settings icon
share icon
Swali

Kunalo jambo ambalo Mungu hawezi kutenda?

Jibu


Katika majira ya usiku wakati anga li wazi, angalia nyota angani. Mwanza 1 inanakili kuwa Mungu aliziumba zote! Hebu fikiria mwanga wa nyota moja! Lakini hiyo sio umeme halisi. Katika anga kuna ujuzi na mcharo ndani yake hata ile chembe chembe nyembamba, hata vile vitu vidogo vidogo vinavyoguzika. Nguvu za Mungu na ubasara wake zinapita fahamu zetu. Ndiposa Bwana akamwambia Ibrahimu katika Mwanzo 18:14,"Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana?" Ndio maan Bwana akamwambia Musa wakati Musa alishuku jinsi Mungu angeleta nyama kwa mamilioni ya Waisraeli jangwani, ''Je! Mkono wa Bwana umepungua urefu wake?" (Hesabu 11:23). Ndio maana Yonathani alimwambia yule kijana aliyemchukulia silaha zake kwamba Bwana hakuitaji jeshi kubwa ndio apate ushindi (1Samueli 14:6).

Yeremia 32:17 yasema, "Aa! Bwana MUNGU, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lililo gumu usiloliweza." Hata katika ulimwengu wa kiroho wale wanaonekana kuwa mbali na wokovu kwake haikui ngumu kuwafikia (Marko 10:25-27). Na vile nguvu zake ni kuu, upendo wake na rehema zake vile vile ni kuu… kufika kiwango cha kuwa tayari kumtuma Mwanawe kufa msalabani ili kulipa adhabu ya dhambi ya mwanadamu. Alifanya hili ili Yeye katika haki kamili, aweze kuwasamehe wale wote watakao geuka toka tegemeo nafsi na dhambi hadi kumtegemea Kristo na kazi yake iliyokamilika msalabani. Yohana 3:16, aya inayojulikana na wengi inaelezea upendo mkuu wa Mungu: "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." Upendo huu haukuwa wa watu "wema" pekee (na hakuna hata mmoja), bali wetu sisi wote…tulioanguka, wenye dhambi, tusiopendeka, na watu wanaoasi (Warumi 3:10-23)… na huku alichagua kutunyeshea upendo wake (Warumi 5:6-10) hata wakati hatukuustahili.

Kitu pekee ambacho Mungu hawezi kufanya ni kutenda kilicho kinyume na sifa yake an asili yake. Kwa mfano, Tito 1:2 yasema kwamba hawezi kudanganya. Kwa sababu yeye ni mtakatifu (Isaya 6:3; 1Petro 1:16), hawezi kutenda dhambi. Kwa sababu Yeye ni wa haki, hawezi fumba macho yake kwa dhambi. Kwa sababu Kristo alilipa adhabu ya dhambi, Yeye saa hii ana uwezo wa kusamehe wale ambao watamgeukia Kristo (Isaya 53:1-12; Warumi 3:26).

Kwa kweli Mungu wetu ni wa ajabu…habadiliki, ni wa milele, nguvu zake hazina kipimo, kwa uweza, kitika maarifa, kitika busara, katika upendo, katika rehema na katika utakatifu. Walakini hata sisi pia tu kama Waisraeli ambao hata baada ya kumwona Mungu akionesha nguvu zake na Upendo kila mara, walishauku upondo wake na nguvu zake pindi tu walipokabiliana na majaribu mapya maishanani mwao (mfano, Hesabu 13-14). Mungu na atusaidie kumheshimu kwa mtegemea na kumtumainia katika "hali" tutakayo kabiliana, maana yeye ni "msaada wetu daima wakati wa taabu" (Zaburi 46:1).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kunalo jambo ambalo Mungu hawezi kutenda?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries