Swali
Nadharia mbalimbali juu ya upatanisho ndio gani?
Jibu
Katika historia ya kanisa, maoni mbalimbali ya upatanisho, baadhi yao ni kweli na baadhi yao ni uongo, yamewekwa mbele na watu tofauti au madhehebu . Mojawapo ya sababu za maoni mbalimbali ni kwamba zote Agano la Kale na Jipya zafunua kweli nyingi juu ya upatanisho wa Kristo, na kuifanya ngumu, kama siyo haiwezekani, kupata "nadharia" yoyote ile moja kwamba kikamilifu inasingatia au inaelezea utajiri wa upatanisho. Chenyesisi hugundua tunaposoma maandiko ni picha tajiri na yenye sura mbili ya upatanisho kama vile Biblia inavyochanua kweli nyingi zinazohusiana ukombozi ambao Kristo ametimizza. Sababu nyingine inayochangia kwa nadharia mbalimbali ya upatanisho ni kwamba sehemu kubwa ya kile tunachoweza kujifunza juu ya upatanisho kinahitaji kueleweka kutokana na uzoefu na mtazamo wa watu wa Mungu chini ya Agano la Kale katika mfumo wa sadaka.
Upatanisho wa Kristo, kusudi lake na kile ulitimiza, ni somo tajiri kiasi nakala zimeandikwa juu yake. Nakala hii itakuwa tu ya kutoa muhtasari wa nyingi za nadharia ambazo zimekwisha wekwa mbele kwa wakati mmoja au mwingine. Kwa kuangalia maoni tofauti ya upatanisho, tunapaswa kukumbuka kwamba maoni yoyote ambayo haitambui hali ya dhambi ya mwanadamu au asili badala ya upatanisho ni ya upungufu na ni uzushi mbaya sana.
Fidia kwa Shetani: Mtazamo huu unaona upatanisho wa Kristo kama fidia iliyolipwa kwa shetani, ili inunue uhuru wa mwanadamu na kumtoa kutoka kuwa mtumwa wa Shetani. Ni kwa kuzingatia imani kwamba hali ya kiroho ya mwanadamu ni mtumwa wa Shetani na kwamba maana ya kifo cha Kristo kilikuwa kupata ushindi wa Mungu juu ya Shetani. Nadharia hii ina kidogo , kama upo, uungwaji wa maandiko na umekuwa na wafuasi wachache katika historia ya kanisa. Sio kibiblia kwamba inaona Shetani badala ya Mungu, kama ambaye alihitaji malipo kufanywa kwa ajili ya dhambi. Hivyo, kabisa huacha mahitaji ya haki ya Mungu kama inavyoonekana katika maandiko. Pia una mtazamo wa juu kwa Shetani aaidi ya unavyostahili na kumwona kuwa na nguvu zaidi ya zile anazo. Hakuna uungwaji wa maandiko kwa wazo kwamba wenye dhambi wana deni kwa Shetani, lakini katika maandiko tunaona kwamba Mungu ni mmoja ambaye anahitaji malipo kwa ajili ya dhambi.
fikira mpya ya nadharia: Nadharia hii inasema kwamba upatanisho wa Kristo umebadilisha mtindo wa watu kutoka uasi hadi utii. Ni imani kuwa maisha ya Kristo yafanya upya hatua zote za maisha ya binadamu na katika kufanya hivyo kukadilisha hatua za uasi mwanadamu zilizoanzishwa na Adam. Nadharia hii haiungwi na kimaandiko.
Nadharia ya uigizo: Mtazamo huu unaona upatanisho wa Kristo kama ushindi dhidi ya vita ya mema na mabaya na kumshindia mwanadamu ukombozi kutoka katika utumwa wa Shetani. Maana ya kifo cha Kristo ni kuhakikishia ushindi wa Mungu dhidi ya Shetani na kutoa njia ya kukomboa ulimwengu kutoka kwa utumwa wake kwa uovu.
Nadharia fumbo: Nadharia fumbo inaona upatanisho wa Kristo kama ushindi dhidi ya dhambi yake mwenyewe ya asili kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Wale wanaoshikilia mtazamo huu huamini kwamba elimu ya hili kifumbo itashawishi mwanadamu na kuamsha " fahamu ya kiungu." Pia wanaamini hali ya kiroho mwanadamu sio matokeo ya dhambi lakini kukosekana kwa " fahamu -mungu." Ni wazi, hii ni ya kibiblia. Kuamini hili, mtu ni lazima aamini kwamba Kristo alikuwa na asili ya dhambi, huku maandiko yakiwa wazi kuwa Yesu alikuwa kikamilifu mwanadamu na Mungu, bila dhambi katika kila nyanja ya mwili wake ( Waebrania 4:15).
Nadharia ya maadili -shawishi: Hii ni imani kwamba upatanisho wa Kristo ni dhihirisho la upendo wa Mungu ambao husababisha moyo wa mwanadamu kuyeyuka na kutubu. Wale wanaoshikilia mtazamo huu huamini kuwa mwanadamu ni mgonjwa kiroho na anahitaji msaada na mwanadamu anavutiwa na kuukubali msamaha wa Mungu kwa kuona upendo wa Mungu kwa mwanadamu. Wanaamini kwamba kusudi na maana ya kifo cha Kristo, ilikuwa kudhihirisha upendo wa Mungu kwa binadamu. Huku kukiwa ni kweli kwamba upatanisho wa Kristo ni mfano wa mwisho wa upendo wa Mungu, mtazamo huu ni wa kibiblia kwa sababu unakanusha hali halisi ya kiroho ya mtu kufa kwa sababu ya makosa na dhambi (Waefeso 2:1) - na unakanusha kuwa Mungu kweli ahitaji malipo kwa ajili ya dhambi. Mtazamo huu wa upatanisho wa Kristo wamwaacha mwanadamu bila sadaka ya kweli au malipo kwa ajili ya dhambi.
Nadharia Mfano: Mtazamo huu unaona upatanisho wa Kristo kama wa kutoa mfano wa imani na utiifu wa kuhamasisha mwanadamu kuwa mtiifu kwa Mungu. Wale wanaoshikilia mtazamo huu huamini kwamba mtu yu hai kiroho na kwamba maisha ya Kristo na upatanisho ulikuwa tu mfano wa imani ya kweli na utii na unapaswa kutumika kama msukumo kwa wanadamu kuishi maisha sawia ya imani na utii. Mtazamo huu na ule wa nadharia maadili ushawishi ni sawia kwa kuwa hiyo yote hukana kwamba kwa kweli haki ya Mungu ahitaji malipo kwa ajili ya dhambi na kwamba kifo cha Kristo msalabani kilikuwa ni malipo hayo. Tofauti kubwa kati ya nadharia maadili-shawishi na nadharia mfano ni kwamba nadharia maadili-shawishi inasema kuwa kifo cha Kristo hutufundisha jinsi gani Mungu anatupenda na nadharia mfano inasema kuwa kifo cha Kristo huwafundisha jinsi ya kuishi. Bila shaka, ni kweli kwamba Kristo ni mfano kwetu sisi kufuata, hata katika kifo chake, lakini nadharia mfano unashindwa kutambua hali ya mwanadamu ya kweli kiroho na kwamba haki ya Mungu inahitaji malipo kwa ajili ya dhambi ambayo mwanadamu hana uwezo wa kulipia.
Nadharia ya kibiashara: Nadharia ya kibiashara watizama upatanisho wa Kristo kama wa kuleta heshima isio na mwisho kwa Mungu. Hii ilimsababisha Mungu kumpa Kristo malipo ambayo hakuhitaji, na Kristo akapitisha ujira huo kwa mwanadamu. Wale wanaoshikilia mtazamo huu huamini kwamba hali ya kiroho ya mwanadamu ni ile ya kutomtii Mungu na hivyo kifo cha Kristo, ambacho kilimletea Mungu heshima isiyo na mwisho, chaweza tumika kwa wenye dhambi kwa ajili ya wokovu. Nadharia hii, kama zingine nyingi, imekanusha hali ya kweli ya kiroho kwa watu wenye dhambi wasi hawajazaliwa mara ya pili na mahitaji yao ya asili mpya kabisa, ipatikanayo tu katika Kristo (2 Wakorintho 5:17).
Nadharia ya Kiserikali: Mtazamo huu unaona upatanisho wa Kristo kamaule uonyeshao heshima ya juu ya Mungu kwa sheria yake na mtazamo wake kwa dhambi. Ni kwa njia ya kifo cha Kristo kwamba Mungu ana sababu ya kusamehe dhambi za wale walio tubu na kukubali kifo cha Kristo kuwa fidia ya dhambi. Wale wanaoshikilia mtazamo huu huamini kwamba hali ya kiroho ya mwanadamu ni kama ya mtu ambaye amevunja sheria ya Mungu ya maadili na kwamba maana ya kifo cha Kristo kilikuwa mbadala kwa ajili ya adhabu ya dhambi. Kwa sababu Kristo alilipa fidia ya dhambi, inawezekana kwa Mungu kisheria kusamehe wale wanaokubali Kristo kama mbadala wao. Mtazamo huu umepungukiwa kwa kuwa hauna mafundisho kwamba kwa kweli Kristo alilipa adhabu ya dhambi halisi ya watu wowote, lakini badala yake mateso yake yalionyesha watu kwamba sheria ya Mungu ilivunjwa na kwamba baadhi ya adhabu hiyo kulipiwa.
Nadharia ya Adhabu badala: Nadharia hii inaona upatanisho wa Kristo kama uwakilishi, sadaka badala ambayo huridhisha mahitaji ya haki ya Mungu juu ya dhambi. Na sadaka yake, Kristo alilipa adhabu ya dhambi ya mwanadamu, na kuleta msamaha, na kuwahesabia haki, na kumpatanisha mwanadamu na Mungu. Wale wanaoshikilia mtazamo huu huamini kwamba kila nyanja ya mwanadamu mawazo yake, mapenzi, na hisia- zimekuwa za kupotoshwa na dhambi na kwamba mwanadamu kabisa amepotea na kufa kiroho. Mtazamo huuu unashikilia kuwa kifo cha Kristo kililipa fidia ya dhambi na kwamba kwa njia ya imani mwanadamu anaweza kukubali badala ya Kristo kama malipo kwa ajili ya dhambi. Mtazamo huu wa upatanisho wafungamana kwa usahihi zaidi na maandiko katika mtazamo wake wa dhambi, asili ya mwanadamu, na matokeo ya kifo cha Kristo juu ya msalaba.
English
Nadharia mbalimbali juu ya upatanisho ndio gani?