Swali
Je, Mkristo anaweza kulaaniwa? Je, Mungu anaweza kuruhusu laana kwa muumini?
Jibu
Biblia inatuambia kwamba "kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu." (Mithali 26: 2b). Hii ina maana kwamba laana ya kijinga haina mathara. Mungu hawaruhusu watoto wake kulaaniwa. Mungu ni mtawala. Hakuna mtu ana uwezo wa kulaani mtu ambaye Mungu ameamua kubariki. Mungu ndiye wa pekee ana uwezo wa kutoa hukumu.
"Laana" katika Biblia daima ilimeelezwa vibaya. Kumbukumbu 18: 10-11 imeorodhesha wale ambao wanalaani na wale wanaofanya vitendo vingine "chukizo kwa Bwana" kama vile –Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto,wala asionekane mtu atazamaye bao,wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Mika 5:12 inasema kwamba “name nitakatilia mbali uchawi, usiwe mkononi mwako;wala hutakuwa tena na watu wenye kutabana. Ufunuo 18 inaelezea laana kama sehemu ya udanganyifu ambao itatumiwa na maadui wapinzani wa Kristo na "mji wake mkuu wa Babeli" (v. 21-24).Kwa maana watatokea makristo wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. (Mathayo 24:24), Mungu atamwangamiza shetani kabisa kabisa , makristo wa uongo, na wote ambao wanawafuata(Ufunuo sura ya 19-20 ).
Mkristo amezaliwa tena kama mtu mpya katika Yesu Kristo (2 Wakorintho 5:17), na tuko katika uwepo wa mara kwa mara wa Roho Mtakatifu ambaye anaishi ndani yetu na ambaye chini ya ulinzi wake tuko hai (Warumi 8:11). Hatuna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya mtu yeyote anayetoa aina yoyote ya laana ya kikafiri juu yetu. uchawi,ulozi,urogi, na laana hazina mamlaka yoyote juu yetu kwa sababu huja kutoka kwa Shetani, na tunajua kwamba "aliye ndani yenu [Kristo] ni mkuu kuliko yule [Shetani] aliye duniani" (1 Yohana 4: 4). Mungu amemshinda tayari, na tumekuwa huru kumwabudu Mungu bila hofu (John 8:36). "Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu,nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, nimhofu nani? "(Zaburi 27: 1).
English
Je, Mkristo anaweza kulaaniwa? Je, Mungu anaweza kuruhusu laana kwa muumini?