Swali
Inaamanisha nini kuwa Mungu ni mwema?
Jibu
Yesu alitangaza, "Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake" (Luka 18:19). Yohana wa Kwanza 1:5 inatuambia kwamba "Mungu ni mwanga na hamna giza lolote ndani yake." Kusema kuwa Mungu ni mwema hiyo inamaanisha kuwa Mungu kila wakati hutenda kile kilicho cha haki, kweli, na chema. Wema ni sehemu asili ya Mungu, na hawezi kukanganya asili yake. Utakatifu na haki ni sehemu ya asili ya Mungu; hawezi kufanya chochote kisicho takatifu or haki. Mungu ndiye kiwango cha chochote kilicho chema.
Hoja kwamba Mungu ni mwema inamaanisha kwamba ndani yake hamna ubatili, nia yake na motisha kila mara huwa njema, huwa anafanya kilicho haki na matokeo ya mpango wake kila mara huwa mazuri (angali Mwanzo 50:20). Ndani ya hamna kisicho pendeza, ubatili, au giza. Biblia inafunza kwamba wema wa Mungu huchipuka kutoka asili yake hadi kwa kila kitu afacho (Zaburi 119:68). "Mwenyezi-Mungu ni mwema; fadhili zake zadumu milele, na uaminifu wake katika vizazi vyote" (Zaburi 100:5).
Kila kitu ambacho Mungu aliumba kilikuwa kizuri: "Mungu akaona kila kitu alichokifanya kuwa ni chema kabisa" (Mwanzo 1:31; cf 1Timotheo 4:4). Wema wa Mungu hujidhihirisha katika sheria alizowapa Waisraeli; amri ni takatifu, haki na njema (Warumi 7:12). "Kila kipaji chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni" (Yakobo 1:17). Mungu anaweza kuudna chenye ambacho ni chema, kwa sababu kikamilifu Yeye ni mwema.
Mungu hakuumba maovu (Habakuki 1:13; 1Yohana 1:5). Ile hali, uovu ni kukosekana kwa wema; ni chochote kile ambacho Mungu hana. Kwa sababu yaw ema wake, Mungu anachukia ubatili na ataihukumu siku moja (Warumi 2:5). Kamwe si mapenzi ya Mungu aliye mwema sisi kutenda dhambi: "Maana Mungu hawezi kujaribiwa na uovu, wala yeye hamjaribu mtu yeyote" (Yakobo 1:13).
Wema wa Mungu unafaa kutuongoza katika shukrani kwa upande wetu: "Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake zadumu milele" (Zaburi 107:1); cf 1Mambo ya Nyakati 16:34; Zaburi 118:1; 136). Ingawaje, watu wengi hawapendi kumfuata au kumshukuru Mungu. Badala yake, "watu wakapenda giza kuliko mwanga, kwani matendo yao ni maovu" (Yohana 3:19). Katika Agano la Kale, Waisraeli mara kwa mara walitaa amri nzuri za Mungu, wakasaau wema Wake kwao, na wakakosa kuwa waaminifu kwake: "Walisahau mambo aliyokuwa ametenda, miujiza aliyokuwa amewaonesha" (Zaburi 78:11).
Hatimaye, wema wa Mungu unadhihirika katika mpango wake wa kutukomboa kutoka dhambini. Injili ni "habari njema." Katika wama Wake, Mungu alimtuma mwanawe kuwa dhabihu kamili isiyo na lawama yeyote ili tupate kusamehewa dhambi zetu. Mungu hapendi "hata mmoja wenu apotee, bali huwavuta wote wapate kutubu" (2Petro 3:9), na ni "wema wake huo una shabaha ya kukuongoza upate kutubu" (Warumi 2:4).
Kunaye mmoja tu pekee ambaye ndiye mwema kamili-Mungu. Mungu aliye mwema anatualika tumtafute na "Jaribuni mwone Mwenyezi-Mungu alivyo mwema. Heri mtu anayekimbilia usalama kwake" (Zaburi 34:8).
English
Inaamanisha nini kuwa Mungu ni mwema?