settings icon
share icon
Swali

Je! wanaume au wanawake Wakristo wanapaswa kuvaa vipuli kwa masikio?

Jibu


Kulikuwa na wanaume na wanawake katika Biblia ambao walivaa vipuli (Kutoka 32:2-3; Hesabu 31:50; Waamuzi 8:24; Wimbo 1:10-11). Hakuna mahali Biblia inakemea vipuli katika wanawake au wanaume. Baadhi ya watu hushangaa ni kwa nini vipuli vimekubaliwa mahali kwingi, lakini kutoboa sehemu zingine za mwili kunachukuliwa kuwa jambo la kutiliwa shaka. Hii ni hoja nzuri. Suala zima la kutoboa sio moja ya “Je! biblia inakataa hili?” badala yake, “Je, hili ni jambo ninalopaswa kufanya?”

Ingawa hakuna shauri hususan katika Biblia kuhusu vipuli, Paulo alikuwa na kauli za jumla za kusema kuhusu mapambo ya vito wakati alipomshauri Timotheo kuhusu ibada katika kanisa: “Vivyo hivyo nataka wanawake wajipambe kwa adabu na kwa heshima katika mavazi yanayostahili, si kwa kusuka nywele, kuvalia dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa, bali kwa matendo mazuri kama iwapasavyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu” (1 Timotheo 2:9-10). Kanuni hapa inatumika ndani na nje ya kanisa: adabu, heshima, utaratibu, na matendo mema ndio alama za Mkristo wa kweli katika wanaume na wanawake.

Iwe tumechagua kuvaa vipuli au aina yoyote ya mapambo ya vito ni jambo la dhamiri ya kibinafsi. Kwa hali yoyote, jukumu letu kama Wakristo ni kuleta heshima na utukufu kwa Mungu tunayekiri kumpenda, kwa kufanya lolote bila kujitukuza kwa majivuno (Wafilipi 2:3) na kukumbuka kwamba “Mwanadamu hutazama katika sura ya nje, lakini Bwana hutazama moyoni” (1Samweli 16:7).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! wanaume au wanawake Wakristo wanapaswa kuvaa vipuli kwa masikio?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries