Swali
Neema ya pamoja (kwa wote ni nini)?
Jibu
Kanuni ya neema ya pamoja (watu wote) inahusu neema kuu ya Mungu iliyotolewa kwa wanadamu wote, haijalishi ikiwa wamechaguliwa au la. Kwa maneno mengine, Mungu daima ameweka neema Yake juu ya watu wote katika sehemu zote za dunia nyakati zote. Ingawa fundisho la neema ya pamoja limekuwa wazi sikuzote katika Maandiko, mnamo mwaka wa 1924, dhehebu la Christian Reformed Church (CRC) lilikubali fundisho la neema ya pamoja katika mkutano wa majimbo wa Kalamazoo (Michigan) na kuunda kile kinachojulikana kuwa “hoja tatu za neema ya pamoja.”
Jambo la kwanza linahusu nia nzuri ya Mungu kwa viumbe vyote, na sio kwa wateule tu pekee. “Bwana ni mwema kwa wote, ana huruma kwa vyote alivyovifanya” (Zaburi 145:9). Yesu alisema Mungu husababisha “Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu waovu na watu wema, naye huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki” (Mathayo 5:45). Na Mungu “yeye ni mwema kwa watu wasio na shukrani na kwa wale waovu” (Luka 6:35). Baraba na Paulo baadaye walisema mambo hayo: “Ameonyesha wema kwa kuwanyeshea mvua toka mbinguni na kuwapa mazao kwa majira yake, naye amewapa chakula tele na kuijaza mioyo yenu na furaha” (Matendo 14:17). Zaidi ya huruma, wema, na fadhali zake, Mungu pia anatoa subira yake kwa wateule na wasio wateule. Ingawa subira Yake kwa wale ambao Hajawachagua, Mungu bado huonyesha “ustahimilivu” kwa wale ambao Hajawachagua (Nahumu 1:3). Kila pumzi anayovuta mtu mwovu ni mfano wa huruma ya Mungu wetu mtakatifu.
Jambo la pili la neema ya pamoja ni kizuizi cha dhambi katika maisha ya mtu binafsi na katika jamii. Maandiko yamenakili Mungu akiingilia kati moja kwa moja na kuwazuia watu wasitende dhambi. Katika Mwanzo 20, Mungu alimzuia Abimeleki asimguse Sara, mkewe Ibrahimu, na akamthibitishia katika ndoto kwa kusema, “Ndiyo, najua ya kwamba umefanya haya kwa dhamiri safi, kwa hiyo nimekuzuia usinitende dhambi. Ndiyo sababu sikukuacha umguse” (Mwanzo 20:6). Mfano mwingine wa Mungu akizuia mioyo mibaya ya watu waovu inaonekana ni ulinzi wa Mungu kwa nchi ya Israeli dhidi ya kuvamiwa na mataifa ya kipagani kwenye mpaka wao. Mungu aliwaamuru wanaume wa Israeli kwamba mara tatu kwa mwaka wataacha shmba lao ili waende mbele zake (Kutoka 34:23). Ili kuhakikisha ulinzi kwa watu wa Mungu dhidi ya uvamizi katika nyakati hizi, ingawa mataifa ya kipagani yaliyowazunguka yalitamani nchi yao mwaka mzima, Mungu aliahidi kwamba, “wala hakuna mtu yeyote atakayeitamani nchi yako wakati unapokwenda mara tatu kila mwaka kuonana na Bwana Mungu wako” (Kutoka 34:24). Mungu pia alimzuia Daudi asilipize kisasi kwa Nabali kwa kuwadhiaki wajumbe ambao Daudi alituma kumsalimia Nabali (1 Samueli 25:14). Abigaili, mkewe Nabali, alitambua neema ya Mungu alipomsihi Daudi asilipize kisasi dhidi ya mumewe, “Basi sasa, kwa kuwa Bwana amekuzuia, wewe bwana wangu, kutokumwaga damu na kutolipiza kisasi kwa mikono yako mwenyewe… (1 Samueli 25:26). Daudi alitambua ukweli huu kwa kuitikia, “La sivyo, hakika kama Bwana, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye amenizuia nisiwadhuru….” (1 Samueli 25:34).
Hii hoja ya pili ya neema ya pamoja haijumuishi tu Mungu kuzuia uovu, bali pia kuachilia kwa ukuu wake kwa makusudi yake. Wakati Mungu anapofanya mioyo ya watu kuwa migumu (Kutoka 4:21; Yoshua 11:20; Isaya 63:17), Yeye hufanya hivyo kwa kuachilia kizuizi chake juu ya mioyo yao, na hivyo kuwaacha kwa dhambi inayoishi humo. Katika kuwaadhibu Waisraeli kwa uasi wao, Mungu aliwapeana “niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao wafuate mashauri yao wenyewe” (Zaburi 81:11-12). Kifungu cha Maandiko kinachojulikana zaidi kusungumzia juu ya Mungu kuachilia kizuizi kinapatikana katika Warumi ambapo Paulo anaelezea wale ambao wanakandamiza ukweli kwa uovu wao. Mungu “akawaachilia wafuate akili za upotovu, watende mambo yale yasiyostahili kutendwa” (Warumi 1:28).
Hoja ya tatu ya neema ya pamoja kama ilivyopitishwa na Christian Reformed Church (CRC) inahusu “haki za kiraia kwa wasiozaliwa upya.” Hii inamaanisha kwamba Mungu, bila kufanya upya mioyo yao, anafanya ushawishi wa namna hiyo hata mtu ambaye hajaokoka anawezeshwa kufanya matendo mema kwa wanadamu wanzake. Kama vile Paulo alivyosema kuhusu kundi la watu wa Mataifa ambalo halikuwa limezaliwa upya, wao “wanapofanya kwa asili mambo yatakiwayo na sheria, wao ni sheria kwa nafsi zao wenyewe, hata ingawa hawana sharia” (Warumi 2:14). Hitaji la Mungu kuzuia mioyo ya wale ambao hawajakombolewa inakuwa wazi wakati tunaelewa kanuni ya kibiblia ya upotovu kamili. Ikiwa Mungu hangezuia dhambi ambayo inakaa ndani mioyo ya wanadamu wote, mioyo ambayo ni “mdanganyifu na mwovu kupita kiasi” (Yeremia 17:9), ubinadamu ungejiangamiza wenyewe karne nyingi zilizopita. Lakini kwa sababu Anafanya kazikupitia neema ya pamoja iliyopewa watu wote, mpango mkuu wa Mungu kwa historia haukatizwi na mioyo yao mibaya. Katika kanuni ya neema ya pamoja, tunaona makusudi ya Mungu yakisimama, watu wake wakibarikiwa, na utukufu wake kutukuka.
English
Neema ya pamoja (kwa wote ni nini)?