settings icon
share icon
Swali

Mkristo wamwili ni nini?

Jibu


Je, Mkristo wa kweli anaweza kuwa wa kimwili? Katika kujibu swali hili, hebu kwanza tufafanue neno "kimwili." Neno "kimwili" limetafsiriwa kutoka kwa neno la Kigiriki sarkikos , ambalo maana yake halisi ni "mwili." Neno hili la maelezo linaonekana katika mazingira ya Wakristo katika 1 Wakorintho 3:1 -3. Katika fungu hili, mtume Paulo anawatambua wasomaji kama "ndugu," neno analolitumia kikamilifu kurejelea Wakristo wengine; yeye kisha anaendelea kuwaeleza hao kama wa "kimwili." Kwa hiyo, tunaweza kuhitimisha kwamba Wakristo wanaweza kuwa wa kimwili. Biblia ii wazi kabisa kwamba hakuna mtu hana dhambi (1 Yohana 1:8). Kila wakati sisi hutenda dhambi, sisi twakaa kimwili.

Kitu muhimu kuelewa ni kwamba Mkristo anaweza kuwa, kwa wakati mmoja wa kimwili, Mkristo wa kweli hawezi baki kidunia kwa ajili ya maisha. Baadhi ya wengine wemelitumia vibaya wazo la "Mkristo wa kidunia" kwa kusema kwamba inawezekana watu kuja kwa imani katika Kristo na kisha kuendelea kuishi ya maisha yao katika namna ya mwili kabisa, na hakuna ushahidi wa kuzaliwa mara ya pili au kiumbe kipya (2 Wakorintho 5:17). Dhana hiyo ni ya kibiblia kabisa. Yakobo 2 huiweka wazi kwamba imani ya kweli daima huleta matendo mema. Waefeso 2:8-10 inasema kwamba wakati sisi tuliokolewa kwa neema tu kupitia imani peke yake, wokovu huo utasababisha kazi. Mkristo anaweza wakati wa kushindwa na / au uasi, kuonekana kuwa wa kidunia? Naam. Je, Mkristo wa kweli anaweza baki kuwa wa kidunia? La.

Tangu usalama wa milele ni ukweli wa maandiko, hata Mkristo wa kidunia bado ameokolewa. Wokovu hauwezi kupotea, kwa sababu wokovu ni zawadi ya Mungu kwamba Yeye hawezi kuichukua (angalia Yohana 10:28; Warumi 8:37-39, 1 Yohana 5:13). Hata katika 1 Wakorintho 3:15, Mkristo wa kimwili amehakikishiwa wokovu: " Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto." Suala siyo kama mtu ambaye anadai kuwa Mkristo lakini anaishi kwa uasherati amepoteza wokovu wake, lakini ikiwa mtu huyo kwa kweli aliokolewa mara ya kwanza (1 Yohana 2: 19).

Wakristo ambao hugeuka na kuwa wa kidunia katika tabia zao wanaweza kumtarajia Mungu kwa upendo kuwapa nidhamu (Waebrania 12:5-11) ili waweze kurejeshwa kwa karibu na ushirika naye na kufunzwa kumtii. Mapenzi ya Mungu katika kutuokoa sisi ni kwamba kuendelea kukua karibu na mfano wa Kristo (Warumi 12:12), tuzidi kuwa wa kiroho na umwili wetu kupungua, mchakato unaojulikana kama utakaso. Mpaka sisi tukombolewe katika miili yetu ya dhambi, kutakuwa na milipuko ya umwili. Kwa muumini wa kweli katika Kristo, ingawa milipuko huu wa kimwili kamwe utakuwa uchaguzi sio sheria.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mkristo wamwili ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries