settings icon
share icon
Swali

Je, ni makossa kwa Mkristo kusongwa na mawazo?

Jibu


Unyogovu ni suala kinzano miongoni mwa Wakristo. Wengine wanatangaza waziwazi kuwa ni dhambi. Wazo ni kwamba unyogovu hudhihirisha ukosefu wa imani katika ahadi za Mungu, hukumu ya Mungu juu ya tabia ya dhambi, au uvivu tu. Tunajua kwamba Mungu ni mwema na mwenye upendo na kwamba tuko salama ndani Yake, kwa hivyo ni nini cha kutuhuzunisha? Wengine hutangaza wazi kuwa unyogovu ni suala la kimatibabu. Wazo ni kuwa unyongovu wote ni matokeo ya kemikali katika ubongo kutolingana, kwa hiyo unyongovu sio mbaya zaidi kuliko kuwa na mafua. Na kisha kuna wale walio katikati ambao hawana hakika kabisa mfadhaiko ni nini. Imani inaonokena kuhusiana kwa kiwango fulani, lakini vile vile kemikali za ubongo pia. Bila shaka pia kunao Wakristo walio na unyongovu, walioachwa kuhisi hatia, kujitetea, kuchanganyikiwa, kupotea au kufadhaishwa sana kiwango kwamba hawajali kile kanisa inafikiria kuwahusu. Kwa hivyo, ni makosa kwa Mkristo kufadhaika?

Neno unyogovu ni legelege. Linaweza kuwa linataja hali ya kiafya inayoweza kutambulika (fadhaiko la kiafya), lakini pia linaweza kuwa linataja hisia ya muda ya huzuni au kutojali au hali mbaya, uchovu unaodumu. Nakala hii itajaribu kuzingatia kwa ufupi maana kadhaa ya unyogovu.

Kwa watu wengine kutolingana kwa kemikali au homoni husababisha hali ya kufedheheka. Hii ni kawaida kwa wanawake wanaougua unyogovu baada ya kujifungua au watu wanaotumia dawa fulani. Nyakati zingine, unyogovu unatokana na hali fulani, unasababishwa na hali mbaya, mabadiliko ya maisha, mgogoro wa kiroho, nk. Mwitikio wetu wa kihisia kwa matatizo hayo unaweza kusababisha kutolingana kwa kemikali. Kwa kweli, wanadamu “wameumbwa kwa namna ya ajabu na ya kutisha” (Zaburi 139:14), na haipaswi kuwa mshangao kwamba maumbile yetu ya kibaolojia yanaadhiriana na hisia na kinyume chake vile vile. Pindi mtu anapofedheheka, mzunguko wa kemikali kutolingana na hisia inaweza kuwa ngumu kuimaliza. Iwe kwamba hisia husababisha baolojia kubadilika au baolojia husababisha hisia kubadilika, dadili zinazotokea huwa sawia.

Kuwa na hali ya kiafya sio dhambi. Ijapokuwa kinachosabaisha hali hiyo kinaweza kuwa na mzizi yake katika dhambi. Kwa mfano, sio makosa kuwa na kisukari, bali ni makosa kuwa mlafi (na yote mawili mara nyingi yana uhusiano). Pia, jinsi mtu anavyoitikia hali halisi ya kiafya inaweza pia kuwa dhambi. Kwa mfano, itakuwa dhambi kwa mtu aliye na kisukari kutumia ugonjwa wa kisukari kuwadanganya wengine au kuwa na mawazo ya “mhasiriwa” au nia ya kustahiki.

Walakini mara nyingi tunashikilia kuwa wale walio na hali zingine za kimatibabu kuwa wasio na hatia kuliko tunavyofanya watu walio na unyogovu. Kwa sababu fulani, magonjwa hasa ya akili yanahusishwa mara nyingi na visababishi vya dhambi kuliko magonjwa mengine ya kimwili. Unyogovu sio suala ya matibabu tu, na sio suala la kihemko au la kiroho.

Unyogovu mara nyingi huchukuliwa kuwa hisia inayoendelea ya huzuni.Ni sawa kuwa na huzuni. Tunaishi katika ulimwengu wa maumivu (Mwanzo 3:14-19; Warumi 8:20-22), na Yesu alilia kwa kifo cha Lazaro (Yohana 11:35). Hakuna haja ya kuweka uso wa furaha kila wakati na kujifanya kuwa mambo yako shwari wakati yameharibika.

Kunayo mifano mingi ya kibiblia ya watu wa Mungu waliopambana huzuni hadi wakawa na unyogovu. Daudi aliandika, “Andika maombolezo yangu, orodhesha machozi yangu katika gombo lako: je, haya hayapo katika kumbukumbu zako?” (Zaburi 56:8). Daudi, “mtu anayeupendeza moyo wangu” (Matendo 13:22), hakuficha huzini yake; aliileza kwa Mungu. Musa (Hesabu 11:15) na Eliya (1 Wafalme 19:3-5), mashujaa wawili wa imani, walikiri kwa Mungu kwamba walipendelea kufa kuliko kuishi katika maisha yao na yale waliyoyapitia. Hakuna kati yao aliyekemewa na Mungu kwa hisia zake; badala yake, wote wawili walikutana na upendo na utele wa Mungu. Biblia haioni haya kukiri ukweli wa hisia za mwanadamu. Huzuni ni sehemu ya maisha, na haikemewi.

Kama waumini, tunahimizwa kuona uhalisi wa mpango wa Mungu hata katikati mwa huzuni na unyogovu wetu. Naam, ulimwengu huu umeanguka na mara nyingi kuwa mchungu. Inaweza fedhehesha. Lakini Mungu ni mkuu zaidi. Yuko kazini kwa ushindi. Musa na Eliya walipokea utele wa Mungu na kupata kuburudishwa. Muda mfupi baada kueleza huzuni yake, Daudi alimsifu Mungu. Yesu alisema, “Nimewaambia mambo haya, ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu” (Yohana 16:33).

Wakristo wanaruhusiwa kuita shida jinsi ilivyo. Wakati huohuo tunajitia moyo katika utunjazi wa Mungu. Kujitia moyo hakumaanishi kutabasamu au kupuuza hisia ya utupu ambayo fedheha huleta. Haimaanishi kuwa utekeleze kutibu unyogovu kupitia ushauri na matibabu. Haimaanishi kupuuza maumivu yatokanoyo na uhusiano au ung’amuzi potovu ambao umesababisha unyogovu (uongo wa Shetani, ikiwa tunauamini, utatuongoza katika kukata tamaa). Haimaanishi kukataa ukweli kwamba unyogovu unawea kuwa mapambano ya maishani.

Kujitia moyo kunamaanisha kuyaleta maumivu yetu yote kwa Mungu. Inamaanisha kuendelea kumwamini. Inamaanisha kuamini kwamba kile Anachosema juu Yake na kutuhusu ni kweli, hata wakati hatuhisi hivyo. Inamaansiha kupata msaada tunaohitaji, kupambana na unyogovu badala ya kukufa moyo. Tunakubali opotovu wa ulimwengu, lakini tunakubali utoshelevu wa Mungu.

Sio makosa kuwa na unyogovu. Bali ni makosa-na hasa haisaidii katika kushinda hali kufedheheka-kuacha kumtumainia Mungu wakati tumefedheheshwa. “Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa sababu bado nitamsifu Mwokozi wangu na Mungu wangu” (Zaburi 43:5).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni makossa kwa Mkristo kusongwa na mawazo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries