settings icon
share icon
Swali

Mungu angeweza kuumba mwamba mzito sana ambao hangeweza kuuinua?

Jibu


Swali hili mara nyingu huulizwa na wasomi wachunguzi wa Mungu, Biblia, Ukristo na kadhalika. Ikiwa Mungu anaweza kuumba mwamba ambao hawezi kuuinua, basi Mungu si mwenye enzi yote. Ikiwa Mungu hangeweza kuumba mwamba mzito ambao hangeweza kuuinua basi Mungu sio mwenye enzi. Kulingina na maoni haya, uanaenzi unajikanganya wenyewe. Kwa hivyo, Mungu hawezi kuwa mwenye enzi. Basi, swali, Mungu angeweza kuumba mwamba mzito sana ambao hangeweza kuuinua? Jibu la hark ani "La." Lakini elezo ni la muhimu sana kuelewa kuliko jibu…

Swali hili lina misingi yake katika elezo maarufu sana ambalo halijaeleweka kuhusu neno kama "mwenyezi" au "mwenye enzi." Maneno haya hayamaanishi kuwa Mungu hawezi kufanya kitu. Badala yake, yanaelezea kiwango cha nguvu za Mungu. Nguvu ni uwezo wa kusababisha mabadiliko-kusababisha kitu kiwepo. Mungu (kutokuwa na mipaka) ana nguvu sisizo na mipaka, na Biblia inathibitisha hili (Ayubu 11:7-11, 37:23; 2 Wakorintho 6:18; Ufunuo 4:8; na kadhalika.). kwa hivyo Mungu anaweza kufanya chochote kinaweza kufanywa. Mungu hakika hawezi kufanya kile hakiwezekani. Hii ni kwa sababu kutowezekana ya kweli haiko juu ya kiwango cha nguvu mtu alizo nazo, misingi yake iko juu ya kile kiwezekanacho. Kile kisichowezekana kwa kweli hakiwezi ezekana kwa kuongezea nguvu zaidi. Kwa hivyo, ijapokuwa mkudhatha uonyeshe vingine (kwa mfano Mathayo 19:6 mahali uwezo wa binadamu umeonyeshwa kwa kulinganisha ule wa Mungu), lisilowezekana inamaanisha kitu kile kile hata kama Mungu amehusika au la.

Kwa hivyo, sehemu ya kwanza ya swali msingi wake uu katika dhana potovu-kwamba Mungu kuwa mwenye enzi inamaanisha kuwa hawezi kufanya chochote. Kwa kweli, Biblia yenyewe inataja mambo ambayo Mungu hawezi akafanya- kama vile uwongo au kujikana mwenyewe (Waebrania 6:18; 2 Timotheo 2:13; Tito 1:2). Sababu hawezi hakafanya mambo haya ni kwa sababu ya hali yake na hali ya uhalisi wa vitu. Mungu hawezi kufanya kile kisicho wezekana, kama vile kuumba mnara wa pande mbili au mkwasi na ameoa. Kwa sababu maneno hayawezi vutwa pamoja njia hii haifanyi lisilowezekana kuwezekana-mambo haya ni mkanganyo, katika uhalisia hayawezekani. Sasa, namna gani kuhusu mwamba huu? Mwamba ungelazimika uwe mkubwa sana ndio ushinde nguvu sisizo na mwisho. Lakini mwamba uliyo na mwisho ni mkanganyo sababu kile kinachoonekana hakiwezi kuwa cha milele. Ni Mungu pekee asiye na mipaka. Hakuwezi kuwa na vitu viwili visivyo na mwisho. Kwa hiyo swali hakika linauliza ikiwa Mungu anaweza sababisha mkanganyo-jambo ambalo hawezi lifanya.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mungu angeweza kuumba mwamba mzito sana ambao hangeweza kuuinua?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries