Swali
Ni kwa nini Mungu anaruhusu kuwe na walemavu/viwete?
Jibu
Bwana ni Mungu wa wale walio na afya nzuri ya kimwili, nguvu ya akili, na bado pia ni Mungu wa wale walio na ulemavu wa kimwili na akili. Yeye ni mwenye uwezo kwa walio wanyonge na wadhaifu vile vile Mungu wa werevu na wenye nguvu. Biblia inafunza kuwa kila mtu aliyezaliwa katika ulimwengu huu ni kiumbe cha ajabu (ona Zaburi 139:16), na hii ni pamoja na walemavu na viwete.
Swali la kawaida ni, ni kwa nini Mungu anaruhus baadhi ya watu kuzaliwa na udhaifu au ulemavu au ni kwa nini anaruhusu ajali zinazoleta udhaifu au ulemavu baadaye katika maisha. Swali liko chini ya mwavuli wa theolojia/mjadala wa kifalsafa uitwao "shida ya maovu" ua "shida ya uchungu." Ikiwa Mungu ni mwema na mwenye enzi, ni kwa nini anatuhusu mambo mabaya kutokea? Kuna haja gani mtu kupoteza uwezo wa kuona au kulazimishwa kutembea na sehemu bandia? Tunawezaje kuyaweka pamoja hoja Mungu kuwa mwema na mkamilifu ile hali ukweli ni kwamba viumbe wake vimevunjika na kulemazwa?
Kabla tuendelee, lazima tukubali kwamba kwa njia moja au nyingine sisi ni wadhaifu au walemavu. Haja kuwa na miwani inaonyesha udhaifu au ulemavu wa kuona. Vikaza meno ni dalili ya kutokuwa na meno dhabiti. Kisukari, ugonjwa wa yabisi kavu, uvimbe wa uso, kiungo chenye hakisongi vyema-hii inaweza chukuliwa kuwa ulemavu kwa kiwango fulani. Kizazi chote cha mwanadamu kinaisha na ukweli wa unyonge. Kila mtu anakumbana hali isiyo kamili. Sisi wote tumeadhirika kwa njia moja au nyingine. Ulemavu tunaoisho nao ni wa kiwango Fulani.
Wakati mtu ni mlemavu au kiwete iwe ni kiwango gani, ni dalili ya dhambi ya asili wakati dhambi iliingia duniani. Dhambi iliingia duniani kwa sababu ya mwanadamu kutomtii Mungu, na hiyo dhambi ilileta magonjwa, udhaifu, na maradhi (angalia Warumi 5:12). Ulimwengu ukalemazwa. Sababu moja ya Mungu anawaruhusu watu kuwa walemavu au viwete ni kwamba hali kama hizo ni matokeo ya asili ya uasi wa mwanadamu dhidi ya Mungu. Naam tunaishi ulimwengu ambao umeanguka. Yesu alisema kwamba, "Ulimwenguni mnayo dhiki" (Yohana 16:33). Hii sio kusema kuwa kila mlemavu ni kwa mjibu wa dhambi yake (Yesu aliangazia swala hili katika Yohana 9:1-3), lakini kusema kwa ujumla, kuwepo kwa viwete na walemavu ikifuatiliwa chanzo chake ni pale dhambi ilipoingia dunia.
Sababu ingine rahisi ya Mungu kuwaruhusu watu wengine kuwa walemavu au viwete ni kwamba Mungu atajitukuza mwenyewe. Huku wanafunzi wakishangaa kuhusu mtu aliyezaliwa kipofu, Yesu alisema, "bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake" (Yohana 9:3). Wakati wanafunzi hao hao baadaye walishangaa kuhusu ugonjwa wa Lazaro, Yesu aliwaambia, "bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo" (Yohana 11:4). Katika matukio yote mawili, Mungu alitukuzwa kupitia kwa ulemavu- katika hali ya mtu aliyezaliwa kipofu, viongozi wa hekalu walikuwa na udhibitisho potovu wa nguvu za Yesu za uponyaji; katika hali ya Lazaro, "Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini" (Yohana 11:45).
Sababu nyingine anaruhusu ulemavu na kasoro za mwili ni kwamba tujifunze kumtumainia badala ya kujitumaini. Wakati Bwana alimwita Musa jangwani, Musa alikawia kutii wito huo. Alijaribu kutumia ulemavu wake kama kijisababu cha kujinasua kutoka kwa huduma: "Bwana akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, Bwana? Basi sasa, enenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena" (Kutoka 4:11-12). Katika ukurasa huu wa ajabu kuwa uwezo wote wa binadamu na ulemavu wowote- ni baadhi ya mpango wa Mungu na Mungu atawazaidia watumishi wake. Hawaiti wale ambao wamejiami, bali anawaami awaitao.
Joni Eareckson Tada alipata jeraha akiwa kijana wakati wa kupiga mbizi, na miongo mitano iliyopita amekuwa akiishi na ulemavu huo. Joni huwaza kukutana na Yesu mbinguni na kusungumza naye kuhusu machela yake: "Nilivyo zidi kuwa mdhaifu nilikuwa katika machela ile, zaidi nilivyokutegemea. Na nilivyo kutegemea zaidi, zaidi niligundua jinsi ulivyo na nguvu. Haingewezekena pasingekuwa na mkwaruso wa hii machela ya baraka." Joni anamuitikio mtume Paulo ambaye alikubali kuwa neema ya Kristo ilimtosha kwa mwiba uliokuwa mwilini mwake kwa maneno haya: "Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu... Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu" (2Wakorintho 12:9-10).
Sababu nyingine ya Mungu kuruhusu watu wengine kuwa na ulemavu au viwete ni kwamba, katika mpango wake mkuu amevichagua vilivyo vinyonge vya dunia hii kwa manufaa maalum: "bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu" (1Wakorintho 1:27-29).
Mungu haitaji uwezo wa mwanadamu au ubunifu wake au ustadi wake kukamilisha kazi yake. Anaweza kutumia wadhaifu na walemavu vile vile. Anaweza kutumia Watoto: "Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe; Uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi" Zaburi 8:2). Anaweza kutumia mtu yeyote. Kumbuka ukweli huu unaweza saidia waumuni walemavu kuendelea kumtazamia Mungu. Ni raisi kutaka kufa moyo hasa wakati maisha hayana maana tena, lakini nguvu za Kristo zimekalimilishwa katika unyonge (2Wakorintho 12:9).
Kwa kadri, wakati Yesu alikuja katika ulimwengu huu, alikuwa mlemavu kwa hiari. Alijilemaza yeye mwenyewe huku akiruhusu ukamilifu wa mbinguni kuishi miongoni mwa wenye dhambi duniani. Aliuweka utukufu wake ndio avae ubinadamu usio na utukufu. Katika ubadilisho wake, Yesu aliuchukua mwili wa binadamu na unyonge wake pamoja na udhaifu wake wote. "bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa" (Wafilipi 2:7). Mwana wa Mungu alitwaa sehemu ya ubinadamu wetu na akatezeka kwa ajili yetu. Na ndio maana, "hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu" (Waebrania 4:15); badala yake, tuna mwombezi ambaye anaelewa, na kuhusiana na udhaifu wetu na anajua uchungu wetu.
Mungu anaahidi kuwa ulemavu na udhaifu ni wa muda. Hali hizo ni sehemu ya ulimwengu huu ulio anguka, sio ule ulimwengu ujao. Watoto wa Mungu-wale kupitia kwa Imani katika Kristo wamefanywa wana wa Mungu (Yohana 1:12)-wako na hatima inayong'aayo na yenye utukufu. Wakati Yesu alipokuja mara ya kwanza, Alitupa kionjo cha mambo mazuri yajayo: "wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya" (Mathayo 4:24). Yesu atakapokuja kwa mara ya pili, "Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa. Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani" (Isaya 35:5-6).
Mtazamo wa Joni wa kufungwa katika machela ni wa kufungua macho: "Pengine walemavu wa kweli ndio hawamuitaji Mungu." Hali unyonge, ulemavu, na udhaifu-hali ya kumwamini Mungu katika ulimwengu huu- ni hali ya heshima na baraka kwa kweli.
English
Ni kwa nini Mungu anaruhusu kuwe na walemavu/viwete?