settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Mungu hutaka, hutafuta, au kuomba kwamba tumwabudu?

Jibu


Kuabudu ni "kutoa heshima, ustahi, uchaji, ibada, sifa, au utukufu kwa aliye mkuu." Mungu anaomba ibada kwa sababu ni Yeye peke yake anayestahili. Yeye ndiye pekee anayestahiki ibada. Anaomba kwamba tutambulishe ukuu wake, nguvu zake, na utukufu wake. Ufunuo 4:11 inasema, ''Wastahili ee Bwana Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na nguvu; Kwa maana Wewe uliumba vitu vyote, Na kwa mapenzi yako zipo na zimeumbwa. "Mungu alituumba, na Yeye hatonyang'anywa ufalme. Aliwaamuru Waisraeli: "Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu kwa miungu ya uongo, au kinyango cha chochote mbinguni, katika nchi au chini au majini chini ya dunia. Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nnecha hao wanichukiao.

"(Kutoka 20: 3-5). Lazima tuelewe kwamba wivu wa Mungu sio wivu wa dhambi ambao tunapata, uliozaliwa kwa kiburi. Ni wivu mtakatifu na mwenye haki ambao huwezi kuruhusu utukufu unaofaa tu kwake Yeye upewe mwingine.

Mungu anatarajia tumwabudu Yeye kama mfano wa heshima na shukrani kwake. Lakini Mungu anatarajia pia sisi kumtii. Yeye hahitaji tu kupendwa; Anataka tufanyie haki kwa kila mmoja, kuonyesha upendo na huruma kwa wengine. Kwa njia hii, tunajionyesha kwa yeye kama dhabihu iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza kwake. Hii inatukuza Mungu na ni "huduma yetu ya busara" (Warumi 12: 1). Tunapoabudu na moyo wenye utii na roho iliyo wazi na ya kutubu, Mungu hutukuzwa, Wakristo wanatakaswa, kanisa linaadilika, na waliopotea wanahubiriwa. Hii ni baadhi ya viungo vya ibada ya kweli.

Mungu pia anatamani kwamba tunamwabudu Yeye kwa sababu ibada ni majibu ya asili na yaliyotarajiwa baada ya Yeye kutuokoa kupitia Yesu Kristo. Wafilipi 3: 3 inaelezea kanisa la kweli, mwili wa waumini katika Yesu Kristo ambao hatima yake ya milele ni mbinguni. "Watu waliotahiriwa kikweli ni sisi, si wao; kwani sisi twamwabudu Mungu Kwanjia ya Roho Wake, na kuona fahari katika kuungana na Yesu Kristo. Mambo ya nje tu hatuyathamini". Kwa maneno mengine, kanisa linajulikana kama watu wa Mungu, lakini siyo kwa kutahiriwa kimwili. Kanisa ni wale wanaomwabudu Mungu katika roho yao wakifurahia katika Kristo, na hawajitegemeaiwenyewe kwa wokovu. Wale ambao hawaabudu Mungu wa kweli na aliye hai sio wake, na hatima yao ya milele ni kuzimu. Lakini waabudu wa kweli wanajulikana kwa ibada yao ya Mungu, na hatima yao ya milele ni pamoja na Mungu wanaoabudu na kusujudu.

Mungu anataka, hutafuta, na kuomba ibada yetu kwa sababu Yeye anastahili, kwa sababu ni tabia ya Mkristo kumwabudu Yeye, na kwa sababu hatima yetu ya milele inaitegemea. Hiyo ndiyo makusudiya historia ya ukombozi: kuabudu Mungu wa kweli, hai, na mwenye utukufu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Mungu hutaka, hutafuta, au kuomba kwamba tumwabudu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries