Swali
Mungu ananionaje katika Kristo?
Jibu
Sehemu nyingi katika Maandiko hurejelea waumini wakiwa “katika Kristo” (1 Petro 5:14; Wafilipi 1:1; Warumi 8:1). Wakolosai 3:3 inatupa ufahamu zaidi: “Kwa maana ninyi mlikufa, nao uhai wenu sasa umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.” Wakati tunakuja kwa Kristo kama wenye dhambi waliovunjika, Yeye hubadilisha dhambi zetu kwa haki yake (2 Wakorintho 5:21).
Kupitia toba na kukubali kifo cha Yesu kwa niaba yetu, tunaitwa watoto Wake (Yohana 1:12; Wagalatia 3:26). Mungu haoni tena kutokamilika kwetu; badala yake Anaona haki ya Mwanawe (Waefeso 2:13; Waebrania 8:12). Kwa sababu tuko ndani ya Kristo, Mungu anaona haki ya Kristo imetufunika. Ni kupitia “Kristo pekee” deni ya dhambi zetu imefutwa, uhusiano wetu na Mungu unarejeshwa, na umilele wetu kuulindwa (Yohana 3:16-18; 20:31).
Katika Kristo, Mungu ananiona kama kiumbe kipya: ”Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya” (2 Wakorintho 5:17). Tuna amani na Mungu na tunahesabika kuwa wenye haki mbele za Mungu (2 Wakorintho 5:17-21). Badala ya kuona dhambi zangu, Mungu anaona haki ya Mwanawe. Ananiona kuwa mwenye haki, aliyekombolewa, aliyetakaswa, hata aliyetukuzwa (ona Warumi 8:30).
Katika Waefeso 1:3-14 tunajifunza baadhi ya njia ambazo Mungu hutuona katika Kristo. Mungu “aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo” (Waefeso 1:3). Tumepewa kila kitu tunachohitaji. Tumechaguliwa tuwe “aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo” (Waefeso 1:4). Tunaonekana kuwa watakatifu na wasio na hatia kwa sababu tuko ndani ya Kristo (rejelea 2 Wakorintho 3:18).
Waefeso 1:5 inatuambia kwamba, katika Kristo tumechaguliwa tangu asili “alitangulia kutuchagua tuwe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo.” Hii inamaanisha kwamba Mungu ananiona kama mtoto Wake (ona pia Yohana 1:12-13). Hii ni kwa “kumsifu Mungu kwa huruma zake kuu alizotumiminia sisi katika Mwanawe Mpendwa” (Waefeso 1:6). Katika Kristo Mungu ananiona kwa upendo, na kunitunukia zawadi yake tele na “wingi wa neema yake” (Waefeso 1:7-8).
Mungu ananiona katika Kristo kama mrithi wa utele wa mbinguni (Waefeso 1:11; ona pia Warumi 8:17). Mungu ananiona kama mwana Wake milele. Amenitia muhuri kwa Roho Mtakatifu “akituhakikishia urithi wetu hadi ukombozi wa wale walio milki ya Mungu kwa sifa ya utukufu wake” (Waefeso 1:13-14).
Mungu ananiona kama kazi ya mikono yake (Zaburi 139:13b, 16; ona pia Waefeso 2:10); kama Rafiki yake (Yakobo 2:23); na kama mteule, “mtakatifu na mpendwa” (Wakolosai 3:12). Ananiona kuwa mwenye “amekufia dhambi” (Warumi 6:11) lakini “kufufuliwa pamoja na Kristo” (Wakolosai 3:1); kama hekalu la Roho Mtakatifu (1 Wakorintho 3:16); kama jiwe lilo hai na lililowekwa na Mjenzi Mkuu (1 Petro 2:5); kama sehemu ya “ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu walio milki ya Mungu” (1 Petro 2:9); na kama mmoja wa “wageni na wapita” katika ulimwengu (1 Petro 2:11). Mungu ananiona kama mmoja wa kondoo Wake: “kwa maana yeye ndiye Mungu wetu, na sisi ni watu wa malisho yake, kondoo chini ya utunzaji wake” (Zaburi 95:7).
English
Mungu ananionaje katika Kristo?