Swali
Je! Mungu husikia/hujibu maombi ya mwenye dhambi/asiyeamini?
Jibu
Yohana 9:31 inasema, “Tunajua kwamba Mungu hawasikilizi watu wenye dhambi. Yeye husikiliza mcha Mungu anayetimiza mapenzi yake.“ Na pia imesemekana kwamba “sala tu Mungu anasikia kutoka kwa mwenye dhambi ni sala kwa ajili ya wokovu.” Kwa madhumni hayo, , baadhi ya wengine huamini kuwa Mungu hawasikizi / au kamwe hajibu maombi ya asiyeamini. Kwa mkudhatha ingawa, Yohana 9:31 inasema kwamba Mungu hatendi miujiza kupitia kwa asiyeamini. Kwanza Yohana 5:14-15 inatuambia kwamba Mungu anajibu maombi kama yameombwa kwa mujibu wa mapenzi yake. Kanuni hii, labda, inatumika hata kwa makafiri. Kama kafiri anaomba maombi yanayoambatana na mapenzi yake, hakuna kitu kitakacho mzuia Mungu kujibu sala kama hizi, kulingana na mapenzi yake.
Baadhi ya maandiko yanaeleza kuwa Mungu anasikia na kujibu maombi ya makafiri. Katika kesi kama hizi, maombi yalihuzishwa. Katika mara moja au mbili, Mungu alijibu kilio cha moyo (haijaelezwa kama hicho kilio kilielekezwa kwa Mungu). Katika baadhi ya kesi hizi zingine, sala inaonekana kujumulishwa pamoja na toba. Lakini katika kesi zingine, sala ilikuwa kwa ajili ya mahitaji ya kidunia au baraka, na Mungu alijibu aidha kwa ajili ya huruma au kwa kukubaliana na ile imani ya kweli ya anayeomba. Hapa kuna baadhi ya vifungu vinavyoangazia maombi ya kafiri:
Watu wa Ninawi waliomba kwamba Mungu asiipitie Ninawi (Yona 3:5-10). Mungu alijibu maombi haya na hakuuharibu mji wa Ninawi kama alikuwa amewatishia.
Hajiri alimwomba Mungu amulinde mwanawe Ishmaeli (Mwanzo 21:14-19). Si kumkinga peke Mungu alimkinga Ishmael, pia Mungu alimbariki sana.
Katika 1 Wafalme 21:17-29, hasa mistari ya 27-29, Ahabu anafunga na kuomboleza juu ya unabii wa Elia juu ya wazawa wake. Mungu anajibu kwa kutoleta msiba wakati Ahabu.
Mwanamke wa Mataifa wa eneo la Tiro na Sidoni aliomba kwamba Yesu amkomboe bintiye kutokana na pepo (Mariko 7:24-30). Yesu alilitoa pepo nje ya binti wa mwanamke.
Konelio, Jemadari wa Kirumi katika Matendo 10, alipata Mtume Petro kutumwa kwake kwa misingi kwamba Konelio alikuwa mtu mwema. Matendo 10:2 inatuambia kwamba Konelio “aliomba kwa Mungu mara kwa mara”
Mungu huweka ahadi ambazo u huzisha wote (waliokolewa na wasiookoka sawia) kama vile Yeremia 29:13: “Mtanitafuta na kunipata mimi wakati mnanitafuta kwa moyo wako wote” Hii ilikuwa hali sawia na ya Konelio katika Matendo 10: 1-6). Lakini kuna ahadi nyingi, kulingana na mazingira ya vifungu hivi, na ni kwa Wakristo pekee. Kwa sababu Wakristo wamempokea Yesu kama mwokozi, wanatiwa moyo kusongea kwa ujasiri katika kiti cha neema ili wapate msaada wakati wa mahitaji (Waebrania 4:14-16). Tunaambiwa kwamba wakati tunapoombea jambo fulani sawasawa na mapenzi ya Mungu, Yeye husikia na kutupa tunachoomba (1 Yohana 5:14-15). Kuna ahadi zingine nyingi kwa ajili ya Wakristo kuhusu maombi (Mathayo 21:22; Yohana 14:13, 15:07). Kwa hiyo, naam, kuna matukio ambayo Mungu hajibu maombi ya kafiri. Wakati huo huo, katika neema na huruma zake, Mungu anaweza kuingilia kati katika maisha ya walio kufuru kwaniapa maombi yao.
English
Je! Mungu husikia/hujibu maombi ya mwenye dhambi/asiyeamini?