Swali
Pepo waovu ni nini?
Jibu
Pepo waovu wanarejelewa katika Agano la Kale na Agano Mpya lakini mara nyingi wanaitwa majine mengine kama “ roho wachafu” au “roho najisi,” “roho wadanganyao” “roho wa uongo,” “roho wa kishetani,” na “pepo mbaya,”. Katika hali hizi zote, roho wabaya ni viumbe wasio wa ulimwengu wenye nia mbaya. Pepo waovu hufanya kazi kinyume na Mungu lakini Biblia inatujulisha kwamba Mungu katika ukuu wake anazweza kuchagua kutumia roho waovu kutekeleza mipango na makusudi yake, na hivyo kuonyesha kwamba yeye ni Mtawala wa ulimwengu wote.
Biblia haionyeshi chanzo cha pepo waouvu. Kuna uwezekano mkubwa kuwa wao ni malaika walioanguka pamoja na shetani (Mathayo 25:41; Ufunuo 12:7-9). Ingawa pepo waovu wapo kama kama sehemu ya uongozi wa uovu (Waefeso 6:12) shetani akiwa kiongozi wao (Mathayo 12:24), hawana uwezo wa kujiondoa kabisa kutoka utawala wa Mungu.
Pepo waovu wengi wanaotajwa katika agano la Kale walitumwa kutoka kwa Mungu kama adhabu kwa wanadamu wasiotii (1 Wafalme 22:20–23). Katika Waamuzi 9:23, roho mbaya alitumika na Mungu kumhukumu Abimeleki na kulipisha kisasi mauaji ya wana wa Gideoni. Mungu sio mwanzilishi wa uovu lakini anaweza kuruhusu nguvu za uovu, chini wa udhibiti wake kuleta matokeo fulani kulingana na mpango wake.
Bwana alituma roho muovu kuonyesha kwamba alikuwa amemkataa Sauli kama Mfalme. Roho mbaya ilimfanya Sauli kuwa na hasira na kukata tamaa. “Basi Roho wa Bwana alikuwa ameondoka kwa Sauli, nayo roho mbaya ikaachiwa nafasi na Bwana ili imtese. Watumishi wa Sauli wakamwambia, “Angalia, roho mbaya imeachiwa nafasi na nayo inakutesa’” (Samweli 16:14-15).
Katika Agano Jipya, neno pepo hutumika kwa kubadilishana na neno roho mbaya. Viumbe hawa waovu wanachafua na kuleta uovu kwa binadamu. Huenda nia yao ikawa kuleta madhara ya kimwili, ulemavu na ugonjwa badala ya maadili potovu.
Yesu alifukuza pepo wachafu kutoka kwa watu waliokuwa nao (Mathayo 8:16; Marko 5:1–13; 7:24–30) na akawapa wanafunzi wake uwezo wa kufanya hivyo kwa Jina lake (Mathayo 10:1; Matendo 5:12-16; 8:4-8;16:18). Pepo waovu wanamjua Yesu na wanajua kwamba atawahukumu wakati ujao (Mathayo 8:29; Marko 1:24; 5:7).
Katika wakati wa mwisho watu wengi watadanganywa na pepo waovu na mafundisho ya uongo ambayo wanashauri (1 Timotheo 4:1). Kitabu cha Ufunuo kinazungumzia Roho waovu wadanganyifu ambao watakua na jukumu kuu katika nyakati za mwisho: “Kisha nikaona roho wachafu watatu waliofanana na vyura wakitoka katika kinywa cha lile joka na katika kinywa cha yule mnyama na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Hizo ndizo roho za pepo wachafu zitendazo miujiza. Nazo huwaendea wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya tayari kwa ajili ya vita katika siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. “Tazama, naja kama mwizi! Amebarikiwa yeye akeshaye na kuziweka tayari nguo zake ili asiende uchi na kuonekana aibu yake.” Ndipo wakawakusanya wafalme pamoja mahali paitwapo Armagedoni kwa Kiebrania” Ufunuo 16:13–16).
Katika Luka 11:24–26,tunaona mfano wa pepo waovu ambao wanahusishwa na uovu wa kimaadili. Yesu anatoa mfano ili kuonyesha kwamba kushinda Shetani na kuondoa pepo waovu sio lengo kuu ya maisha ya Mkristo. Wanafunzi wa kweli ni lazima wafanye zaidi ya kuondoa pepo wachafu. Ili kuzuia uovu usikae katika nyumba zetu za kiroho ni lazima tujaze maisha yetu na mambo mema ya Mungu na Ufalme wake.
Pepo waovu hawapaswi kamwe kuzingatiwa kuwa katikati. Wao ni sehemu ya nguvu za giza za shetani, adui wa Mungu na watu wake. Pepo waovu huendeleza ufisadi, uovu na hasara duniani na katika wanadamu. Wanapinga utakatifu, wema, haki , nuru na upendo wa Mungu. Wao ni kinyume na Roho Mtakatifu kwa hivyo pepo waovu wanawakilisha kinyume cha tabia, asili na mapenzi ya Mungu. Wanachukia kazi ya Mungu na Yesu Kristo, na waumini wanapaswa kuwapinga daima: “ Mwe na kiasi na kukesha, maana adui yenu ibilisi huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mtu ili apate kummeza. Mpingeni, mkiwa thabiti katika imani” (1 Peter 5:8–9; tazama pia Waefeso 6:13; Yakobo 4:7).
English
Pepo waovu ni nini?