Swali
Mungu anasema mini ni nani?
Jibu
Wengi wetu tunapoteza muda tukijusumbua juu ya kile watu wengine wanafikiria juu yetu. Tunataka kuthaminiwa, kupendwa, kuheshimiwa, kutamanika. Lakini ni kwa nini tutegemee utambulisho wetu na hisia ya kujistahi juu ya maoni ya watu wengine wenye kasoro ilhali maoni ya Mungu kutuhusu ndiyo pekee yaliyo muhimu? Swali muhimu zaidi tunaloweza kuuliza kuhusu utambulisho wetu ni hili: Je! Mungu anasema mimi ni nani? Biblia ina majibu pekee ya kutegemewa kuhusu sisi ni nani katika Kristo na kile ambacho Mungu anatuwazia sisi ambao tumezaliwa mara ya pili.
La kwanza kabisa, Mungu anaseme mimi ni mtoto wake mpendwa: “Tazameni ni pendo kuu namna gani alilotupa Baba, kwamba sisi tuitwe wana wa Mungu! Na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye” (1 Yohana 3:1). Mungu haogopi kueleza upendo wake usio na mipaka kwetu; Anathibitisha mara kwa mara katika Maandiko kwamba sisi tumezaliwa na Mungu, watoto Wake wa kuthaminiwa sana (Yohana 1:12-13; 2 Wakorintho 6:17-18; Wagalatia 3:26; Warumi 8:17; Isaya 43:1).
Mungu anasema nimechaguliwa, nimefanywa kuwa mwana katika familia yake kwa njia ya Yesu Kristo ili niwe mtoto wake milele: “Kwa maana alituchagua katika yeye kabla ya kuumbwa ulimwengu ili tuwe watakatifu na bila lawama mbele zake. Kwa upendo alitangulia kutuchagua tuwe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo kwa furaha yake na mapenzi yake mwenyewe. Kwa hiyo tunamsifu Mungu kwa huruma zake kuu alizotumiminia sisi katika Mwanawe Mpendwa” (Waefeso 1:4-6 soma pia 1 Wathesalonike 1:4; 2:13).
Mungu anasema mini ni wa thamani. Anasema mimi ni kazi ya mikono yake: “Kwa maana sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tupate kutenda matendo mema, ambayo Mungu alitangulia kuyaandaa tupate kuishi katika hayo” (Waefeso 2:10). Sisi sio mabonge ya udongo nasibu. Mungu anasema sisi ni matokeo ya ustadi wake wa kisanaa na ufundi. Mungu alituumba kwa umbo na mfano wake (Mwanzo 1:26-27; 5:1; 9:6; Yakobo 3:9).
Mungu anasema nimekombolewa. Sisi ni wenye dhamani kubwa kwa Mungu hivi kwamba alitununua kwa damu yenye thamani ya Mwana Wake, Yesu Kristo: “Kwa maana mnafahamu kwamba mlikombolewa kutoka mwenendo wenu usiofaa ambao mliurithi kutoka kwa baba zenu, si kwa vitu viharibikavyo kama fedha na dhahabu, bali kwa damu ya thamani ya Kristo, yule Mwana-Kondoo asiye na dosari wala doa” (1 Petro 1:18-19). Kupitia kwa damu ya Yesu Kristo tumesamehewa na kuwekwa huru kutoka katika dhambi: “Ndani yake tunao ukombozi kwa njia ya damu yake, yaani, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake” (Waefeso 1:7 soma pia Wagalatia 5:1; 1 Wakorintho 6:20; 1 Yohana 1:9).
Mungu anasema mimi ni kiumbe kipya katika Kristo Yesu. Kupitia wokovu Wake, tunapata utambulisho mpya kabisa na maisha mapya kabisa: “Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya” (2 Wakorintho 5:17; soma pia Waefeso 4:24). Anasema mimi ni haki ya Mungu katika Kristo Yesu (2 Wakorintho 5:21), hekalu hai la Roho Wake Mtakatifu (1 Wakorintho 3:16), na mtakatifu (Waefeso 2:19; Wafilipi 4:21).
Mungu anasema mimi ni Rafiki yake. Kupitia uhusiano na Yesu, Mungu anashiriki moyo wake nasi: “Siwaiti ninyi watumishi tena, kwa sababu watumishi hawajui bwana wao analofanya, bali nimewaita ninyi rafiki, kwa maana nimewajulisha mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu” (Yohana 15:15).
Mungu anasema mimi ni balozi wake (2 Wakorintho 5:20; Waefeso 6:20), nuru Yake gizani, na mshahidi Wake kwa ulimwengu (Mathayo 5:13-16; Matendo 1:8; Waefeso 5:8). Mungu ametukabidhi kazi ya kuwafanya wanafunzi (Mathayo 28:19).
Mungu anasema mimi ni mshirika wa mwili wa Yesu Kristo: “Siri hii ni kwamba, kwa njia ya Injili, watu wa Mataifa ni warithi pamoja na Israeli, viungo vya mwili mmoja na washiriki pamoja wa ahadi katika Kristo Yesu” (Waefeso 3:6; soma pia 5:30). Kwa sababu mimi ni wa Kristo-nimeunganika Naye katika maisha Yake, kifo, kufufuka, na kutukuka Kwake (Yohana 15:1-10; Warumi 6:4-6; Waefeso 2:6)-Mungu anasema mimi ni mrithi wa Ufalme Wake na utukufu Wake (Wagalatia 4:7; Waefeso 1:11; Warumi 8:17), raia wa mbinguni (Wafilipi 3:20).
Mungu anasema nimependwa zaidi: “Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu” (Warumi 5:8; soma pia 8:31-39; Yohana 3:16-17). Upendo wake kwetu ni mkuu sana kwamba alitupa uzima kwa rehema: “Lakini Mungu kwa upendo wake mwingi kwetu sisi, ambaye ni mwingi wa rehema, hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu, yaani, mmeokolewa kwa neema” (Waefeso 2:4-5).
Kadri tunavyojifunza Neno la Mungu, ndivyo tunavyogundua sisi ni nani ndani ya Kristo. Tunabadilishwa kuwa mtu ambaye Mungu anasema sisi tuko wakati tunamfanya Yesu Kristo kuwa kile tunatafuta katika maisha yetu: “Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji tunadhihirisha utukufu wa Bwana, kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, utokao kwa Bwana, ambaye ndiye Roho” (2 Wakorintho 3:18; soma pia Warumi 8:29; 12:2; Wafilipi 1:6; Waefeso 4:15).
English
Mungu anasema mini ni nani?