. Yeye ndiye mkate unaotosheleza njaa yetu ya kiroho. Yeye hudumisha mioyo yetu. Wakati tunamuuliza Mungu mkate wetu wa kila siku, kwa unyenyekevu tunatambua yeye kama mtoaji wa yote tunayohitaji. Tunaishi siku baada ya siku, hatua moja baada ya nyingine. Tunatumia imani rahisi Kwake ili kutoa kile tunachohitaji wakati tunapohitaji-kwa kila hali la maisha.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, inamaanisha nini kuomba mkate wetu wa kila siku?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries