Swali
Je Mungu huzungumza nazi hii leo?
Jibu
Bibilia imenakili Mungu akizungumza kwa sauti kwa watu mara nyingi sana (Kutoka 3:14; Yoshua1:1; Waamuzi 6:18; 1Samweli 2:1; Ayubu 40:1; Isaya 7:3; Yeremia 1:7; Matendo ya Mitume 8:26; 9:15 hizi ni baadhi ya zile tulikusanya Mungu akizungumza kwa sauti na watu). Hakuna sababu yoyote ya kibibilia na ni kwa nini Mungu hataweza au hawezi kuzungumza na mtu hii leo. Pamoja na zaidi ya mara mia za sehemu ambazo Mungu ananena, lazima tukumbuke kwamba hii ilitokea katika kibindi cha miaka 4,000 ya historia ya mwanadamu. Mungu kunena na watu ni chaguo lake si sheria. Hata kwa matukio ya kibibilia ambayo yamenakiliwa Mungu akinena, haiko wazi kuwa kama alinena nao kwa sauti inayosikika au sauti ya ndani ama kupitia kwa picha ya kimawazo.
Mungu hunena na watu hata leo hii. Mungu hunena nasi kupitia kwa neno lake (2 Timotheo 3:16-17). Isaya 55: 11 yatuambia, “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.” Bibilia imeandika kila neno la Mungu, kila kitu tunachohitaji kujua ili tuokoke na kuishi maisha ya Kikristo. 2 Petero 1:3 yasema, “Kwa kuwa uweza wake wa uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.”
Pili, Mungu hunena kupitia mifano, matukio, na mawazo. Mungu hutusaidia kubainisha kati ya zuri na baya kupitia kwa hisia zetu (1 Timotheo 1:5; 1 Petero 3:16). Mungu ako katika harakati ya kuyabadilisha mawazo yetu kuwaza yaliyo yake (Warumi 12:2). Mungu hurusu matukio kutukia katika maisha yetu iliyatuongoze, yatubadilishe, na yatusaidie kukua kiroho (Yakobo 1:2-5; Waebrania 12:5-11). 1 Petero 1: 6-7 yatukumbusha, “Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; ili kwamba kujaribiwa kwa imai yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.”
Mwihso, Mungu wakati mwingine hunena kwa sauti na watu. Ingawa ni jambo kubwa la kushuku, kwamba hili hutokea kila mara vile watu wengine hudai. Pia, hata kwa Bibilia, Mungu kunena kwa sauti ni chaguo lake, si kawaida. Ikiwa mtu yeyote anadai kwamba Mungu amemnenea, kila mara linganisha chenye kimesemwa na chenye Bibilia inasema. Ikiwa Mungu alikuwa anene hii leo, neno Lake litakubaliana kikamilifu na chenye alisema katika Bibilia. (2 Timotheo 3:16-17). Mungu hajichanganyi mwenyewe.
English
Je Mungu huzungumza nazi hii leo?