settings icon
share icon
Swali

Je, nafsi ya binadamu hufa au ni ya milele?

Jibu


Bila shaka nafsi ya binadamu ni ya milele. Hii inaonekana wazi katika maandiko mengi katika Agano la Kale na Jipya: Zaburi 22:26; 23:6; 49:7-9, Mhubiri 12:7; Danieli 12:2-3; Mathayo 25:46; na 1 Wakorintho 15:12-19. Danieli 12:2 anasema, "Tena wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka. Wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele" Vile vile, Yesu mwenyewe alisema kwamba waovu "Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele, bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele" (Mathayo 25:46). Kwa neno la Kigiriki hutumiwa kwa kurejelea zote "adhabu" na "uhai," ni wazi kwamba waovu na wema wana nafsi ya milele / nafsi ikufayo.

Mafundisho ya Biblia yasio na makosa ni kwamba watu wote, hata kama wameokolewa au wamepotea, kuwepo milele, aidha katika mbinguni au kuzimuni. Maisha ya kweli au maisha ya kiroho hayakomi wakati miili yetu ya kimwili hupita katika kifo. Nafsi zetu zitaishi milele, ama katika uwepo wa Mungu mbinguni kama sisi tutaokolewa, au katika adhabu kuzimuni kama sisi tutaikataa zawadi ya Mungu ya wokovu. Kwa kweli, ahadi ya Biblia ni kwamba sio tu nafsi zetu zitaishi milele, bali pia miili yetu itafufuliwa. Matumaini haya ya ufufuo wa mwili yako ndani ya moyo wa imani ya Kikristo (1 Wakorintho 15:12-19).

Huku nafsi zote zitaishi milele, ni muhimu kukumbuka kwamba sisi hatuko hali ile ile Mungu milele atakuwa. Mungu ndiye kiumbe cha kweli milele kwamba Yeye peke ndiye hana mwanzo wala mwisho. Mungu amekuwepo na daima ataendelea kuwepo. Viumbe wengine wote ni wa muda, hata kama wao ni binadamu au malaika, wana mwisho kwamba walikuwa mwanzo. Huku nafsi zetu zikiishi milele mara tu sisi huwa, Biblia haiungi dhana kwamba nafsi zetu daima huwepo. Nafsi zetu ni za milele, hinvyo ndivyo Mungu aliziumba, lakini zilikuwa na mwanzo; kulikuwa na wakati hazikuwepo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, nafsi ya binadamu hufa au ni ya milele?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries