Swali
Sheria dhidi ya neema-ni kwa nini kuna mabishano mengi miongoni mwa wa Wakristo kuhusu suala hili?
Jibu
Upande mmoja unasema, “Wokovu ni kwa neema na neema pekee.” Upande mwingine unapinga, “Wazo hilo linaelekeza katika kuasi sheria. Kiwango cha uadilifu wa Mungu katika Sheria lazima kidumishwe.” Na mtu yeyote anaweza piga sauti kwa kusema, “Wokovu ni kwa neema, lakini neema inawajia wale ambao wanatii Sheria ya Mungu.” Msingi wa mjadala huo ni maoni tofauti juu ya msingi wa wokovu. Umuhimu wa suala hilo linasaidia kusisimua uzito wa madajadiliano.
Biblia inapozungumza kuhusu “sheria,” inarejelea kiwango cha kina ambacho Mungu alimpa Musa, kuanzia Kutoka 20 na Amri Kumi. Sheria ya Mungu ilieleza matakwa yake kwa watu watakatifu na ilitia ndani makundi matatu: sheria za kiuraia, utaratibu rasmi, na maadili. Sheria ilitolewa ili kuwatenganisha watu wa Mungu na mataifa maovu yaliyowazunguka na kufafanua dhambi (Ezra 10:11; Warumi 5:13; 7:7). Sheria ilionyesha wazi kwamba hakuna mwanadamu ambaye angeweza kujitakasa vya kutosha ili kumpendeza Mungu-yaani, Sheria ilifunua hitaji letu la Mwokozi.
Kufika nyakati za Agano Jipya, viongozi wa kidini walikuwa wameteka nyara Sheria na kuongeza ndani yake kanuni na desturi zao (Marko 7:7-9). Sheria yenyewe ilikuwa nzuri, lakini ilikuwa dhaifu kwamba ilikosa uwezo wa kubadili moyo wenye dhambi (Warumi 8:3). Kushika Sheria, kama ilivyotafsiriwa na Mafarisayo, ilikuwa ya kukandamiza na mzigo uliolemea (Luka 11:46).
Ilikuwa ni katika hali hii ya kuishika sheria ndipo Yesu alikuja, na halikuwa jambo kuepuka katika kukabiliana na waliosuluhisha sheria kinafiki. Lakini Yesu mtoa sheria, alisema, “Msidhani kwamba nimekuja kufuta Sheria au Manabii; sikuja kuondoa bali kutimiza” (Mathayo 5:17). Sheria haikuwa mbaya. Ilitumika kama kioo ili kufunua hali ya moyo wa mtu (Warumi 7:7). Yohana 1:17 inasema, “Kwa kuwa sheria ilitolewa kwa mkono wa Musa, lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo.” Yesu aliunganisha usawa kamili kati ya neema na Sheria (Yohana 1:14)
Mungu siku zote amekuwa mwingi wa neema (Zaburi 116:5; Yoeli 2:13), na watu daima wameokolewa kwa imani katika Mungu (Mwanzo 15:6). Mungu hakubadilika kati ya Agano la Kale na Agano Jipya (Hesabu 23:19; Zaburi 55:19). Mungu yule yule aliyetoa Sheria ndiye yule aliyemtoa Yesu(Yohana 3:16). Neema yake ilidhihirishwa kupitia mfumo Sheria wa dhabihu ili kufunika dhambi. Yesu alizaliwa “chini ya sheria” (Wagalatia 4:4) na akawa dhabihu ya mwisho ili kutimiza Sheria na kuanzisha Agano Jipya (Luka 22:20). Sasa kila mtu anayekuja kwa Mungu kupitia kwa Kristo anatangazwa kuwa mwadilifu (2 Wakorintho 5:21; 1 Petro 3:18; Waebrania 9:15).
Mvutano kati ya Yesu na waliojiona kuwa wenye haki uliibuka. Wengi wa walioishi kwa muda mrefu chini ya mfumo dhalimu wa Kifarisayo kwa tamanio kubwa walikubali rehema ya Kristo na uhuru alioutoa (Marko 2:15). Hata hivyo, baadhi, waliona onyesho hili jipya la neema kuwa hatari: ni nini kingemzuia mtu asitupilie mbali vizuizi vyote vya maadili? Paulo alishughulikia suala hili katika Warumi 6: “Tuseme nini basi? Je, tuendelee kutenda dhambi ili neema ipate kuongezeka? La hasha! Sisi tulioifia dhambi, tutawezaje kuendelea kuishi tena katika dhambi?” (aya ya 1-2). Paulo alifafanua kile ambacho Yesu alikuwa amefundisha: Sheria inatuonyesha kile ambacho Mungu anataka (utakatifu), na neema inatupa hamu na uwezo wa kuwa watakatifu. Badala ya kuitegemea Sheria kutuokoa, tunamwamini Kristo. Tunawekwa huru kutoka kwa utumwa wa Sheria kupitia dhabihu yake ya mara moja kwa wote (Warumi 7:6; 1 Petro 3:18).
Hakuna mvutano kati ya neema na Sheria. Kristo alitimiza Sheria kwa niaba yetu na anatoa uwezo wa Roho Mtakatifu, ambaye hutia nguvu nafsi iliyozaliwa upya kuishi katika kumtii Yeye (Mathayo 3:8; Matendo 1:8; 1 Wathesalonike 1:5; 2 Timotheo 1:14). Yakobo 2:26 inasema, “Kama vile ambavyo mwili pasipo roho umekufa, kadhalika nayo imani pasipo matendo imekufa.” Neema ambayo ina uwezo wa kuokoa pia ina uwezo wa kuhamasisha moyo wa dhambi kuelekea utauwa. Ambapo hakuna msukumo wa kuwa mcha Mungu, hakuna imani iokoayo.
Tumeokolewa kwa neema kupitia imani (Waefeso 2:8-9). Kuitunza Sheria hakuwezi mwokoa mtu yeyote (Warumi 3:20; Titus 3:5). Kwa kweli, wale wanaodai kuwa waadilifu kwa misingi ya kuitunza Sheria wao hufikiria kuwa wanailinda Sheria; hii ilikuwa mojawapo ya hoja za Yesu katika Mahubiri yake Mlimani (Mathayo 5:20-48; ona pia Luka 18:18-23).
Lengo la Sheria lilikuwa hasa kutuelekeza kwa Kristo (Wagalatia 3:24). Pindi tu tumeokolewa, Mungu anatamani kujitukuza Yeye mwenyewe kupitia metendo yetu mema (Mathayo 5:16; Waefeso 2:10). Kwa hivyo, metendo mema huandama wokovu; hayatangulii wokovu.
Mvutano kati ya “neema” na “Sheria” unaweza kuibuka wakati mtu 1) anakosa kuelewa lengo la Sheria; 2) anafafanua neema kuwa kitu kingine mbali na “ukarimu wa Mungu kwa mwenye hastahili” (ona Warumi 11:6); 3) anajaribu kupata wokovu kwa njia yake au “kuongezea” juu ya dhabihu ya Kristo; 4) anafuata njia potovu za Mafarisayo kwa kuchukua desturi za kibinadamu na mila katika mafundisho yake; au 5) anakosa kuangazia “ushauri wa Mungu pekee” (Matendo 20:27).
Wakati Roho Mtakatifu anaongoza kusoma kwetu kwa Maandiko, tunaweza “jitahidi kujionyesha kwa Mungu kuwa tumekubaliwa naye” (2 Timotheo 2:15) na kugundua uzuri wa neema inayokuza matendo mema.
English
Sheria dhidi ya neema-ni kwa nini kuna mabishano mengi miongoni mwa wa Wakristo kuhusu suala hili?