Swali
Je! Mungu anatuhitaji?
Jibu
Mungu ni mtakatifu, wa milele, Mwenye nguvu, na anayejitoshelesha kabisa. Hahitaji kiumbe chochote, lakini tunamhitaji Yeye. Uumbaji wote unategemea maisha ambayo Mungu peke yake anaimarisha. " Huyameesha majani kwa makundi," na "Hao wote wanakungoja Wewe, Uwape chakula chao kwa wakati wake. . . . Waiondoa pumzi yao, wanakufa, Na kuyarudia mavumbi yao (Zaburi 104: 14, 27, 29).
Mungu, kwa upande mwingine, hatagemei kitu chochote au mtu yeyote. Hasumbuli na ukosefu, hazuiliki ni kitu chochote, na hana uzoefu wa upungufu. Yeye ni " MIMI NIKO AMBAYE NIKO" bila sifa au ubaguzi (Kutoka 3:14). Ikiwa alihitaji kitu chochote ili aishi au kujisikia kamili, basi Yeye hangekuwa Mungu.
Kwa hiyo, Mungu hatuitaji. Lakini, kwa kushangaza, Yeye anatupenda, na kwa wema Wake anataka tuishi pamoja Naye milele. Kwa hiyo miaka 2,000 iliyopita, Mungu Mwenyewe amevaa ngozi, alikuja duniani, na alitoa uhai wake kwa msamaha wa dhambi zetu na kuthibitisha upendo wake wa kina kwa ajili yetu. Alilipa bei ya mwisho kutupatanisha na yeye mwenyewe, na hakuna mtu anayeweza kulipa gharama hiyo ya dhamani kwa kitu ambacho hakitaki au kukithamani.
Yesu hakika alijua kile ambacho kukumbana nacho mwishoni mwa huduma yake duniani (Marko 8:31; Yohana 18: 4). Katika maumivu yake huko Gethsemane, alipokuwa akisali kuhusu majaribu ambayo yangemjia, jasho la damu lilimwagika kutoka kwenye uso wake (Luka 22:44). Na kwa hakika Yesu alijua vizuri sana unabii wa Isaya 52:14, "Kama vile wengi walivyokustaajabia, uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake zaidi ya wanadamu." Mwana wa Adamu alipigwa mfupa kwa kiasi kwamba Yeye hakuonekana tena kuwa kama mwanadamu. Na mateso hayo yalifuatiliwa na kitu kibaya zaidi, kusulubiwa kwenyewe, namna ya maumivu zaidi na maovu iliyo waitekelezwa.
Yesu alipokuwa akipigwa msalabani, Baba yake mbinguni "akageuka" kutoka kwake. Habakuki 1:13 inathibitisha kwamba macho ya Mungu "wewe usiyeweza kutazama ukaidi." Na wakati huo, Kristo alilia, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?" (Mathayo 27:46).
Hii ndio bei Mungu alilipa kwa niapa yetu, na hivi ndivyo tunavyojua jinsi anavyotupenda. Kwa sababu ya upendo huu wa ajabu na usiofaa kwetu sisi wenye dhambi wasiotii, tumepewa uzima wa milele. Wokovu ni zawadi, iliyotolewa kwa hiari bila kuuliza, kwa sababu ya kuchukua uhai, kwa hiari dhabihu ya Mungu mmoja wa kweli. Warumi 5: 8 inasema, "Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi."
Mara tu umejiunga na Kristo, hakuna kitu kinachoweza kututenganisha na Yeye. Warumi 8: 38-39: "Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu."
Waumini katika Kristo wamefanywa wapya. Tunaelewa kina cha upendo wake kwetu: "Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu" (Wagalatia 2:20).
Wewe, pia, unaweza kujizamasha ndani ya upendo wa milele wa Mungu kwako na kujua uhakikisho wa uzima wa milele. Endelea kusoma hapa ili ujifunze maana ya kukubali Kristo kama Mwokozi wako binafsi.
English
Je! Mungu anatuhitaji?