Swali
Je, Mungu hufanya makosa?
Jibu
Mungu hafanyi makosa yoyote. Ukamilifu wake na ukuu wake hauruhusu makosa: "Bwana ni mkuu na anastahili sifa; ukuu wake hakuna mtu anayeweza kufahamu "(Zaburi 145: 3). Katika lugha ya asili, neno linalotafsiriwa kama"kutafakari" linahusisha mawazo ya "uwezo wa kufafanua au kuhesabu" Kwa maneno mengine, ukuu wa Mungu hauwezi kuwa na kipimo fulani. Neno hili haliwezi kutaja mtu aliye na hatia, kwa kuwa, hata kwa kosa moja, ukuu wake ungekuwa wa pekee na wa mwisho. Mungu ana uwezo wa kufahamu chochote kile na hawezi fanya makosa. Bwana wetu ni mkuu, ana nguvu nyingi.'' (Zaburi 147:5). Kwa mara nyingine, maandiko yanaonyesha kwamba Mungu hawezi kuwa na kosa. Upungufu wa hekima huchangia kuweo kwa makosa, lakini mungu ana hekima isiyo na mwisho na hafanyi makosa.
Mungu hakufanya makosa katika uumbaji wake wa ulimwengu. Hekima isiyo na mwisho ya Mungu, nguvu isiyo na mwisho, na wema usio na mwisho umejumuishwa pamoja ili kuufanya ulimwengu mkamilifu. Baada ya siku sita za uumbaji, Mungu alichunguza yote aliyoifanya na kuiita "nzuri sana" (Mwanzo 1:31). Hamna chochote kilikua na kasoro,vyote vilikua vizuri.
"Mungu si mtu, aseme uongo, wala si binanadamu, abadili nia yake. Je! Ataahidi kitu na asikifanye? Au kusema kitu asikitimize?"(Hesabu 23:19). Tofauti na mwanadamu, Mungu hafanyi makosa na huwa habadilishi nia. Mungu hakufanya amri ambazo lazima apate kufuta kwa sababu hakuwa na matokeo yote au kwa sababu hakuwa na uwezo wa kutimiza. Pia, Mungu si kama mtu ambaye dhambi yake inahitaji hukumu. "Mungu ni mwangaza; ndani yake hakuna giza hata "(1 Yohana 1: 5b). "Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote na mwaminifu katika yote anayofanya" (Zaburi 145: 17).
Wengine wanadai kwamba Maandiko yanaonyesha Mungu kuwa na mawazo ya pili juu ya uumbaji wake: "Mwenyezi Mungu alipoona wingi wa uovu wa binadamu duniani na kwamba kila analokusudia binadamu moyoni mwake ni ovu daima. Mwenyezi Mungu alisikitika sana kwa kumuumba mwanadamu duniani. Mwenyezi Mungu alihuzunika sana moyoni mwake. Hivyo akasema, "Nitamfuta kabisa duniani. Binadamu niliye muumba; nitafutilia mbali pia wanyama wa porini, viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Ninasikitika kwamba niliwaumba duniani''( Mwanzo 6: 5-7).
Ni vizuri kuelewa neno la majuto katika kifungu hiki. Ikiwa neno hilo limetumika kiMungu, kujuta huhusisha mawazo ya huzuni ya huruma na hatua iliyochukuliwa. Mungu hakuonyesha udhaifu, kukubali kosa, au kujuta kwa sababu ya kosa. Badala yake, alikuwa akielezea haja yake ya kuchukua hatua maalum, ya kupambana na uovu wa wanadamu: "Kila kitu walichofikiri au kufikiria kilikuwa kibaya kabisa" (Mwanzo 6: 5). Kuwepo kwa dunia kunathibitisha ukweli kwamba Mungu hakuona makossa katika uumbaji wake. Bado tunaishi ijapokuwa sisi ni wenye dhambi. Sifa kwa Bwana kwa neema yake: "Lakini pale dhambi ilipoongezeka, neema iliongezeka zaidi" (Warumi 5: 20b), na "Nuhu akapata neema machoni pa BWANA" (Mwanzo 6: 8).
Mungu hajawahi kufanya makosa. Amekuwa na madhumuni katika kila kitu, na matokeo hayatomshangaza yeye, kwa maana anatangaza mwisho tangu mwanzo: "Mimi ndimi Mungu, na hakuna mwingine; Mimi ni Mungu, wala hakuna mwingine kama mimi. Nilitangaza mambo ya mwisho tangu mwanzo, tangu kale nilitangaza mambo ya mwisho yatakayotukia. Lengo langu litatimia; mimi nitatekeleza nia yangu yote "(Isaya 46: 9) -10).
Binadamu anaweza kufikiria Mungu amefanya kosa katika maisha yake. Baadhi ya matukio na masharti zaidi ya udhibiti wetu hutufanya tufikirie kana kwamba Mungu amefanya hitilafu fulani. Hata hivyo, "tunajua kwamba katika mambo yote Mungu hufanya kazi na kuifanikisha pamoja na wote wampendao, yaani wale aliowaita kadiri ya kusudi lake". (Waroma 8:28). Hii inahitaji imani kukubali, lakini "tunaishi kwa imani, si kwa kuona" (2 Wakorintho 5: 7). Katika kila kitu tunapaswa kuelewa kwamba mambo ya maisha haya yanatumika na hutumiwa kwa ajili ya tuzo yetu ya milele kulingana na hekima ya Yeye "Kwake yeye awezaye kuwalinda msije mkaanguka, na kuwaleta nyinyi bila hatia mpaka mbele ya utukufu Wake."(Yuda 1:24). Tunaweza kufurahi kwamba Bwana wetu Mungu hafanyi makosa katika maisha yetu bali ana lengo la njema na la upendo kwa kila kitu anachoruhusu.
Hakuna kosa katika Mungu wetu; hakuna makosa aliyoyafanya. Na hakuna kosa katika Mwanawe; Yesu hakufanya dhambi katika mawazo, neno, au tendo (Waebrania 4:15). Shetani alikuwa na hamu ya kufunua hata kosa moja katika Yesu, lakini Ibilisi alishindwa kabisa katika majaribio yake (Mathayo 4: 1-11). Yesu alibaki kondoo wa Mungu asiye na doa (1 Petro 1:19). Mwishoni mwa maisha ya Yesu, hakimu wake wa duniani, Pontio Pilato, alitangaza, "Sioni kosa ndani ya mtu huyu" (Luka 23: 4).
Tunaishi na makosa yetu, kubwa na kidogo, madogo na mabaya, na tunazoea kuyafanya. Lakini tunamtumikia Mungu asiye na hatia, asiye na uovu ambaye ukuu wake hauwezi kueleweka. " Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, umetufanya mengi ya ajabu, na mipango yetu haihesabiki; hakuna yeyote aliye kama wewe. Kama ningeweza kusimulia hayo yote, idade yake ingenishinda"(Zaburi 40: 5). Ni vizuri kujua kwamba Mungu ndiye anayeshika usukani na kwamba Yeye asiyefanya makosa anaweza zaidi ya fidia kwa ajili yetu.
English
Je, Mungu hufanya makosa?