settings icon
share icon
Swali

Je, kuna viwango tofauti vya adhabu jehanamu?

Jibu


Wazo kwamba kuna ngazi mbalimbali ya adhabu katika kuzimu linatokana hasa uigizaji wa uungu, ulioandikwa na Dante Alighieri kati ya 1308 na 1321. Katika shairi, mshairi wa Roma Virgil anamwongoza Dante kwa njia ya mzunguko tisa Jahannamu. Duru yazidi kuwa nyeusi, ikiwakilisha ongezeko la uovu kwa taratibu, na kilele ki katikati mwa nchi, ambapo Shetani amewekwa mateka. Kila mzunguko wenye dhambi wake wanaadhibiwa kwa mtindo unaopasa makosa yao. Kila mwenye dhambi anasumbuliwa milele na dhambi kuu aliyofanya. Kwa mujibu wa Dante, duru mbalimbali hutoka kwenye mzunguko wa kwanza, ambapo wanamokaa wenye hawajabatizwa na makafiri sugu, hadi kitovu cha kuzimu kimewekwa akiba kwa ajili ya wale ambao wamefanya dhambi kuu ya hila dhidi ya Mungu.

Ingawa hasa Biblia haisemi hivyo, inaonekana kuonyesha kuwa kuna ngazi mbalimbali za adhabu katika moto wa Jehanamu. Katika Ufunuo 20:11-15, watu watahukumiwa "kulingana na kile waliyoyafanya jinsi imeandikiwa katika vile vitabu" (Ufunuo 20:12). Watu wote katika hukumu hii, ingawa, wametupwa katika ziwa la moto (Ufunuo 20:13-15). Kwa hiyo, labda, madhumuni ya hukumu ni kuamua jinsi adhabu kali katika Jahannamu itakuwa. Kila kesi, hutupwa sehemu kidogo kidogo katika ziwa la moto sio faraja sana kwa wale ambao bado wamepotea milele.

Dalili nyingine huenda kuna ngazi mbalimbali za adhabu katika Jahannamu hupatikana katika maneno ya Yesu: "Na mtumwa Yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana. Na Yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwa huyo bitatakwa vingi; nay waliyemwekea amna vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi" (Luka 12:47-48).

Kiwango chochote cha adhabu kuzimu itakua nayo, ni wazi kuwa kuzimu ni mahali pa kuepukwa.

Kwa bahati mbaya, Biblia inasema kwamba watu wengi wateelekea Jahannamu: "Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maan mlango ni mpana na njia ni pana iendayo optoveuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachance" (Mathayo 7:13-14). Swali moja lazima mtu aulize ni "Niko katika barabara gani?" "wengi" katika barabara pana wana jambo moja pamoja -wao wote walimkataa Kristo kama njia moja pekee iendayo mbinguni. Yesu akasema, "Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi" (Yohana 14:6). Aliposema kuwa Yeye ni njia pekee, hiyo ni wazi ya chenye alimaanisha. Kila mtu afuataye "njia" nyingine badala ya Yesu Kristo ako katika barabara pana iendayo kuzimuni, na, hata kama mna au hamna ngazi mbalimbali ya adhabu katika kuzimu, mateso ni machungu, ya kutisha, ya milele, na yanaweza kuepukika.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kuna viwango tofauti vya adhabu jehanamu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries