settings icon
share icon
Swali

Ombi la wokovu ni gani?

Jibu


Watu wengi wanauliza, “Kunalo ombi ninaweza kuomba liniakikishie wokovu wangu?” Ni muhimu kukumbuka kwamba wokovu haupokewi kwa kukariri maombi au kutaja maneno fulani. Hakuna mahali Biblia imeandikwa mtu alipata wokovu kwa kuomba. Kwa kusema maombi sio njia ya kibiblia ya wokovu.

Mtindo wa kibiblia wa wokovu ni imani katika Kristo Yesu. Yohana 3:16, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Wokovu unapatika kwa imani (Waefeso 2:8), kwa kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi (Yohana 1:12), na kwa kumwamini yeye pekee (Yohana 14:6; Matendo 2:8), sio kwa kukariri ombi.

Ujumbe wa kibilblia wa wokovu ni rahisi na wazi na vile vile ni wa kushangaza. Wote tumetenda dhambi kinyume na Mungu (Warumi 3:23). Mbali na Kristo Yesu hakuna mtu mwingine amewai ishi bila kutenda dhambi (Mhubiri 7:20). Kwa sababu ya dhambi zetu tumepata hukumu kutoka kwa Mungu (Warumi 6:23), na hukumu hiyo ni kifo cha mwili ambacho kinafuatwa na kifo cha kiroho. Kwa sababu ya dhambi zetu tunastahili adhabu, hakuna kitu tutafanya sisi wenyewe na kutufanya wasafi mbele za Mungu. Kwa ajili ya upendo wake kwetu Mungu akwa mwanadamu katika mwili wa Yesu Kristo. Yesu akaishi maisha makamilifu na kila mara akafunza ukweli. Ingawa wanadamu walimkataa Yesu na wakamwua kwa kumsulubisha. Kupitia kwa kitendo hicho kibaya Yesu akafa kwa ajili yetu (2Wakorintho 5:21). Baadaye Yesu akafufuka (1Wakorintho 15), kuthibitisha ya kwamba fidia yake kwa dhambi ilitosha na alikuwa amekwisha shida dhambi na mauti. Kwa ajili ya Yesu kutolewa kama dhabihu, Mungu anatupa wokovu kama tuzo. Mungu anatuita wote tubadilishe mawazo yetu kumhusu Yesu (Matendo 17:30) na kumpokea kama fidia ya dhambi zetu (1Yohana 2:2). Wokovu unapatikana kwa kupokea tuzo ambayo Mungu ameipeana, sio kwa kuomba ombi.

Sasa, hiyo haimanishi kuwa maombi hayawezi kuhuzishwa katika kupokea wokovu. Kama inaielewa injili, iamini kuwa ni kweli, na umpokee Yesu kama mwokozi wako, ni vizuri kunuia kudhihirisha imani hiyo kwa Mungu katika maombi. Kuwasiliana na Mungu kupitia kwa maombi kunaweza kuwa njia mojawapo ya kuendelea baada ya kumkubali Yesu na kuwa na imani kwake kama mwokozi wa maisha yako. Maombi yanaweza kuunganishwa na kile kitendo cha kuweka imani yako kwa Yesu pekee kwa wokovu.

Tena, ingawa ni muhimu kuwa msingi wa wokovu wako usiuweke kwa maombi ambayo imeyasema. Kukariri ombi hakuwezi kukuokoa. Kama unataka kupokea wokovu ambao unapatikana katika Yesu, weka imani yako kwake. Kikamilifu amini mauti yake kama dhabihu ya dhambi zako. Kwa vyo vyote vile mtegemee yeye pekee kama mwokozi wako. Huo ndio mtindo wa kibiblia wa wokovu. Kama umekwisha mpokea Yesu kama mwokozi wako kwa hali zote sema ombi kwa Mungu. Mwambie Mungu shukrani ikoje uliyo nayo kwa ajili ya Yesu. Toa sifa kwa Mungu kwa ajili ya upedo wake na dhabihu. Mshukuru Yesu kwa kufa kwa ajili ya dhambi zako na kuutoa wokovu kwa ajili yako. Huo ndio muunganiko wa kibiblia kati ya wokovu na maombi.

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ombi la wokovu ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries