settings icon
share icon
Swali

Inaamanisha nini kuwa Mungu yuko pamoja nasi?

Jibu


Ni muhimu kujua kwamba Mungu yuko kila mahali-ni mojawapo ya sifa zake. Inayoambatana na kuwa kila mahali ni sifa ya kujua yote na sifa ya mamlaka yote. Dhana hizi ni tata kidogo kwetu sisi wanadamu kuzifahamu vyema, lakini Mungu anajua hali pia (Isaya 55:8). Mungu hujaza uumbaji wake na Yeye mwenye yuko kila mahali, katika ufahamu na mamlaka nyakati zote. "Mungu hayuko mbali na kila mmoja wetu" (Matendo 17:27).

Kwa njia ya moja kwa moja zaidi, Mungu yuko na waumini wote hii leo kwamba Roho wake Mtakatifu hutujaza. Ujazo huu unaweza fanyika ikiwa mtu amezaliwa mara ya pili (Yohana 3:3). Katika Mathayo 28:20 Yesu aliwahidi mitume wake, "Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati." Yesu pia alisema kwamba Baba anakuja na kuishi nasi: "Mtu akinipenda atashika neno langu, na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kukaa naye" (Yohana 14:23).

Katika Wagalatia 2:20 Paulo anasema, "Kristo anaishi dhani yangu." Pia katika Wagalatia 3:5 anasema kwamba Mungu ametupa Roho Wake. Katika Wagalatia 3:26-27, anasema kuwa waumini "wamebatizwa katika Kristo" na "wamemfika" Kristo. (Mungu yuko karibu kama vile nguo zetu za mwili!) Wagalatia 5 pia inaelezea tunda la Roho na kutaja katika aya ya 25, "Tukiishi kwa msaada wa Roho, na tuufuate mwongozo wake." Mungu katika nafsi zote tatu za Utatu yuko na waliokolewa kila wakati.

mojawapo ya majina ya Yesu ni "Imanueli," ambayo inamaanisha "Mungu pamoja nasi" (Mathayo 1:23). Wakati Yesu alikuja katika ulimwengu huu, kwa kweli kihalisi ni "Mungu pamoja nasi." Kwa sababu Mungu yuko pamoja nasi, tunajua kwamba kamwe hatutawai tenganishwa na upendo wake (Warumi 8:38-39). Uepo wa Mungu unatuakikishia kwamba tunaweza kukamilisha mapenzi yake kwetu (Mambo Ya Nyakati 22:17-19). Uepo wa Mungu unapita hofu yetu, woga, na kutoridhika (Waebrania 13:5).

Roho Mtakatifu ndani yetu kila mara anatuombea (Warumi 8:26). Tunaambiwa tuombe bila kukoma (1Wathesaloniki 5:17), kumaanisha tunapaswa kudumisha nia ya maombi na mtazamo ili tusungumze maombi kwa Mungu wakati yu aongoza. Yeye yu karibu na Watoto wake, anakisikia kilio chao (Zaburi 34:15).

Tunapaswa kuhakikisha kuwa kwa kweli tunatembea na Bwana wetu Mungu kwa ushauri wa Neno lake, ushirika na waumini wengine, na kutafuta ushauri wa kiroho kutoka kwa wachungaji, na Wakristo marafiki. Lazima tuwe na nia kuwa wakati wote tuko katika huduma na Bwana. Roho Mtakatifu atatuongoza. Tutamwona Mungu akifanya kazi. Mungu yu hai, na yuko karibu. Anataka kusungumza na kushiriki nasi. Hiyo ndiyo furaha ya maisha ya Kikristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Inaamanisha nini kuwa Mungu yuko pamoja nasi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries