Swali
Je! Ni dhambi kuwa na ndoto ya ngono?
Jibu
Ndoto ni matukio ya mvuto kwa akili ambayo hutokea wakati tunapolala. Katika Biblia, ndoto zilikuwa na maana kubwa na nyakati nyingine zilitumiwa na Mungu kuwafunulia watu ukweli (Mwanzo 40:8; Danieli 7:1; Mathayo 2:19). Biblia inarejelea ndoto na maono kwa kubadilishana, na mara nyingi watu wenyewe hawakuwa na uhakika ikiwa walikuwa wanaishi katika hali halisi au katika ndoto (soma Matendo 12:9). Hata hivyo, ndoto nyingi hazijaongozwa na Roho wa Mungu na zinaweza hata kuhusisha dhambi na mambo ya kutisha ya kila aina. Je, ni makosa kuota kuwa unatenda dhambi? Je! ni dhambi kuota ukiwa unafanya mambo ya ngono?
Wataalamu wa usingizi wanaweza kutupa maelezo ya kimwili kuhusu akili zetu tunapoota, lakini hakuna maelewano ya kutegemewa kuhusu ni kwa nini tunaota jinsi tunavyoota au ni nini kinachochochea mada fulani. Ndoto ni njia ya ubongo kuchakata habari na matukio, lakini mara nyingi hufanya hivyo kwa njia za nasibu na kiajabu. Matukio, watu, rangi, na hisia huonekana kuja pamoja bila mpangilio ili kuunda hadithi za kina ambazo hazileti maana yoyote wakati wa kuamka. Baadhi ya hadithi hizo zinahusisha vitendo vya ngono ambavyo mtu anayeota ndoto hawezi kamwe kujiingiza akiwa macho. Aina hizo za ndoto zinaweza kuleta hisia za hatia na aibu, ingawa hakuna hatua iliyochokuliwa.
Ingawa ni kweli huwa tunaota sana kuhusu mambo yale ambayo huwa katika akili zetu zilizoamka, huu sio ukweli kabisa. Mtu yeyote ambaye amewahi kuwa na ndoto ya kufanya jambo ambalo anaona ni la kuchukiza maadili anaelewa hili. Mtu ambaye anaota kuhusu kumtazama mwalimu wake wa darasa la tatu akicheza tenisi na mbweha haitaji kulaza kwenye kitengo cha magonjwa ya akili. Ilikuwa ni ndoto ya ajabu tu. Kadhalika, mwanamume anayejitahidi kuishi maisha matakatifu lakini anaota ndoto za kufanya mapenzi na msururu wa wanawake ambao hakuna kati yao ni bibi yake, haitaji kutubu. Wala mwanamke ambaye ana ndoto za kujamiana hahitaji kutubu kwa matendo yaliyofanywa katika ndoto hizo. Ilikuwa ni ndoto ya ajabu tu.
Hata hivyo, ikiwa ndoto hizo za ngono zilikuwa matokeo ya tamaa aliyokuwa nayo mchana, basi toba inaweza kuwa sahihi. Ikiwa ndoto za ngono zitakuwa za kufurahisha na kutamani, basi ni wakati wa kurudia maneno ya Yesu juu ya tamaa (Mathayo 5:28). Tunapoamka, ikiwa tunahisi vibaya juu ya kile tulikuwa tunaota, inafaa sikuzote kumwomba Mungu msamaha na kumwomba Mungu ayatakase mawazo yetu. Kusali Zaburi 19:14 zinapotokea kunaweza kufuta hisia za hatia na pia kurekebisha fikra zetu ili tusiendelee kufikira mawazo na picha zenye dhambi za ngono.
Ndoto pia zinaweza kuonyesha majitaji na matamanio ambayo hayaja kidhiwa, au hata matukio ya zamani, kwa hivyo, ikiwa aina fulani ya ndoto inatokea, inaweza kuwa ishara kwamba kuna eneo ambalo tunahitaji kushughukiwa na Bwana. Ikiwa ndoto hizo zinaendelea, inaweza kusaidia kuzungumza na mshauri wa Kikristo pia. Hatumfichi Mungu chochote; Anajua kuhusu ndoto zetu (Zaburi 139:2; 1 Mambo ya Nyakati 29:17). Hivyo, kuwa waaminifu kuhusu majitaji na matamanio yetu na kumwomba ayakidhi kwa njia za haki kunaweza kugeuza hata ndoto za ngono kuwa njia za ukuaji wa kiroho na kujisalimisha.
English
Je! Ni dhambi kuwa na ndoto ya ngono?