Swali
Mkristo anapaswa kuitikiaje kwa kuwa katika ndoa isiyo na upendo?
Jibu
Neno ndoa isiyo na upendo linaweza kuelezea hali kadhaa, kuanzia kupoteza hisia za awali za upendo hadi uzoefu wa unyanyasaji wa kijeuri. (Katika kesi ya unyanyasaji wa mume na mke, mwenzi aliyenyanyaswa anapaswa kutafuta usaidizi kupitia njia za kisheria na msaada kihisia. Kujiondoa kutoka kwa hali hiyo mara nyingi ni muhimu wakati usharui unaendelea kufanyaka. Mwenzi aliyedhulimiwa hapaswi kamwe kuanza tena kuishi katika nyumba moja na huyu mnyanyasaji wa zamani. Mnyanyasaji ambaye hajathibitisha kwamba anaweza kuaminika.) Kwa madhumini ya makala hii, tutafafanua ndoa isiyo na upendo kuwa ndoa ambayo haina unyanyasaji wa kimwili unaofanywa lakini ambayo mmoja wa wanandoa au wote wawili wamepoteza upendo kwa kila mmoja wao na wanaishi kama wakazi-wenza.
Mpango wa Mungu wa ndoa ulifunuliwa katika bustani ya Edeni wakati Mungu alipomuumba mwanamke kwa ajili ya Adamu na kumleta kwake kama msaidizi (Mwanzo 2:21-24). Neno linalotafsiriwa “msaidizi” linatokana na neno la Kiebrania ambalo pia hutumiwa kueleza msaada ambao Mungu hutoa (Kutoka 18:4; Kumbukumbu 33:26; Zaburi 33:20). Kwa hiyo wajibu mke aliopewa na Mungu ni kumsaidia mume wake katika kazi ambayo Mungu amempa na kumuunga mkono, hekima, kumtia moyo, na nyakati nyingine ukombozi kama vile Mungu anavyotupa. Jukumu la mume limewekwa wazi katika Waefeso 5:25-33. Kumpenda mke wake si pendekezo kwa mume; ni amri. Mume yeyote ambaye hajitahidi kuonyesha upendo usio na ubinafsi, kama wa Kristo kwa mke wake, anakosa kutii Neno la Mungu moja kwa moja. Ikiwa mume atashindwa kufanya hivi, maombi yake yatazuiliwa (1 Petro 3:7).
Wakati mwingine ndoa isiyo na upendo ni matokeo ya kufungwa nira mpamoja na asiyeamini (ona 2 Wakorintho 6:14). Mwenzi asiyeamini hakuweza kujali kidogo kuhusu utiifu kwa Neno la Mungu. Katika visa hivyo, mtume Paulo anatoa maagizo: ikiwa mwenzi asiyeamini anakubali kubaki katika ndoa isiyo na vurugu, Mkristo anapaswa kubaki na kuonyesha upendo wa Kristo (1 Wakorintho 7: 12-16). Tunda la kwanza la Roho Mtakatifu lililoorodheshwa katika Wagalatia 5:22-23 ni upendo. Wakati hatuna upendo wa kibinadamu wa kutoa, tunaweza kumwita Bwana na kumwomba Roho Mtakatifu ampende mwenzi kupitia sisi. Ni jambo la shaka kwamba Yesu alihisi upendo mchangamfu, wa kihisia kwa wanaaume waliokuwa wakimpigilia misumari msalabani. Hata hivyo Alimwomba Baba awasamehe, na hata hivyo Alikufa kwa ajili yao (Luka 23:33-34; Warumi 5:8). Onyesho la Yesu la upendo linaweza kuwa msukumo kwetu sote, hata kuhusiana na ndoa zetu.
Ikiwa ushauri unapatikana, ndoa zisizo na upendo zinaweza kufaidika kutokana na mtazamo wa hekima na usiofaa wa mshauri wa biblia (Mithali 11:14: 15:22). Wakati mwingine ndoa inaweza kuharibika kwa ajili ya kutekelezwa na kukuwepo na tabia ya kutojali ambazo huenda wanandoa hawazijui. Mtazamo wa mtu mwingine unaweza kuwasaidia kuona haraka maeneo ya shida na hitaji la kusuluhisha. Ikiwa wanandoa wako tayari kufanya kazi, ndoa isiyo na upendo inaweza kurejeshwa kwa upendo kwa haraka. Hata kama mwenzi mmoja anakataa kushirikiana na ushauri, mwenzi aliye tayari anaweza kufaidika kwa kwenda peke yake. Maoni yenye kusudi nyakati fulani yanaweza kumsaidia mwenzi mmoja kuona mambo kwa njia tofauti na hivyo kumjibu kwa njia bora mwenzi asiye na upendo.
Kama jiwe linalotupwa kwenye kidimbwi, mabadiliko yanayowekwa katika mazoea yasiyo mazuri hutengeneza mifumo mipya ya majibu. Hapa kunacho kielelezo cha jinsi mwenzi mmoja wa ndoa anavyoweza kubadili mwendo wa ndoa isiyo na upendo: ikiwa Sue hatamfokea tena John wakati yeye ni mfidhuli, ni lazima aitikie jibu lake la upole kwa njia tofauti na vile amaekuwa akifanya hapo awali. Badala ya kupandisha hasira, anapunguza tabia yake ya kihuni ili kuambatana na mtazamo wake uliokomaa. Tabasamu lake la utulivu na kukataa kujihusisha kunaonyesha ubinafsi wake mweneywe, na mara nyingi hujibu kwa uhasama mdogo. Mzunguko wa mapambano unakatizwa, na mzunguko mpya huanza na mkazo mdogo na wema zaidi (Mithali 15:1). Baada ya muda, mzunguko huo mpya ulio mzuri unaweza kubadilika na kuwa mapenzi, na wanandoa kujifunza kufurahiana tena.
Kuna mambo kadhaa ambayo Mkristo anaweza kufanya ili kuwekeza tena katika ndoa isiyo na upendo:
1. Weka mipaka mizuri. Jifunze wakati wa kuondoka, kujitenga, au kukataa maneno au mifumo yenye kuumiza. Kukataa kushiriki katika mapigano ambayo hayaelekei popote ni njia mojawapo ya kuimarisha ndoa.
2. Ombeana. Njia bora ya kusamehe na kumpenda mtu ambaye ametuumiza ni kumwinua mbele za Mungu (Waefeso 4:32). Mungu ako na nia nzuri kwa ndoa, kwa hiyo tunajua tunaomba kulingana na mapenzi Yake tunapoomba urejesho wa upendo na tumaini (1 Yohana 5: 14-15).
3. Chunga maneno yako. Huwa tunaamini kile tunachozungumza. Ikiwa tunajikuta mara kwa mara tukimtukana mwenzi wetu au kulalamika kuhusu ndoa, tutaanza kuamini. Hekima inatuamuru tujizoeze kudhibiti ndimi zetu na kunena yale tu ambayo ni “kweli, na sifa njema, na haki, na safi, yoyote ya kupendeza, staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa” (Wafilipi 4:8).
4. Kuwa mwangalifu kwa mambo madogo. Wanandoa wanapopendana kwa mara ya kwanza, wanagundua mambo machache kwa mwingine na wana hamu ya kufurahishnaa. Hata hivyo, ikiwa hatuna nia ya kuendelea na mazoea hayo, tunaingia kwenye mtego na kuchukuliana kikawaida. Kurejesha upendo kwa ndoa isiyo na upendo unawekuwa kwa kufanya jambo dogo baada ya lingine. Gundua lugha ya upendo ya mwenzi na fanya bidii ili kukidhi hitaji hilo kila siku.
Mkristo anapaswa kuitikia ndoa isiyo na upendo kwa kukataa kushiriki katika tabia zinazosababisha tatizo. Hata ikiwa mmoja wa wenzi wa ndoa haonyeshi haja ya kuanzisha tena uhusiano wa kihisia moyoni, Mkristo anapaswa kufanya lililo sawa. Hatujaitwa kulipiza kisasi au kurudisha ubaya kwa ubaya, bali kuushinda ubaya kwa wema (Warumi 12:21). Tumeitwa kutoka ulimwenguni ili tuwe wale walio katika nuru (Mathayo 5:14), chumvi ya dunia (Mathayo 5:13), na ukuhani uteule (1 Petro 2: 9-10). Dhamira yetu si kujifurahisha wenyewe bali kumpendeza Baba yetu wa mbinguni (1 Wakorintho 10:32). Anafurahi tunapovumilia magumu kwa subira na kufanya lolote tuwezalo ili kufufua ndoa isiyo na upendo.
English
Mkristo anapaswa kuitikiaje kwa kuwa katika ndoa isiyo na upendo?