settings icon
share icon
Swali

Mungu ni mkubwa aje?

Jibu


Swali "Mungu ni mkubwa kiasi gani?" hujibuka katika muktadha mseto wa aina mbili: majadiliano mazito ya kifalsafa na somo la watoto la jumapili. Jibu la swali la nyuma ambalo hutolewa ni "ni mkubwa zaidi ya utakavyo fikiria!" katika falsafa, hasa elimu ya kuchunguza asili ya kila kitu, swali la ukubwa wa Mungu linakadiriwa kuchukua mkondo wa mjadala wa hali halisi ya ukweli, kuwepo kwa kile kisicho cha ulimwengu kama vile wasomi wanaeza chekelea mtoto anayeuliza, "Mungu ni mkubwa kiasi gani?" lakini mtoto naye kwa urahisi anaweza mcheka mwanafalsafa kwa mkanganyo wake kuhusu uhalisi.

Katika kutatua swala la ukubwa wa Mungu, kwanza lazima tutaje kwamba Mungu hajaumbwa na "vitu vingine" kwa hivyo, hana ukadirio, na maelezo ya kujaza nafasi hayawezi tumika kwake. Mungu "hakuumbwa" lakini yuaishi milele, bila mwanzo wala mwisho (Ufunuo 22:13). Yeye anaishi na bile Yeye hamna kitu chochote kitakuwemo. Mungu anaishi kipekee na hategemei kiumbe chake chochote.

Mungu ni roho (Yohana 4:24) na kwa hiyo hana mwili au umbo la kuonekana. Hii sifa ya Mungu ni ngumu kwetu kuelewa. Tuko na roho ambayo imeunganishwa na mwili na kwa karibu sana imeshikanishwa na ulimwengu wa nyenzo. Kwa kawaida tunafikiria kwa namna ya upana, kina na urefu. Tunahisi kuwa ikiwa tunaweza kupima kitu kwa usitadi, tunaweza kukielewa vyema zaidi. Kwa hivyo tunafumbua chombo cha kukadiria, tunasungumza kwa namna ya upana, inchi, mete, maili, na mwaka. Lakini tunajiingiza katika shida wakati tunajaribu kumpima Mungu; tunagundua kwamba yeye hana mwili na kwa hivyo hawezi kupimika. Kwa kila njia Yeye hana mwisho. Mungu anakataa kumkadiria na hawezi nyenyekea jaribio letu la kumchunguza, kumuainisha, na kumtafusiri.

Mungu ni mkubwa kiasi gani? Ni mkubwa sana. Ni mkubwa zaidi, Mungu anapita nyakati zote; Yeye yuko hivyo namna ambayo hatuwezi kuielewa kikamilifu. Wakati huo huo, tumeumbwa kwa mfano wake, na anatupenda sana (Mwanzo 1:27; Yohana 3:16). Amesungumza nasi kupitia kwa neno lake na Mwanawe Yesu. Haijalishi ikiwa swali la ukubwa wa Mungu linatoka kwa mtoto wa shule ya Jumapili au kutoka kwa mwanafisikia, jibu lake huwa hili: Yeye ni "mkubwa" ya kutosha kuumba ulimwengu na "mdogo" ya kutosha kutujua na kutupenda.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mungu ni mkubwa aje?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries