Swali
Ikiwa Mungu ni upendo, ni kwa nini analaani ushoga?
Jibu
hoja inayojulikana na wengi ya kukubali ushoga na ndoa ya jinsia moja ni kwamba, ikiwa Mungu ni upendo, asingehukumu upendo wa wengine. Tatizo kuu na hili ni aina ya “upendo” tunayozungumzia.
Waraka wa kwanza wa Yohana 4:8 wasema, “Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni pendo.” “Upendo” unaorejelewa hapa ni agape ya Kigiriki. Aina hii ya upendo ni tendo la fahamu la kujitolea mhanga matamanio ya mtu mwenyewe, faraja, na hata ustawi kwa ajili ya mwingine. Ni upendo uliomtuma Yesu kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu (Warumi 5:8). Na ni upendo uliomfanya Mungu amtume (Yohana 3:16). Utimilifu mkuu wa upendo huu ni kutoa maisha ya mtu kwa ajili ya mwingine (Yohana 15:13).
Basi swali linakuwa ni, ni nini kinachojumuisha ustawi wa mtu mwingine? Ulimwengu na labda hata hisia zetu wenyewe zinaweza kusema kwamba kuruhusu mtu mwingine kuishi katika uhusiano wa ushoga ni kuona ustawi wao. Biblia inasema tofauti. Warumi 1:26 inasema ni aibu na fedheha. Wakorintho wa kwanza 6:9 inasema kwamba itamweka mtu mbali na ufalme wa Mungu. Wakorintho wa Kwanza 6:18 inasema kwamba tabia ya ushoga ni dhambi dhidi ya mwili wa mtu mwenyewe.
Ikiwa hii ni kweli na tabia ya ushoga ni aibu, kujitenga na baraka za Mungu, na kujidhuru, basi jambo la upendo la kufanya ni kukaa mbali nayo. Kuwatia moyo wengine kujiingiza katika dhambi ni kuwaita moyo kukataa baraka za Mungu maishani mwao. Ni kinyume cha upendo.
Baada ya hayo kusemwa, wale wanaovutiwa na ushoga wanahitaji sana upendo. Hata kama wanakubaliana na Biblia kwamba ushoga ni dhambi na kuazimia kutotafuta kutimiza tamaa zao za ngono, bado lazima wapate upendo katika mahusiano mengine-upendo wa kujitoa kama dhabihu wa agape na ushirikiano wa kirafiki fileo (phileo). Wakati mahitaji yetu ya kihisia na kijamii ya upendo yanapotimizwa kuna uwezekano mdogo wa kutafuta utimizo kwa njia zisizo za kibiblia. Sio tofauti kwa wapenzi wa jinsia tofauti kuliko wale walio na mvuto wa ushoga.
Je! mtu aliye na mvuto wa ngono na mtu wa jinsia yake anaweza kuponywa na kuvutiwa na jinsia tofauti katika mawazo, hamu na matendo? Inawezekana, lakini haina uhakika. Kuokoka na kusamehewa hakuondoi mtu kutoka kwa majaribu. Kwa muumini, maadamu mvuto wa watu wa jinsia moja upo, kujizuia na kwa muhimu-kama vile ilivyo kwa mtu yeyote ambaye hayuko katika ndoa ya jinsia tofauti. Waumini hawapaswi kuunga mkono uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa ya watu wa jinsia tofauti hata kama hao wawili wanaonyesha upendo wa agape na fileo.
Ni uongo kwamba wanadamu wote wanahitaji utimilifu wa kingono (Mathayo 19:12). Ni uongo kwamba ngono ni sawa na upendo. Mungu aliyetuumba anasisitiza kwamba ngono ni dhihirisho la upendo kati ya mume na mke ambao wameoana. Nje ya muktadha huo, ngono ni hatari na haina upendo. Ikiwa tunawapenda wengine, hatutawatia moyo kutenda dhambi, na kujilietea madhara. Badala yake tutafuata amri kuu zaidi na kuwapa upendo wa kweli wanaohitaji kutoka kwetu.
English
Ikiwa Mungu ni upendo, ni kwa nini analaani ushoga?