Swali
Je, namna gani, kwa nini, na ni lini Shetani alianguka kutoka mbinguni?
Jibu
Kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kimfano niv vile ilivyoelezwa katika Isaya 14:12-14 na Ezekieli 28:12-18. Wakati vifungu hivi viwili vinamaanisha hasa wafalme wa Babeli na Tiro, wao pia hurejelea nguvu za kiroho zinazo wasukuma wafalme hao, yaani, Shetani. Vifungu hivi huelezea kwa nini Shetani alianguka, lakini haisemi hasa wakati kuanguka kulitokea. Tunachojua ni hiki: Malaika waliumbwa kabla ya nchi (Ayubu 38:4-7). Shetani akaanguka kabla ya yeye kuwajaribu Adamu na Hawa katika bustani (Mwanzo 3:1-14). Kuanguka kwa Shetani, kwa hiyo, ni lazima kuwa kulitokea mahali fulani baada ya muda malaika waliumbwa na yeye kabla ya kuwajaribu Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni. Kama kuanguka kwa Shetani kulitokea dakika chache, masaa, au siku chache kabla ya yeye kuajaribu Adamu na Hawa katika bustani, maandiko hayasemi hasa.
Kitabu cha Ayubu chatuambia kwamba, kwa wakati angalau, Shetani bado alikuwa anaweza kuingia mbinguni, na kwa kiti cha enzi cha Mungu. "ilikuwa siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda katiyao. BWANA akmwuliza Shetani akamhibu BWNA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo." (Ayubu 1:6-7). Inavyoonekana wakati huo, Shetani alikuwa bado akitembea kwa uhuru mbinguni na duniani, akizungumza na Mungu moja kwa moja na kujibu kwa shughuli zake. Wakati ambapo Mungu alimkomesha kupata ruhusa ya kuingia mbinguni haijulikani.
Kwa nini Shetani alianguka kutoka mbinguni? Shetani alianguka kwa sababu ya kiburi. Alitamani kuwa Mungu, si kuwa mtumishi wa Mungu. Taarifa nyingi "Mimi ..." kauli katika Isaya 14:12-15. Ezekieli 28:12-15 inamwelezea Shetani kama malaika mzuri mno. Yawezekana kuwa Shetani alikuwa juu ya malaika, mzuri zaidi ya wote wa viumbe na Mungu, lakini hakuwa ameridhika katika nafasi yake. Badala yake, Shetani akataka kuwa Mungu, kwa kimsingi "kumtoa Mungu katika kiti chake cha enzi " na kuchukua utawala wa ulimwengu. Shetani alitaka kuwa Mungu, na cha kuvutia, ni kwamba hichi ndicho Shetani aliwajaribu Adamu na Hawa kwalo katika bustani mwa Edeni (Mwanzo 3:1-5). Shetani aliangukaje kutoka mbinguni? Kwa kweli, kuanguka si maelezo sahihi. Itakuwa mbali zaidi sahihi kusema kuwa Mungu alimtupa Shetani kutoka mbinguni (Isaya 14:15; Ezekieli 28:16-17). Shetani hakuanguka kutoka mbinguni, badala yake, Shetani alisukumwa kutoka mbinguni.
English
Je, namna gani, kwa nini, na ni lini Shetani alianguka kutoka mbinguni?