settings icon
share icon
Swali

Ikiwa Yesu alikuwa Mungu, ni kwa nini alisema 'hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake'?

Jibu


Mara nyingi husemekana na wale ambao hukataa uungo wa Kristo kuwa katika Marko 10:17-22 Yesu huukana uungu Wake kwa kukataa dhana kwamba yeye si mwema. Inasoma ifuatavyo:

"Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja alimjia mbio, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, "Mwalimu mwema, nifanyeje niupate uhai wa milele?" Yesu akamjibu, "Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake. Unazijua amri: 'Usizini, Usiue, Usiibe, Usitoe ushahidi wa uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.'" Naye akamjibu, "Mwalimu, hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu." Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia, "Umepungukiwa na kitu kimoja: Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho, uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha uje unifuate." Aliposikia hayo, alisikitika, akaenda zake akiwa na huzuni, kwa maana alikuwa na mali nyingi."

Yesu hapa anamkemea huyo mtu kwa kumwita mwema na hapo kukana Uungu wake? La. Badala yake, anatumia swali la msukumo kumlazimisha huyo mtu kufikiria madhara ya maneno yake, ili aelewe dhana ya wema wa Yesu na hasa vile huyo mtu hakuwa mwema. Huyo Tajiri "aliondoka akiwa amekasirika" (Marko 10:22) kwa sababu aligundua kwamba ingawa alikuwa amejitolea yeye mwenye kutunza amri, alikuwa ameanguka amri ya kwanza na kuu zaidi ya amri kumi- Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote (Mathayo 22:37-38). Utajiri wake ulikuwa wa maana sana kwake kuliko Mungu, na kwa hiyo hakuwa "mwema" machoni mwa Mungu.

Nguzo kuu ya fundisho la Yesu hapa ni kuwa wema wa mtu hautokani kwa matendo yake, bali toka kwa Mungu Mwenyewe. Yesu anamwalika Tajiri huyo amfuate, njia pekee ya kufanya mema katika kanuni za Mungu. Yesu anamweleza tajiri maana ya kumfuata Yeye-kuwa tayari kuacha vyote alivyonavyo, na kumweka Mungu kwanza. Wakati mtu anasingatia kuwa Yesu anaweka tofauti kati ya kanuni za mwandamu za wema na kanuni za Mungu, inakuwa wazi kuwa kumfuata Yesu ni bora. Amri ya kumfuata Kristo ndilo tangazo kuu la kipekee la wema wa Kristo. Hivyo, kwa kanuni hizo Yesu anamhimiza tajiri kumkubali Yesu ni bora. Na kwa umuhimu inafuata kuwa ikiwa Yesu ni mwema kwa kanuni hii, Yesu anatangaza wazi Uungu wake.

Basi swali la Yesu kwa tajari limeundwa kwa njia isiyokana uungu wake, bali kumfanya tajiri kutambua utambulisho wa Kristo na Uungu. Tafsiri kama hiyo imehimizwa na maakindo kama Yohana 10:11 ambapo Yesu anajitangaza Mwneyew kuwa "mchungaji mwema." Vile vile katika Yohana 8:46, Yesu anauliza, "Nani kati yenu awezaye kuthibitisha kuwa mimi nina dhambi?" ijapokuwa jibu ni "hakuna." Yesu "hakuwa na dhambi" (Waebrania 4:15), mtakatifu na asiyetiwa doha (Waebrania 7:26), yeye pekee ndiye hakujua "dhambi" (2 Wakorintho 5:21).

Elimu ya kuwaza kwa akili halisi inaweza weka kwa ufupi ifuatavyo:
1: Yesu anadai kuwa ni Mungu pekee ambaye ni mwema
2: Yesu anadai kuwa Yeye ni mwema
3: Kwa hivyo Yesu anadai kuwa Mungu

Madai kama hayo yanaleta maana nzuri kwa mktadha wa simulizi ya Marko pamoja na kufunuliwa kwa utambulisho halisi wa Yesu. Ni mbele ya kuhani mkuu tu katika Marko 14:62 kwamba swali la utambulisho wa Yesu umeelezwa kwa undani zaidi. Hadithi ya tajiri mtawala ni mojawapo katika msururo wa hadithi iliyotungwa kuelekeza wasomaji kwa Yesu kama Mwana wa Mungu wa milele, wa kiungu na aliyetwaa mwili wa nyama.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ikiwa Yesu alikuwa Mungu, ni kwa nini alisema 'hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake'?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries