Swali
Inamaanisha nini kuwa Mungu ni mwenye haki?
Jibu
Tunaposema kuwa Mungu ni mwadilifu, tunamaanisha kuwa Yeye kikamilifu ni mwenye haki jinsi anavyo tunza viumbe wake. Mungu haonyeshi mapendeleo (Matendo 10:34), anapinga dhuluma dhidi yaw engine (Zekaria 7:10), na kikamilifu yeye hulipisa kisasi kwa wale wanaodhulumu (2Wathesaloniki 1:6; Warumi 12:9). Mungu ni mwadilifu kwa kupeana dhawabu: "Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mliyoonesha kwa ajili yake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake" (Waebrania 6:10). Na vile vile Yeye sawia hutoa adhabu: "Atendaye mabaya atalipwa kufuatana na ubaya wake; Mungu hana ubaguzi" (Wakolosai 3:25). Uadilifu na haki, vyote hufanya kazi kwa pamoja mara kwa mara ndizo nguzo za kiti cha enzi cha Mungu (Zaburi 89:14).
Udilifu ni muhimu kwetu. Fikiria ikiwa Adolph Hitler angepatikana hai, akiwa amejificha nchini Ujerumani, na aletwe mbele ya hakimu. Makosa yake ya jinai yalichukua masaa tisa kuyasoma, lakini mwishowe hakimu akasema, "Nimeona chenye umefanya. Lakini nafikiria umejifunza mwenyewe na kwa hivyo nitakuachilia huru." Akagongesha nyundo ya uamuzi na kulia, "sina hatia!" ni nini huchibuka ndani ya mioyo yetu pindi tunapowaza hali kama hiyo? Hisia hiyo ni hasira kwa ukosefu wa haki. tunujua uamuzi huo sio wa haki, ni linaonekana jambo lisilo kubalika kwetu. Uovu unahitaji adhabu sawia. Tunarithi hisia ya haki kutoka kwa Muumbaji kwa sababu Yeye ni mwenye haki.
Kila kweli chini ya jua ni kweli ya Mungu. Kila mfumo wa hesabu, kila sheria ya kisayansi, kila mipaka ya uhusiano inapata miziai yake katika sifa ya Mungu. Ujuzi ya mwanadamu inafumbua ukweli ambao bado upo. Mungu ameficha sehemu za hekima katika anga ndio sisi tuzitafute. Haki ni mojawapo ya hizo kweli ambayo haina mwanzo wala elezo. Ikiwa sisi tulijibuka kutoka kitu chochote basi haki haiwezi kuwa na maana. Wanadamu hawawezi kuwa na haki, bila maadili ya kiutu, bila haja ya maisha ya milele. Lakini, kwa sababu tuliumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:27), tuko ma moyo kama wake kwa mambo kama, maadili, ujaziri, upendo, na haki. Yeye ndiye taswira kamili ya sehemu ya sifa tunazomiliki. Yeye ni upendo kamilifu (1Yohana 4:16). Yeye ni wema kamilifu (Zaburi 106:1). Yeye ni upole kamilifu (Zaburi 25:10). Na Yeye ni haki kamilifu (Isaya 61:8).
Adamu na Hawa walifanya dhambi (Mwanzo 3), haki haingeweza funga macho kwa hilo. Kosa lao halionekani kubwa sana kwetu. Lakini liangalie kutoka kwa mtazamo wa mbinguni. Mungu Mwenyezi Mkuu, mfalme wa kila kitu asiyepingwa, Bwana wa jeshi la malaika, anayestahili kuhimidiwa na kuabudiwa alikaidiwa na vumbi aliyoiunda na kuwa mtu. Aliumba kiumbe hiki kwa makusudi yake mwenyewe na furaha. Ulimwaga upendo tele kwao. Lakini pia aliwapa hiari huru. Aliifanya hivyo ndiposa waweze kuwa na uhusiano wa kweli Naye, kumaanisha wangeweza kuchagua kuenenda kinyume naye. Mungu aliwapa amri moja-msikule kutoka kwa mti mmoja kwenye bustani aliowaweka. Ikiwa walifanya hivyo wangekufa. Mungu aliwaonyesha chaguo waliokuwa nalo na akawaambia madhara yake.
Mungu kwa upendo wake aliwatunza viumbe wake na akawaonya kwa kile ambacho alijua kitatokea ikiwa hawangemtii. Lakini Adam una Hawa waliamua kuasi; walichagua njia zao dhidi za Mungu. Alidanganywa na Shetani na akafikiria pengine Mungu alikuwa anazuia bure, na hivyo akaamua kula lile tunda walikuwa wamekatazwa. Adamu kwa uepesi akalila lile tunda pia. Katika wakati huo viumbe wakafanya uasi dhidi ya Muumbaji. Haki huitaji hatua. Mungu kukosa kuadhibu au kusamehe uasi haitakuwa haki. Kwa sababu Mungu ni mwenye haki, hawezi fanya uamuzi, au kuweka adhabu, nab ado akose kuifuata wakati sharia hiyo imevunjwa. Kwa sababu Mungu pia ni upendo, alikuwa na njia ya kuridhisha haki bila kuangamiza wanadamu. Haki ilihitaji adhabu ya kifo kwa uasi mkuu, kwa hivyo kitu au mtu alifaa kufa. Njia mbadala ililetwa ili iridhishe matakwa ya haki. Mnyama asiye na hatia aliuwawa ili atoe dhama kwa Adam una Hawa, sio kwa minajili ya kuwafunika uchi wao, bali kwa dhambi zao pia (Mwanzo 3:21).
Maelfu ya miak baadaye, haki iliridhishwa mara moja na kwa niapa ya wote Mungu alipotuma Mwanawe kuwa dhamana yetu (2Wakorintho 5:21). Mungu kwa upendo ametuonya dhidi ya madhara ya dhambi katika vizazi vyote, akitusihi tusijitenge naye na kuenenda katika njia iendayo kuzumuni (Warumi 3:23). "tutafanya tupendavyo," hata hiyo tutakuwa tumeitikia. Mungu hawezi kosa kuangalia uasi wetu dhidi Yake, au hatakuwa mwadilifu kikamilifu. Kwa hivyo Yesu akawa kondoo (Yohana 1:29) ambayo Mungu alichinja madhabauni ya haki. Kristo "alikufa kwa ajili ya dhambi zenu; alikufa mara moja tu na ikatosha, mtu mwema kwa ajili ya waovu, ili awapeleke nyinyi kwa Mungu" (1Petro 3:18).
Kwa sababu haki imeridhishwa, Mungu ametangaza "hamna hatia" kwa wale wote ambao wako ndani ya Kristo (Warumi 3:24), wale wanaoliita jina lake (Yohana 1:12). Haki sasa inasisitiza kwamba, pindi dhambi ishalipiwa haiwezi fufuliwa tena. Wakati dhambi zatu ziko chini ya damu Yake ya dhamana, Mungu hatuesabii hizo dhambi tena (Warumi 8:1; Wakolosai 2:14; 1Petro 2:24; Isaya 43:25). Mungu anabaki kuwa mwadilifu, hawezi kaidi amri zake mwenyewe za uadilifu kwa kuwasamehe wale wanaostahili adhabu yake. Wokovu ni matokeo ya haki kwa sababu Mungu ametangaza kufa na kufufuka kwa Yesu kuwa vyatosha kuridhisha ghadhabu Yake. Laana ya sheria ambayo tuliistahili kwa haki imeondolewa na Yesu msalabani (Wagalatia 3:13).
Mungu ni mwenya haki, na haki yake ni sehemu murwa ya sifa yake sawa na vile upendo wake na huruma vilivyo shikamana. Bila haki yake, dhambi itaendelea bila kuadhibiwa. Uovu utatawala. Hakutakuwa na dhawabu ya utiivu. Hatutamweshimu Mungu ambaye si wa haki. Mika 6:8 inafupisha sifa tatu kuu ambazo Mungu anatakusiona ndani yetu: Mungu amekuonesha yaliyo mema, ewe mtu; anachotaka Mwenyezi-Mungu kwako ni hiki:
Kutenda mambo ya haki, kupenda kuwa na huruma, na kuishi kwa unyenyekevu na Mungu wako."
English
Inamaanisha nini kuwa Mungu ni mwenye haki?