Swali
Je, ni kwa nini nisamehe?
Jibu
Msamaha ni suala linalojulikana katika Biblia. Kwa hakika, mpango wa Mungu wa kuwasamehe wanadamu dhambi zao ndiyo mada kuu ya Biblia (1 Petro 1:20; Yohana 17:24). Kwa hiyo tunapojiuliza ni kwa nini tuwasamehe wale wanaotukosea, hatuhitaji kuangalia zaidi ya mfano ambao Mungu alitupa. Wakristo lazima wasamehe wengine kwa sababu Mungu ametusamehe (Waefeso 4:32).
Yesu alitoa mfano katika Mathayo 18:21-35 kuhusu ni kwa nini tunapaswa kusamehe. Anasimulia hadithi kutoka kwa mtazamo wa mfalme ambaye amemsamehe mtumishi wake deni kubwa. Lakini mtumishi huyo anakutana na mtumishi mwingine aliyekuwa na deni lake la hela chache, na mtumishi aliyesamehewa akawa mkali kwa mtumishi mwenzake na akamtaka alipe deni lake papo hapo. Mfalme alipojua kilichotokea, alikasirika na kuamuru yule ambaye aliyekuwa amesamehewa aadhibiwe mpaka deni kubwa ilipwe kabisa. Yesu anamalizia mfano huo kwa maneno haya ya kutia moyo: “Hivi ndivyo Baba yangu wa mbinguni atakavyomfanyia kila mmoja wenu ikiwa hatamsamehe ndugu yake kutoka moyoni mwake” (aya ya 35).
Msamaha ni jambo la lazima kwa wale wote ambao wamepokea msamaha wa Mungu (Waefeso 4:32). Yesu alitufunza tuombe, “Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tulivyokwisha kuwasamehe wadeni wetu” (Mathayo 6:12), akitukumbusha kwamba Mungu anatuwajibisha kwa ajili ya kulipa yale ambayo ametufanyia. Kukataa kuwasamehe wanaotukosea ni dharau kwa Mungu ambaye ametusamehe zaidi. Tunasamehe kama kitendo cha shukrani kwa yote ambayo tumesamehewa.
Wale ambao wamesamehewa na Mungu wanageuzwa na kuwa watu wa kusamehe. Kumkaribia Bwana na kuomba msamaha wake huku wakati huo huo unakataa kuwasamehe kaka na dada zetu ni kilele cha unafiki. Ikiwa mtu anayedai kuwa Mkristo anakataa kuwasamehe wengine, mtu huyo anaonyesha uthibitisho wa kwamba yeye kwa kweli hajazaliwa mara ya pili. Tunawasamehe wengine kwa sababu msamaha uu katika asili yetu mpya (angalia 1Yohana 3:9).
Msamaha sio kumwaacha mtenda dhambi bila kuwajibikia makosa yake. Bali ni kuwa tayari kuwaonea huruma wale waliotukosea. Tunaposamehe, tunajiweka huru kutoka katika utumwa ambao makosa ya mtu fulani yametutengenezea. Haiwezekani kushi kwa utii kamili kwa Mungu wakati mwingine anadhibiti hisia zetu. Wafuasi wa Yesu hawatawaliwi na chochote ila Roho Mtakatifu (Waefeso 5:18). Ili kukua kiroho na kushi kwa utii kwa Neno la Mungu, ni lazima tutii hata amri ngumu kuhusu msamaha (Luka 6:46).
Msamaha mara nyingi ni njia ambayo ulimwengu hutazama rehema ya Mungu. Tunaposamehe, tunaiga mafundisho ya Mungu juu ya fadhili, rehema, upendo, na unyenyekevu. Watu hawawezi kumwona Yesu ndani yetu wakati tunatembea katika uchungu na hasira. Wakati tunachoweza kuzungumza ni jinsi tulivyodhulumiwa, jinsi mtu fulani alivyotusaliti, au majeraha tuliyo nayo, tunapoteza utume wetu wa msingi, ambao ni kuwafanya wanafunzi (Mathayo 28:19). Kutosamehe hutufanya tujifikirie kibinafsi badala ya kumlenga Mungu na kuiba upendo wetu, amani, na furaha (ona Wagalatia 5:22).
Msamaha hufanyika kwa uepesi kwa wengine kuliko unavyo fanyika kwa wengine, lakini sisi wote tunahitajika kusamehe ikiwa tunataka kutembea katika ushirika na Mungu. Wengine hupata ugumu wa kusamehe kwa sababu hawaelewi maana ya kusamehe. Msamaha si sawa na upatanisho. Tunaweza kusamehe kutoka moyoni huku tukiwaweka mbali wasaliti. Msamaha hauruhusu wanyanyasaji wasiotubu warudi katika maisha yetu, lakini unaruhusu amani ya Mungu irudi katika maisha yetu.
Kutoka msalabani, Yesu aliomba kwa ajili ya waliomuua: “Baba wasamehe” (Luka 23:34). Tunaakisi Yesu wakati tunasamehe wale waliotukosea, na kwa waumini kuwa kama Yesu ndilo lengo kuu (Warumi 8:29).
English
Je, ni kwa nini nisamehe?