settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Mungu atamtuma Yesu alipofanya? Kwa nini hakumtuma mapema? Kwa nini hakumtuma baadaye?

Jibu


Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria” (Wagalatia 4:4). Aya hii inasema ya kwamba Mungu Baba alimtuma Mwana wake "wakati ulipotimia." Kulikuwa na mambo mengi yaliyokuwa yakiendelea wakati wa karne ya kwanza kwamba, angalau kwa hoja za binadamu, wanaonekana kufanya hivyo ili ionekane bora zaidi Kristo kuja wakati huo.

1) Kulikuwa na tarajio kubwa sana kwa Wayahudi wa wakati huo kwamba Masihi atakuja. Utawala wa Kirumi juu ya Israeli uliwafanya Wayahudi kutamani kuja kwa Masihi.

2) Roma ilikwisha weka kwa pamoja dunia yote chini utawala wake, ndio ilete hisia za umoja kwa nchi mbalimbali. Pia, kwa sababu himaya ilikuwa na amani, usafiri ulikuwa rahisi, ukiruhusu Wakristo wa kwanza kueneza Injili. Kama uhuru wa kusafiri ingekuwa vigumu katika vipindi nyingine.

3) Wakati Roma ilikuwa ameshinda kijeshi, Ugiriki ilikuwa ameshinda kiutamaduni. Aina ya lugha "Kawaida" ya Kigiriki (tofauti na Kigiriki fasiri) ilikuwa lugha ya biashara na ilizungumzwa katika himaya, ikiifanya rahisi kwa kunena injili kwa vikundi vingi mbalimbali vya watu kwa kutumia lugha moja ya kawaida.

4) Ukweli kwamba sanamu nyingi za uongo zilishindwa kuwapa ushindi juu ya washindi wa Kirumi kuliwafanya wengi kuachana na ibada ya sanamu hizo. Wakati huo huo, katika mji "uliotamdunishwa" falsafa ya Kigiriki na sayansi ya wakati huo iliacha wengine kuwa tupu kiroho katika njia sawa na waaminio zaidi ya Mungu mmoja wa serikali ya ujmaa ambayo yaacha watu tupu kiroho hii leo.

5) Dini za siri za wakati huo zilisisitiza mungu mkombozi na ilihitaji waja kutoa sadaka ya umwagaji damu, na hivyo kufanya Injili ya Kristo ambayo ilihuzisha sadaka moja kuu ya kuaminika kwao. Watu wa mataifa mengine pia aliamini katika kutokufa kwa roho (lakini si kwa mwili).

6) Jeshi la Kirumi liliajiri askari kutoka kwa mikoa, ikiwafundisha watu hawa utamaduni wa Kirumi na mawazo yake (kama vile Injili) ambayo bado haikuwa imefikia mikoa ya nje. Mwanzo wa kuanzishwa kwa injili Uingereza ni matokeo ya juhudi ya askari Wakristo waiokuwa wamewekwa huko.

Kauli ya juu msingi wake umewekwa juu ya watu kuangalia wakati huo na kudadisi kuhusu ni kwa nini hatua hiyo hasa katika historia ulikuwa wakati mzuri kwa kuja kwake Kristo. Lakini sisi tunaelewa kwamba njia za Mungu si njia zetu (Isaya 55:8), na uenda hii inaweza au inaweza kosa kuwa baadhi ya sababu ambazo ni kwa nini alichagua wakati huo kutuma Mwana wake. Kutokana na muktadha ya Wagalatia 3 na 4, ni dhahiri kwamba Mungu alitaka kuweka msingi kwa njia ya Sheria ya Wayahudi ambayo ilikua inaandaa kuja kwa Masihi. Sheria ilikuwa na madhumni ya kuwasaidia watu kuelewa kina cha dhambi zao (kwa kuwa walikuwa hawana uwezo wa kutunza sheria) ili wapate urahisi zaidi kukubali tiba kwa ajili ya dhambi kwa njia ya Yesu Kristo (Wagalatia 3:22-23, Warumi 3:19- 20). Sheria pia "iliwekwa ili isimamie" (Wagalatia 3:24) kuongoza watu kwa Yesu kama Masihi. Ilifanya hivyo kupitia unabii wake wingi kuhusu Masihi Yesu ukitimia. Kuongeza mfumo huu wa kafara ambao ulilenga ile sadaka ya dhambi vile vile na upungufu wake mwenyewe (na kila sadaka daima wanaohitaji ndio baadaye ya ziada). Agano la Kale pia lilijenga picha ya mtu na kazi ya Kristo kupitia matukio kadhaa na sikukuu za kidini (kama vile nia ya Abrahamu kumtoa Isaka, au maelezo ya Pasaka wakati wa kutoka Misri, nakadhalika).

Hatimaye, Kristo alikuja katika wakati huo ili unabii utimizwe. Danieli 9:24-27 yasungumzia "Muda wa majuma sabini” au sabini na “saba” kutoka kwa muktadha haya “majuma” au “saba” yarejelea kikundi cha miaka saba, si siku saba. Tunaweza chunguza historian a kuorodhesha matukio yote ya majuma sitini na tisa (Juma la sabini litachukua wakati ujao). Siku Za kuesabika za majuma saba huanza na " kwenda nje ya amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu" ( mstari wa 25 ). Amri hii ilitolewa na Artashasta Longimanus katika mwaka wa 445 Kabla Yesu azaliwe (BC) (angalia Nehemia 2:5). Baada ya saba "saba" ongeza 62 saba saba, " au 69 x 7 miaka, unabii unataja, "Na baada yay ale majuma sitini na mawili, masihi atakataliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa” (maana uharibifu mkubwa) (aya ya 26). Hapa tuna kumbukumbu isiyo na kosa kuhus kifo cha Mwokozi juu ya msalaba. Karne moja iliyopita katika kitabu chake

Mfalme ajaye, Robert Anderson alitoa mahesabu ya kina ya majuma sitini na tisa, kwa kutumia 'miaka ya unabii,' kuruhusu ule mwak mfupi, makosa katika kalenda, mabadiliko kutoka BC hadi AD, nakadhalika, na akatamatisha kwamba juma sitini na tisa zilikamilika siku ile ile ya kuingia kwake Yesu katika Yerusalemu, siku tano kabla ya kifo chake. Kama mtu anatumia orodha hii au nyingine, uhakika ni kwamba muda wa Kristo kubadilika katika mwili washikana na unabii huu wa kina ambao ulinakiliwa na Danieli zaidi ya miaka mia tano kabla Yesu kuzaliwa.

Majira ya mwili wa Kristo ilikuwa kwamba watu wa wakati huo walikuwa tayari kwa kuja kwake. Watu wa kila karne tangu wakati huo na zaidi wako na ushahidi wa kutosha kwamba, hakika Yesu ndiye Masihi aliyeahidiwa na kupitia kwake maandiko yametimia ambayo yalilenga na kutabili kuja kwake kwa kina.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Mungu atamtuma Yesu alipofanya? Kwa nini hakumtuma mapema? Kwa nini hakumtuma baadaye?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries