Swali
Mungu anaweza fanya dhambi? Ikiwa Mungu hawezi sini, je kwa kweli yeye ni mwenye nguvu zote?
Jibu
Ili kujibu swali hili, kwanza lazima tusingatie Mungu ni nani. Mawazo ya binadamu hayawezi kuelewa kikamilifu Mungu ni nani pasingekuwa na ufunuo maalumu ambao ametupa. Njia moja ya huo ufunuo ni kupitia uumbaji wa Mungu (Zaburi 19:1-6). Uajabu wa uumbaji, muundo na mpangalio unatuelekeza kutambua kuwa kuna Muumbaji wa ajabu ambaye alisababisha vinavyoonekana na kuviudumisha.
Njia nyingine Mungu hujifunua ni kupitia Neno lake andishi. Kutoka kwa sehemu za Maandiko tunaweza kukadiria sifa au uadilifu ambao uu ndani ya Mungu, ambao hutupa mwanga kuhusu maadili yake. Mwanatheolojia mmoja anatasema kuwa maadili yake ni "ukamilifu wake." Baadhi ya hayo ni: Umilele wake (Zaburi 90:2); kutoharibika kwake, au ubora usio badilika (Yakobo 1:17); upendo wake (1Yohan 4:8); uwezo wake wote, au kuwa na mamlaka yote, Mwenyezi (Ufunuo 1:8); Kuwepo kwake kila mahali, au kuwa kila mahali wakati mmoja (Zaburi 139:7-11); utakatifu wake, usafi wake na kujitenga na dhambi (Habakuki 1:13), matakwa yake au haki yake (Zaburi 11:7), na kweli yake (Tito 1:2).
Hii ni taswira fupi ya Mungu ambaye hujidhihirisha mwenyewe katika utatu, Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu na maadili yake au ukamilifu wake vi kweli katika kila mhusika wa utatu. Kwa sababu Mungu ni mtakatifu, haki na kweli, hawezi akafanya chochote chenye hakiambatani naye, na tunaafikia hitimizo hili kwamba Mungu hawezi kufanya dhambi. Huku usafi, utakatifu na ukamilifu wingine wa Mungu ni zile Mungu alivyo na ikiwa Mungu angekuwa anafanya dhambi basi angekosa kuwa Mungu. Kweli kuwa Mungu ni "mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu" humzuia kufanya chochote ambacho si kitakatifu kwa mfano dhambi.
Hatuwezi tamatiza hata hivyo bila kutambua kweli ya ajabu kuwa Mungu mtakatifu anajihusisha mwenyewe katika dhambi ya mwanadamu. Alimtuma mwana wake wa pekee katika ulimwengu huu afe ili alipe deni ya dhambi. "Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa" (1Petro 3:18). "Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa" (1Petro 2:24). "kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake" (Warumi 3:23-25).
English
Mungu anaweza fanya dhambi? Ikiwa Mungu hawezi sini, je kwa kweli yeye ni mwenye nguvu zote?