Swali
Je, Mungu anathibitika? Nawezaje kujua ya kwamba kweli Mungu ni dhahiri?
Jibu
Tunajua ya kwamba Mungu anathibitika kwa kuwa amejidhihirisha kwetu kwa njia tatu: katika uumbaji, katika neno lake na katika mwanawe, Yesu kristo.
Kithibitisho cha msingi ya kuweko kwa Mungu ni katika vile alivyoviumba. “ Kwa yale yasiyoonekana na macho juu yake katika uumbaji yanadhihirika waziwazi, akieleweka kwa yale aliyoyaumba, hata uwezo wake wa milele na mungu Baba ili (wasioamini) wawe hawana kisingizio” (Warumi 1:20). “Mbingu zinashuhudia utukufu wa Mungu, na anga yadhihirisha kazi za mikono yake” (Zaburi 19:1).
Kama ningeona saa ya mkono katikati ya uwanja, singechukulia tu imejitoa tu yenyewe kutoka mahali Fulani wala kuwa ilikuweko hapo toka jadi. Kutokana na muundo wake ningejua ya kuwa iliundwa na mtu Fulani stadi. Hata hivyo ninaona miundo mingi ya vitu tofauti tofauti katika mazingira yetu. Kutazama nyakati kwetu hakutokani na saa za mikono balikazi za mkono wa Mungu --- kuzunguka kwa dunia (na hali za kitonoradi za atomi ya cesium-133). Ulimwengu unadhihirisha kazi za ustadi zinazothibitisha kuweko kwa mwenye kuviumba kwa ustadi.
Ningepokea ujumbe kupitia mtandao Fulani ambao hausomeki ningemtafuta mwenye utaalamu wa kusambaza habari kupitia mitandao ilianifahamishe kuhusiana na jinsi ningeweza kuutafsiri na kuusoma. Ningekuwa na uhakika kuna mtaalam aliyenitumia ujumbe na mwenye ufahamu juu ya kuutafsiri. Je, tafsiri ya ujumbe unaobebwa ndani ya chembe chembe za mwili wa mwanadamu za “DNA” si ngumu zaidi? Je, hii haitoshi kukujulisha juu ya mtaalam wa hali ya juu zaidi?
Mungu hakuumba tu ulimwengu mgumu kufafanua bali pia ameweka ndani ya moyo wa kila mwanadamu umilele (Mhubiri 3:11). Mwanadamu ana hisi ndani ya moyo wake kwamba kuna mengine zaidi ndani ya maisha yake kuliko yale ayaonayo na macho yake. Haya huthibitika katika mambo mawili: katika utunzi wa sheria na ibada.
Kila aina ya kizazi duniani kimezingatia aina Fulani ya mfumo wa kisheria unaofanana.Kwa mfano swala la mapenzi limeheshimiwa ulimwenguni kote na uongo umekataliwa duniani kote. Utamaduni huu wa kujua mema na mabaya unadhihirisha kuwepo kwa mtakatifu mmoja aliyetupatia mwongozo huu.
Kwa njia hiyo hiyo,duniani kote watu wameendelea kufanya ibada kwa Mungu bila kujali mila na desturi zao. Lengo la ibada laweza kutofautiana lakini kuwepo kwa Mungu hakupingiki. Kuendelea kwetu kufanya ibada ni kwa sababu Mungu alituumba, “Kwa mfano wake” (Mwanzo 1:27).
Mungu pia amejidhihirisha kwetu katika neno lake Biblia. Ndani mwote ya maandiko, swala la kuwapo kwa Mungu lashughulikiwa kama la waziwazi (Mwanzo 1:1; Kutoka 3:14). Benjamin Franklin alipoandika habari zake mwenyewe hakupoteza muda kuthibitisha kama yeye mwenyewe alikuwapo. Vivyo hivyo Mungu hapotezi muda kuthibitisha kama yeye mwenyewe yupo ndani ya maandiko yake. Hali yake ya kubadilisha maisha ya mwanadamu, heshima na miujiza iliyoandamana na kuandikwa kwake kunatosha kuvutia mtu ayaangalie maandiko kwa makini.
Njia ya tatu ambayo Mungu alijidhihirisha nayo ni kupitia mwanawe Yesu kristo (Yohana 14:6-11). “Hapo mwanzo kulikuwako neno; na neno alikuwako kwa Mungu na Huyo neno alikuwa Mungu… na neno akafanyika mwili, akakaa pamoja nasi” (Yohana 1;1, 14). Ndani ya Yesu kristo, “mnadumu utimilifu wote wa Mungu Baba katika mwili” (Wakolosai 2:9).
Ndani ya kuishi kwake Yesu kristo, alizingatia Agano la kale lote kwa ukamilifu na kutimiza unabii woye unaohusiana na masihi (Mathayo 5:17). Alitenda miujiza mingi na kuwahurumia wengi kuuthibitisha ujumbe wake kuwa alikuwa Mungu (Yohana 21:24-25). Tena siku tatu baada ya kusulubiwa kwake akafufuka kutoka kwa wafu jambo lililothibitishwa na wengi (Wakorintho wa kwanza 15:6). Historia yote imejaa ithibati ya Yesu alikuwa nani. Kama mtume Paulo alvyosema, “mambo haya hayakufanyika pembeni” (Matendo 26:26).
Tunajua kuwa wengine watasoma ushahidi huu na mawazo yao wenyewe na baada ya kuufahamu vyema wakubali. Wengine hata baada ya ushahidi huu bado watarudia hali zao za kutoshashawishika (Zaburi 14:1) Yote yanahitaji Imani (Waebrania 11:6).
English
Je, Mungu anathibitika? Nawezaje kujua ya kwamba kweli Mungu ni dhahiri?