settings icon
share icon
Swali

Je! Mungu aliumbwa na mwanadamu?

Jibu


Watu wengine ubishi kuwa Mungu aliumbwa na mwanadamu; hivyo, dhana ya Mungu ni uwongo wa binadamu uliorithiwa na vizazi kutoka kwa wale ambao hawakujua vyema. Wanadai kwamba dhana ya Mungu au miungu ni njia ya mwanadamu ya kuelezea vitu ambavyo ni vigumu kuelewa. Wengine husema kuwa imani katika kile kisicho cha kawaida hupuuza sayansi na kushikilia ushirikina. Kwa hivyo, dhana ya Mungu ni ndoto msingi wake uu katika kukosa maarifa na ulianzishwa na mababu wetu kabla ya sayansi kuudhibitisha kuwa wa uwong?

La, Mungu hakuumbwa na mwanadamu; badala yake, Mungu ndiye aliumba mwanadamu. Hata wasomi hukubali kuwa kuna mwanzo wa kila kitu kilichoumbwa, hii ikiwa ni pamoja na mwanadamu. Kwa hivyo, ndio mwanadamu awe na mwanzo, lazima kuwe na "msababishi" aliyekuwepo kabla yake. Wale wanaoshikilia dhana ya kuota ubishana kuwa chanzo sababishi cha kwanza ilikuwa nguvu fulani, "mlipuko mkubwa," ambao ulianzisha ulimwengu. Lakini hata maelezo yake yanaacha maswali mengi ambayo hayajajibiwa. Jibu rahisi kwa fikira kama hii ni, "Ni nini kilisababisha mlipuko mkubwa? Ni nini au nani aliunganisha hizo nguvu ndio kukawa na kusonga?" hamna jibu lifaalo lilitolewa nje ya Biblia.

Biblia inaanza na kweli ya Mungu katika Mwanzo 1:1, "Hapo mwanzo Mungu…." Tunapo weka kando ubaguzi, jibu la Biblia linaonekana kuwa elezo sahii la sababishi la kwanza. Hapo mwanzo kulikuwa na Mungu. Hakuumbwa na kwa hivyo haitaji sababisho la kwanza. Nyakati zote amekuwa na atakuwa milele, mbali na nyakati na nafasi (Zaburi 90:2). Alijitambulisha mwenyewe kwa Musa kama MIMI NDIYE (Kutoka 3:14). Maana ya jina lake linaashiria asili yake ya milele. Kila wakati amekuwa na atakuweko siku zote, anajisimamia mwenyewe (Ufunuo 1:8; 4:8).

Zingatio la pili kwa mambo ikiwa Mungu aliumbwa na mwanadamu au la ni asili ya Mungu jinsi amejifunua yeye Mwenyewe kupitia kwa kurasa za Biblia. Sifa nyingi za Mungu sio zile ambazo mwanadamu anaweza kufikiria kujumulisha ikiwa yeye ndiye alimuumba. Tabia ya Mungu ni pamoja na mwenye hekima yote (Malaki 3:6), mwenye enzi (2 Samueli 22:3; Zaburi 18:2), mvumilivu (2Petro 3:9) na asiyebadilika (Malaki 3:6). Ameelezewa kuwa mwenye upendo (Zaburi 25:10), mwaminifu (Zaburi 31:23), na ana aja sana ya kuwa na uhusiano nasi (Yeremia 29:13; Yakobo 4:8). Vile vile yeye ni mwenye haki mkamilifu, na kwamba haki inahitaji dhamana kwa niapa ya mwanadamu kwa makosa ya jinai dhidi ya Muumba wake (Sefania 3:5; Warumi 6:23). Badala ya kutoa orodha ya mahitaji tunayopaswa kutimiza ili tupate kibali chake (namna dini zingine wanafanya), Mungu wa Biblia alichukua mwili wa mwanadamu, akaishi kati yetu, na akawaruhusu watu aliowaumba kumtesa hadi kufa huku akiwasamehe (Luka 23:34; Wafilipi 2:5-11). Aina hiyo ya kujitoa, upendo wa dhabihu uu mbali na uzoefu wa mwanadamu na hauko miongoni mwa dini zilizotengezwa na mwanadamu. Neema ni dhana ambalo ni la kipekee kwa Mungu wa Biblia.

Miungu iliyotengezwa na mwanadamu huwa inahiga umbo la mwanadamu. Miungu ya tamaduni za kigeni imejawa na kasoro, hubadilika badilika, na kasoro kama zile za mwanadamu. Ni hafifu, binafsi, katili, na bila faida yoyote, kwa ufupi wanafanya namna ile iliyotengezwa na mwanadam watafanya, ikiwa na dhambi ile ile, na uchoyo unaopatikana ndani ya moyo wa mwanadamu. Ili Mungu awe aliumbwa na mwanadamu, asili yake ingefika pale mawazo ya mwanadamu yatapanuka kufika. Mungu wa Biblia kwa umbali anapita fahamu zetu, bali anatuachia vidokezo kama njia ya kiroho ili sisi tuifuate tunapokuja kumtambua vyema.

Jambo la tatu la kuzingatia katika swala la ikiwa Mungu aliumbwa na mwanadamu au la ni ubora wa kiroho wa moyo wa manadamu. Kila mwanadamu ni wa kipekee na ako na hisia za ndani za "mimi." Tuna uelewe wa kuzaliwa nao ndani kuhusu milele (Mhubiri 3:11) na hisia kuwa kunayo mengi baada ya ulimwengu huu. Mwanzo 1:27 yasema kuwa wanadamu waliumbwa kwa mfano wa Mungu; Wakolosai 1:16 yasema kwamba tuliumbwa kwa makusudi yake na mapenzi yake. Kwa njia fulani tuliumbwa kama yeye lakini haimanishi kuwa yeye anaonekana kama sisi (Hesabu 23:19). Ikiwa Mungu ni uwongo wa binadamu basi maswali mengi mapya hujibuka: Ni kitu gani huwafanya wanadamu tofauti na wanyama? Wanadamu huto dhana ya haki, ukarimu, kujitolea, na upendo- ambazo ni sifa hazipatikani kitika shamba la wanya? Sifa kama hizo zinapatikana kwa kila tamaduni ulimwenguni, hazingestahimili mchakato wa mchibuko. Ingawa, wakati tunaona sifa hizo zikijidhihirisha ndani ya sifa za Mungu mwenyewe tunaelewa ni kwa nini tunazimiliki.

Zingatio lingine katika suala la ikiwa Mungu aliumbwa na mwanadamu au la ni uaminifu wa Biblia. Ili ibishane kuwa Mungu hayuko, mtu lazima ashughulike kwa usahihi na kitabu ambacho humuelezea. Katika kuraza za Biblia, Mungu amejifunua yeye mwenyewe kwetu na ametupa mamia ya mifano ya jinsi amekuwa akishughulika na mwanadamu katika karne zote. Wengi wanaopinga kwa bidii dhidi ya uhalisi wa Mungu kwa kutojua hawaijui Biblia pia. Mara nyingi wanadai kuwa ni "kitabu cha kale kilichoandikiwa na Wayahudi wachache." Kauli kama hiyo inaonyesha msingi hafifu ambao juu yake mabishano yao yanategemea. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vilivyoandikwa na zaidi ya waandishi 40 tofauti zaidi ya miaka 1,500, na kutoka bara tatu, na lugha tatu tofauti. Lakini kikaunganishwa pamoja vipande vya hadhiti moja kama mchoro ukanganyao uliounganishwa pamoja. Biblia ni hadhiti ya Mungu ya naman ametafuta bila kukoma jinsi ya kukomboa viumbe wake walioanguka.

Wale ambao wanaamini wazo kwamba Mungu aliumbwa na mwanadamu lazime wazingatie njia ambayo Biblia inadhihirisha mwanadamu, hasa Wayahudi. Ikiwa Wayahudi waliandika Biblia ili kujiheshimu wenyewe walianguka vibaya. Hata Bwana mwenyewe alikuwa wazi kuwa aliwachagua Waisraeli kwa sababu zake mwenyewe, sio kwa sababu walistahili heshima maalum (Kumbukumbu 7:7). Mapungufu ya taifa la Israeli yanaonyeshwa tean na tena hadi pale kusulubiwa kwa Mwana wa Mungu (Isaya 65:2; Marko 15:9-15). Ubinadamu umedhihirishwa kweli kweli akiwa na dhambi, mwasi na adhabu. Hakuna kundi au mtu binafsi anasifiwa. Hii inaibua swali Dhahiri: ikiwa mwanadamu alianzisha wazo la Nungu, nia yake ilikuwa gani? Katika Agano la kale na Jipya shujaa pekee ni Mungu. Badala ya kupisha njia kwa manufaa ya kibinafsi, kweli za biblia zinaongoza kujitolea kwa dhabihu na kunyenyekea. Badala ya kutufundisha jinsi ya kupokea kibali cha Mungu, Biblia inatuonya kwamba hakuna mwenye haki (Warumi 3:10,23). katika historia yote wale wanaotangaza kweli za Biblia wameteswa hadi kufa, walipigwa mawe, na kuchukuliwa mahali fiche (1 Wafalme 19:10; Matendo 7:58; 2 Wakorintho 11:25).

Ikiwa wazo kuwa Mungu aliumbwa na mwanadamu, basi hakuna Mungu kwa kweli, na swali kubwa ambalo halijajibiwa linahusiana na ugumu na muundo msingi wa ulimwengu. Chembe moja ya DNA inaonyesha hekima ya maalum ambayo bahati ghafula haiwezi kuikaribia ili kuifafanua. Zaidi ya hayo, mabilioni ya chembe zilizoanishwa kikamilifu, molekuli mifumo, na ulimwengu hutusungumzia kuhusu Mbunifu. Kumwondoa Mungu kutoka ulimwngu wa maelezo hufanya njia ya maswali mengi yasiyo na majibu. Hamna elezo lingine litakuwa na maana. Nadharia zimeongezeka, lakini hamna hata moja inaweza dai uthibitisho Dhahiri wa kisayansi wa jinsi ulimwengu unaoshangaza uliunganishwa. Hata Charles Darwin aliweza kukubali kuwa, "kudhania kuwa jicho na udhaifu wake wote usiorekebika ili kuangazia mbali, kwa kukubali wingi wa mwanga tofauti, na urekebisho wa uduara wa asili na mpangilio wa sauti vingeundwa toka kwa asili teuzi, ninakiri kwa wazi upumbavu wa hali ya juu kabisa" ((The Origin of Species, J. M. Dent & Sons, Ltd., London, 1971, p. 167).

Hatuwezi kuondoa dhana ya Mungu bila kubadilishana na dhana ambayo ina maelezo ya kuridhisha. Maswali hayapotei kwa kuondoa uwezekano wa Mungu. Walakini, wakati tunaondoa ubaguzi na dhanio la kabla ambazo hukana kuruhusu Mungu kusingatiwa, Anabaki kuwa elezo makinifu kwa ulimwengu huu wa ajabu. Wale ambao wemeamua kwamba Mungu hawezi kuwepo hujenga mtazamo wao katika dhana hiyo na kujifanya kuwa majibu yao yaliyo na kasoro yanajaza pengo. Kukana kuwepo kwa Mungu dhanio za dini ambazo huto taswira mbaya kwa kile wanachoita kutafuta kweli. Walakini, wale wanaotamani kwa kweli kuwa na mawazo wazi na kutafuta ukweli popote itakayowaelekeza wanapata kuwa ushahidi wote huelekeza kwa Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mungu aliumbwa na mwanadamu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries