settings icon
share icon
Swali

Nitajuaje wakati nimempata mke kamilifu kwa ajili yangu?

Jibu


Biblia haisungumzii ya kupata "mke mwema," wala kutupa sifa maalum jinsi tunavyo taka katika la suala la kutafuta mpenzi mwema katika ndoa. Jambo moja neno la Mungu linatuambia wazi ni kuwa tuhakikishe kwamba tusioe kafiri (2 Wakorintho 6:14-15). Wakorintho wa Kwanza 7:39 inatukumbusha kwamba, huku tukiwa huru kuoa, tunapaswa kuoa wale ambao wamekubalika kwa Mungu kwa njia nyingine, Wakristo pekee. Zaidi ya hapo, Biblia ii kimya kuhusu kile tunapaswa kujua wakati wa kuoa mtu "mwema".

Sasa kwa nini Mungu asituambie chenye tunafaa kuangalia kwa mchumba tunayemtaka? Kwa nini hatuna vihitimisho maluum kuhusu suala hilo muhimu? Ukweli ni kwamba Biblia ii wazi juu ya Mkristo ni jinsi tunastahili kuhiga sifa muhimu. Wakristo wanatakiwa kuwa na msimamo kuhusu masuala muhimu, na kama Wakristo wawili wameingia katika ndoa na kumtii Kristo, tayari wanamiliki viungo muhimu kwa mafanikio. Hata hivyo, kwa sababu jamii yetu huathiriwa na wengi wanaokiri kuwa Wakristo, itakuwa busara kutumia utambuzi kabla ya kujitoa wenyewe kwa dhamira ya ndoa ya maisha. Mara baada ya vipaumbele wanaotazamiwa kwa mchumba vimetambuliwa-kama yeye kweli ana bidii kwa kuwa kama Kristo-kisha vihitimisho kuu ni rahisi kuvibaini na kushughulikia.

Kwanza, tunapaswa kuhakikisha kwamba tuko tayari kuoa. Lazima tuwe na ukomavu wa kutosha kuangalia zaidi ya hapa na sasa na kuwa na uwezo wa kujitoa kwa mtu huyum moja kwa ajili ya mapumziko ya maisha yetu. Ni lazima pia kutambua kwamba ndoa inahitaji sadaka na kutokuwa na ubinafsi. Kabla ya kuoa wanandoa wanapaswa kujifunza majukumu na wajibu wa mume na mke (Waefeso 5:22-31, 1 Wakorintho 7:1-16, Wakolosai 3:18-19, Tito 2:1-5; 1 Petro 3: 1-7).

Wanandoa wanapaswa kuhakikisha kuwa wanajuana kila mmoja kwa kiasi cha muda wa kutosha kabla ya kujadili ndoa. Wanapaswa kuangalia jinsi mwingine hutoa hisia zake katika hali tofauti, tabia yake akiwa karibu na familia yake na marafiki, na ni watu wa aina gani hushinda nao. Tabia ya mtu hushawishiwa sana na wale anaendelea kushiriki nao (1 Wakorintho 15:33). Wanapaswa kukubaliana juu ya masuala kama vile maadili, fedha, kanuni, watoto, mahudhurio ya ushiriki kanisani, mahusiano na katika sheria, na ajira. Haya ni maeneo ya migogoro katika ndoa na lazima yaangaliwe kwa uangalifu kabla ya ndoa.

Hatimaye, mwanandoa yeyote anayezingatia ndoa lazima kwanza aende mchungaji kwa ushauri kabla ya ndoa yao au Mkristo mwingine aliyehitimu mafunzo ya ushauri. Wao hapa hujifunza zana thamani ya kujenga ndoa yao juu ya msingi wa imani katika Kristo, na wao pia hujifunza jinsi ya kukabiliana na migogoro isiyoepukika. Baada ya vigezo hivi vyote vimetimizwa, wanandoa wako tayari kwa maombi kuamua kama wanataka kuunganishwa pamoja katika ndoa. Kama kwa hakika tunatafuta kwa bidii mapenzi ya Mungu, Yeye ataongoza njia zetu (Mithali 3:5-6).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nitajuaje wakati nimempata mke kamilifu kwa ajili yangu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries