Swali
Nani alimuumba Mungu? Mungu alitoka wapi?
Jibu
Wazo la pamoja la wasiomwamini Mungu na wanaomshuku Mungu, ni kama vitu vyote vinaitaji mwanzo, kwa hivyo Mungu lazima ahitaji mwanzo. Kaauli yao ni Mungu anaitaji mwanzo, kwa hivyo Mungu si Mungu (na kama Mungu si Mungu, kwa hivyo hakuna Mungu). Hii ndio njia ya kutatanisha sana kwa swali la namna hii “Nani alimuumba Mungu?” kila mmoja anajua kuwa hakuna kitu kinaweza kutoka mahali wazi. Kwa hivyo kama Mungu ni “kitu” kwa hivyo lazima awe na aliye muumba, kweli?
Swali hili latatanisha kwa sababu linaingiza dhana ya kupotosha ya kuwa Mungu alitoka mahali na kuuliza, mahali hapo panaweza kuwa wapi. Jibu kwa swali hili halina maana. Ni sawa na kuuliza, “Rangi ya samawati huwa na harufu gani?” Samawati si kikundi cha harufu, kwa hivyo swali limekuwa na dosari. Vile vile Mungu hayuko kwa kikundi cha vitu vilivyoumbwa ama kutengezwa. Mungu hawezi kuumbwa au kutengezwa, huwa anaishi.
Tunawezaje kujua haya? Tunajua kutoka uwazi, hakutoki kitu. Kwa hivyo kama kulikuwa na wakati hakukuwa na kitu chochote ulimwenguni, kwa hivyo hakungekuwa na kitu chochote ulimwenguni. Lakini vitu huwepo. Kati ya vyote kinachodumu ni Mungu. Mungu ni kitu kisicho tengenezwa ambacho kilifanya vyote viwepo. Mungu hawezi kuumbika ambaye ndiye muumbaji wa ulimwengu na vyote vilivyomo.
English
Nani alimuumba Mungu? Mungu alitoka wapi?