settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Mungu huruhusu kuzaliwa na ulemavu?

Jibu


Jibu la kipekee la swali hili gumu ni kwamba wakati Adam una Hawa walitenda dhambi (Mwanzo 3), walileta dhambi, maradhi, magonjwa na kifo duniani. Dhambi imekuwa ikisababisha madhara kwa kizazi cha binadamu tangu enzi hizo. Kuzaliwa na upungufu hutokea kwa sababu ya dhambi… sio kwa sababu ya dhambi za wazazi wametenda au mtoto, bali ni kwa sababu ya dhambi yenyewe. Sehemu ngumu ya swali ni, ni kwa Mungu huruhusu watu kuzaliwa na upungufu mbaya/ulemavu. Ni kwa nini Mungu asizuie upungufu wa kuzaliwa kutokea?

Kitabu cha Ayubu hushugulikia hali ambazo hatuelewi ni kwa nini Mungu huruhusu baadhi ya mambo kutokea. Mungu alimruhusu Shetani kufanya chochote alichotaka kwa Ayubu lakini asimuuwe. Ayubu aliitikiaje? "Tazama, ataniua; sina tumaini; ila hata hivyonitaithibitisha njia yangu mbele yake" (Ayubu 13:15), "Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe" (Ayubu 1:21). Ayubu hukuelewa ni kwa Mungu aliruhusu mambo ambayo aliruhusu yatendeke, lakini alifahamu Mungu alikuwa mwema na hivyo akaendelea kumtumainia. Hatimaye hivyo ndivyo tunapaswa kuitikia pia. Mungu ni mwema, mwenye haki, mpenzi, na mwenye huruma. Mara nyingi matukio hutukumba ambayo hatuyaelewi ni kwa nini. Badala ya kushuku wema wa Mungu, tunapaswa kumtumainia. "Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako."

Hatimaye, jibu kwa swali hili lazima liwe, "mimi sifahamu." Kwamwe hatutaweza kumwelewa Mung una njia zake kikamilifu. Itakuwa makossa kwetu kuswali ni kwa nini Mungu aliruhusu jambo Fulani kutokea. Lazima tuamini kuwa Mungu ni upendo, mwema na mwenye huruma-kama vile Ayubu alifanya- hata kama ushahidi ulionyesha tofauti. Maradhi na magonjwa yako kwa sababu ya dhambi. Mungu alipeana tiba ya dhambi kwa kumtuma Yesu Kristo kufa msalabani kwa ajili yetu (Warumi 5:8). Pindi tu tutafika mbinguni tutakuwa huru kutokana na maradhi, magonjwa na kifo. Hadi siku hiyo, lazima tukabiliane na dhambi, madhara na athari yake. Ijapokuwa tunaweza kumsifu Mungu kwamba atatumia upungufu wa kuzaliwa na majanga mengine kwa manufaa yet una kwa utukufu wake. Yohana 9:2-3 yasema, "Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake."

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Mungu huruhusu kuzaliwa na ulemavu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries