Swali
Je, Shetani ndiye mtawala wa jehanamu? Je, Shetani na mapepo yake huwaadhibu watu jehanamu?
Jibu
Kuna dhana potofu ambayo imezoeleka kwamba Shetani ndiye mtawala wa jehanamu na kwamba yeye na mapepo yake wanaishi humo na kutumia uma zao kutesa nafsi milele na milele. Dhana hii haina msingi wowote katika Maandiko. Kwa kweli, Shetani atakua mmoja wa wale watakaoteswa katika ziwa la moto, bali si yeye ndiye anatesa ( Ufunuo 20:10).
Ni wapi wazo la kuwa Shetani ndiye mtawala wa jehanamu linatoka, kama halitoki katika Biblia? Mawazo mengi ya uongo yanaweza kuwa yanatoka kwa shairi kuu la Dante Alighiere ‘The Divine Comedy’. Kazi nyingi za kisanaa na sehemu za fasihi kama vile riwaya ya Dan Brown ‘Inferno’ hufuata mwongozo wa Dante na kumwonyesha Shetani kama mtawala wa kuzimu.
Shairi la Dante linaelezea asili ya kikatili ya wenye dhambi katika ulimwengu. Dante anapita viwango tofauti vya kuzimu na toharani na hatimaye anafika paradiso. Shairi lenyewe lilikuwa mkusanyiko wa hekaya, mawazo ya kikatoliki(kama toharani), na mila za kiislamu kuhusu ‘usiku wa kupaa’ kwa Muhammed( lailat al-miraj). Mtazamo wa Dante kuhusu jehanamu unaathiriwa zaidi na Kurani kuliko Biblia.
Maono ya kifasihi ya Dante kuhusu jehanamu yameonyeshwa na Botticelli katika mchoro wake wa ramani ya kuzimu kama ardhi ya mateso, yenye mazingira mbaya ya moto, kiberiti, maji taka na zimwi, pamoja na Shetani mwenyewe akiwa ndani yake. Haya yote ni ya kutisha, na yenye ufanisi kama kazi ya sanaa, lakini inategemea na mawazo ya wanadamu, si Neno la Mungu.
Shetani si mtawala wa jehanamu. Ni Mungu ametawala. Yesu anasema, “Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, lakini baada ya hilo hawawezi kufanya lolote zaidi… Mwogopeni yule ambaye baada ya kuua mwili, ana mamlaka ya kuwatupa motoni. Naam, nawaambia, mwogopeni huyo!” (Luka 12:4-5). Yesu anamrejelea Mungu hapa. Yeye pekee ndiye aliye nakw uwezo wa kumtupa mtu jehanamu. Ni nani aliye na funguo za mauti na kuzimu? Yesu ana mamlaka kamili juu ya eneo hilo (Ufunuo 1:18). Yesu anawahakikishia waumini wote kuwa ata milango ya jehanamu haiwezi kushinda kanisa lake (Mathayo 16:18).
Ziwa la moto, ambalo limetajwa tu katika Ufunuo 19:20 na 20:10, 14-15, ni pahali pa mwisho pa adhabu kwa waasi wote wasiotubu, kwa malaika na mwanadamu (Mathayo 25:41).Adhabu ya ulimwengu kwa wale wote wanaomkataa Yesu Kristo kama mwokozi ni kutupwa katika ziwa la moto (Ufunuo 20:15).Biblia inazungumzia jehanamu kuwa pahali pa ‘’giza totoro’’ ambapo kutakuwa na ‘’kilio na kusaga meno’’ (Mathayo 8:12;22:13). Wale ambao majina yao yameandikwa katikan kitabu cha uzima cha Mwana kodoo hawafai kuogopa maafa haya mabaya. Kwa imani katika Kristo na damu yake iliyomwagika, tumekusudiwa kuishi milele katika uwepo wa Mungu.
Shetani hatawali jehanamu au kuongoza mapepo yake kuwatesa wale ambao wametupwa huko. Kwa kweli, Biblia haisemi kama Shetani ameenda jehanamu. Badala yake, “moto wa milele” unamngoja Shetani; pahali hapo paliumbwa ili kumwadhibuShetani na mapepo zake (Mathayo 25:41), bali si kuwapa ufalme wa kutawala.
Hadi shetani atakopohukumiwa na kutupwa katika shimo ilo milele, atakuwa akiishi kati ya mbingu (Ayubu 1:6-12) na dunia (1Petro 5:8). Hatakuwa na uhuru wa kutembea kila wakati, na anajua hilo. “ Kwa hiyo, furahini ninyi mbingu na wote wakaao humo! Lakini ole wenu nchi na bahari,
kwa maana huyo ibilisi ameshuka kwenu, akiwa amejaa ghadhabu, kwa sababu anajua ya kuwa muda wake ni mfupi! ”(Ufunuo 12:12).
English
Je, Shetani ndiye mtawala wa jehanamu? Je, Shetani na mapepo yake huwaadhibu watu jehanamu?