settings icon
share icon
Swali

Ni wakati gani, ni kwa nini na ni jinsi gani Bwana Mungu anatuadhibu wakati tunafanya dhambi?

Jibu


Nidhamu ya Bwana ni kweli mara nyingi - hupuuzwa na Waumini katika maisha. Sisi mara nyingi hulalamika kuhusu hali zetu bila kutambua kwamba hayo ni matokeo ya dhambi zetu wenyewe na ni sehemu ya upendo na neema ya nidhamu ya Bwana kwa ajili ya dhambi. Huu upumbavu wa ubinafsi unaweza kuchangia malezi ya dhambi ya mazoea katika maisha ya muumini, na kumuingiza katika nidhamu kubwa zaidi.

Nidhamu isichanganyishwe na adhabu baridi ya moyo. Nidhamu ya Bwana ni mwitikio wa upendo wake kwetu na hamu yake kwa kila mmoja wetu kuwa takatifu. "Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na Bwana wal usione ni taabu kurudiwa naye. Kwa kuwa Bwana ampendaye humrudi, kama vile baba mwanawe ampendezaye." (Mithali 3:11-12; ona pia Waebrania 12:5-11). Mungu atatumia hali, majaribio, na majanga mbalimbali kuturudisha kwake mwenyewe katika toba. Matokeo ya nidhamu yake ni imani na nguvu na uhusiano upya kwa Mungu (Yakobo 1:2-4),bila kutaja kuharibu mshikilia dhambi fulani uko nao juu yetu.

Nidhamu ya Bwana hufanya kazi kwa manufaa yetu wenyewe, ili aweze kutukuzwa kwa maisha yetu. Yeye anataka sisi tuonyesha maisha ya utakatifu, maisha ambayo yanadhihirisha hali mpya ambayo Mungu ametupa : "Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maan imeandikwa, Mtakauwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu "(1 Petro 1:15-16).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni wakati gani, ni kwa nini na ni jinsi gani Bwana Mungu anatuadhibu wakati tunafanya dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries